Kabla ya maisha kuwapiga Watu wengi Knockout, wengi walifikiri wakifika miaka 30 wangekuwa na nyumba na Gari

Ndio kikubwa uwe njiani tu usijifungie ndani maana mtu wa kukupa mchongo wa kutoka ni mmoja tu. Unakutana nae kwenye harakati zako tu.
Wewe hata kama humwamini Mungu wewe soma Biblia kama kujifunza maisha.

Ukiona kisa cha Musa kutokea na Mungu akiwa pembezoni mwa Bahari na kisha Mungu kumuuliza umeshika nini hapo nae kujibu nina fimbo na Mungu akamwabia piga hayo maji

Wana wa Israel uwavushe.

Hili ni somo kubwa

Ili bahati ikukute lazima kuna mazingira unatakiwa uyatengeneze na kuna namna ya kuwa.
 
Utajiri ni muhimu na unakupa uhuru wa kuishi popote. Sea wengi wetu maisha ya bongo tunaitafta susbsistence tu. Upate kula na kulala pazuri. Mengine yatajiongeza tu mkuu as long as unalala na kuamkia kwako.
 
Neno lako sio sheria
Kuna sehemu nimetaja maneno yangu ni sheria au unapachika vikolombwezo vyako?

Kama ulivyo mtazamo wako kwamba Mungu ndiye mpangaji wa maisha ya watu, Vivyo hivyo na mimi mtazamo wangu mungu huyo siyo mpangaji wa maisha ya binadamu.

Sasa ninyi mnachojaribu kufanya ni kuhalalisha dhana ya huyo Mungu wenu kwamba ndio mpangaji wa maisha ya kila mtu hapa duniani kumbe ni Uongo mtupu.
 
Kabisa mkuu 👏🏾👏🏾👏🏾👏🏾

Unaweza pambana sana ila kama hujapata mtu wa kukupeleka kwenye next level, uwezekano wa kubaki hapo hapo ni mkubwa

Japo, unaweza kutengeneza mazingira ya kukutana na hao watu ila uamuzi bado utakuwa ni wao katika kupiga push 👏🏾👏🏾
 
Watu wengi hawaamini Mungu na wana maisha mazuri tu , na kuna wanaoamini nakusali ila wamepigika vibaya sana .
Hasa hawa wanao jifanya kumtaja taja Mungu hapa kwenye huu uzi ndio life limewachapa vibaya mno.

Wako hapa kujifariji na umaskini wao kwamba ni mipango ya Mungu kwamba huenda kuna siku watafanikiwa.

Wanajifariji na fictional character Mungu...😄

Mtu yeyote anaye amini mafanikio ni "kudra za mwenyezi Mungu" huyo ni maskini wa akili na mali.

Hata akikosa kufanikiwa katika jambo fulani ata amini ni mungu ndiye kafanya hivyo kumbe ni mipango yake mibovu.
 
Kwa ninachokijua mimi mpaka sasa...mafanikio ni jambo pana sana...kuwa na nyumba na gari ni sehemu tu ya mafanikio...wapo wenye magari na nyumba lkn hawana watoto, wapo wenye magari na mali nyingine nyingi, ila wanaumwa...wapo wenye watoto wengi na familia zenye furaha ila hawana hayo magari na huenda wamepanga.
Nadhani tafsiri sahihi ya mafanikio ilenge eneo husika...e.g mafanikio kielemu, mafanikio kifedha, mafanikio kwenye mahusiano na kufanikiwa ktk eneo moja kati ya hayo, haina maana kuwa utafanikiwa ktk eneo jingine.
 
Mambo ya kumuomba we inakuuma nini
We siumesema hakuna Mungu sasa unachukizwa nini ukisikia mtu anasema anamuomba Mungu

Watu tumefanikiwa sababu ya Mungu na ushuhuda tunao aya kasirika
Na wewe unayejua Mungu huyo yupo, ina kuuma nini ukisikia nimesema hayupo?

Hata mimi nimefanikiwa pasipo msaada wowote wa huyo Mungu.
 
Sure
 
Na wewe unayejua Mungu huyo yupo, ina kuuma nini ukisikia nimesema hayupo?

Hata mimi nimefanikiwa pasipo msaada wowote wa huyo Mungu.
Mimi hainiumi wewe kusema hakuna Mungu
Ila tofauti yangu mimi na wewe ni kwamba mtu akisema hamna Mungu simshambulii

We sasa mtu akisema Mungu yupo unakua mbogo
 
Point.
 
Roadmap ya mwanadamu iliyochorwa na Mungu, inawahusu wanadamu ambao wameji 'aline' kwenye mipango na makusudi ya Mungu.
Hawa ni binadamu adimu sana kupatikana katika kipindi hiki.
Wengi wetu, tunamfanya Mungu abadilishe mipango na makusudi yake kwetu kila wakati kutokana na kukosa msimamo thabiti.
Maana unapozaliwa, Mungu ana road map ya maisha Yako yote hapa duniani, utaenda na hii TU iwapo utatembea na Mungu maishani ukimtii Kwa kila jambo(hata kama halikuingii akilini.)
Pale utakapobadilika ukaenda kinyume na maagizo na maelekezo ya Mungu, roadmap hubadilika kutoka kwenye mipango ya maisha kuja mipango ya kukuokoa., na kinyume chake.
Hapo utaona wanadamu wengi (including walokole) tumekuwa hatuna stable roadmap sababu ya kuwa vuguvugu. Kila wakati tunabadilisha roadmap, na kumbuka kila inapobadilika unaanza upya.
Hapa utaona kwamba, watu rahisi kufanikiwa kupitia roadmap ya Mungu ni wale wasiokuwa na time kabisa na Mungu(ambapo Mungu anakuwa roadmap stable kwao akitafuta namna ya kuwarejesha kwake, na wengine ni wale (wachache sana) wanaomtii na kimfuata Mungu Kwa kila neno, ambapo wanapata stability Kwa Mungu katika kufanikisha mipango yao na hasa ya kumtumikia yeye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…