Kabla ya maisha kuwapiga Watu wengi Knockout, wengi walifikiri wakifika miaka 30 wangekuwa na nyumba na Gari

Kabla ya maisha kuwapiga Watu wengi Knockout, wengi walifikiri wakifika miaka 30 wangekuwa na nyumba na Gari

Lakini mbona wapo watu wengi ni wapagani hawamjuwi Mungu, hawahudhurii makanisani wala misikitini na bado ni matajiri wa kutupwa?
Mimi kwangu mafanikio ni muunganiko wa mambo matatu.

1.Uwepo wa watu sahihi waliokuzunguka.
2.Uwezo binafsi ama utayari.
3.Bahati ya mtu.

Hayo matatu ndio yanafanya watu wafanikiwe at most cases. Kusema Mungu ndio anawapa mafanikio watu wanaomuamini hilo sina hakika nalo sana maana kuna watu wanakufuru kinoma na ndio wana hela chafu. Mtu anamgonga mama yake mzazi kila mwezi.
 
Mungu ndio hukupa hiyo roho ya jitihada ili akupe bahati yako.
Unafikiri spirit ya mtu kufanya kazi inatoka wapi?
Lakini pia mtu asipokuwa na ari ya kufanya kazi Unafikiri hiyo inatokana na nini?

Unaposema Mungu unamaanisha chanzo cha yote uyajuayo na yale usiyoyajua. Yawe mazuri au Mabaya. Yeye ndiye mbunifu, mtunzi na muimbaji wa kila kitu.
Hayo mabaya na mazuri unamaanisha mema na dhambi ??

Lengo la Mungu mwisho wa yote ni kuupata uzima wa milelle, hivyo Mungu hawezi kukupatia mafanikio/kukuonesha njia ya mafanikio ambayo mwisho wa siku yatakupoteza na kukuangamiza/kukufanya uukose uzima wa milele. Hapo hata ufanye bidii na juhudi kiasi gani hautotoboa kamwe (kama u wa Mungu kweli).
 
Kwanini unawaza kufika hiyo hatua ya kukosa kodi?

Maisha ni kuwa na PESA bank na cash flow na hisa kadhaa
Umebarikiwa kuwa na vyote hivyo shukuru Mungu. Kuna wenzio ambao hawajui hata siku inaishaje. Tunatakiwa tuishi tukiwaza kwa namna hio sababu dunia haina usawa. Mbaya zaidi tumewapa dhamana watu wenye aina yako ya ufikiri ndio maana leo bongo iko ilivyo.
 
Mbona watu wanoishi dunia ya kwanza wanatimiza hayo malengo Kama nyumba ,gari na kuwa na familia nzuri under 30 yrs.


Mimi naamini katika MUNGU Ila pia naamini MTU kuishi below the average hutokana na mindset na mifumo ya nchi husika.
Hapo kwenye mifumo ya nchi husika ndio umepiga penyewe. Hatuwezi kuharibu mifumo mizuri ya vijana kufanikiwa, kuendekeza mifumo mibovu isiorafiki kwa vijana kutoboa afu tuje tumlaumu Mungu au tukomae kwamba Mungu ndie moangaji wa yote akati yeye mwenyewe alitupatia akili na utashi wa kupambana na kuendesha mambo yetu wenyewe.
 
Umebarikiwa kuwa na vyote hivyo shukuru Mungu. Kuna wenzio ambao hawajui hata siku inaishaje. Tunatakiwa tuishi tukiwaza kwa namna hio sababu dunia haina usawa. Mbaya zaidi tumewapa dhamana watu wenye aina hio ya ufikiri ndio maana leo bongo iko ilivyo.



Unakumbuka ulikuwa unasema tuwe na positive thinking tusiwaze kukosa bali kupata na ukadenda mbali na kusema tutumie positive affirmation.


Nadhani kwa masomo yako ya nyuma ni sahihi

Your" thought become things"
 
Kwanini kila mada ya Mungu unapata uchungu sana
Wewe humuamini Mungu una haki hiyo move on lakin kila ukisikia mambo ya Mungu unatokwa na povu una shida mahali
Nakwambia hivi [emoji116]

Habari za kusema vijana hawafanikiwi kwa sababu eti hawamuombi Mungu ni uongo.

Kuna kundi kubwa la vijana wanasali na kumuomba huyo Mungu wafanikiwe lakini bado vijana hao ni maskini choka mbaya.

Hakuna uhusiano wowote wa mtu kufanikiwa na huyo Mungu.

Kuunganisha mafanikio ya mtu na Mungu ni dhana ya uongo isiyo na mantiki

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Sijui ndio ridhki ama ndio zali, bahati, uwezo binafsi au nyota ya mtu..

Ila nilichokisoma kwenye life, unahitaji mtu wa kukuinua maana hata Mungu hashuki chini kuja kukuinua ila hutumia watu.

Nimekutana na watu ambao wapo hardworking, passionate, God fearing, talented and skilled yaani wana kila sifa za kutoboa ila hawajapata sehemu na watu sahihi wa kuwainua

Halafu kuna wale ambao ni average tu na wengine ni wavivu pasee kama hawa tunaokutana nao kwenye ofisi za umma lakini wanatoboa kwa sababu wapo kwenye system lakini pia wana back up

Kwa hiyo maisha ukiyafikiria kiundani utakosa majibu ila cha msingi uishi tu
Life is not predictable.

Kikubwa fanya kazi kwa bidii na nidhamu ya pesa kuwa nayo.

Ukweli ni kwamba mtu anaekuja kukupa deal ni mtu mmoja tu na kupitia hapo unakuwa mtu mwingine tofauti kabisa kiuchumi
.
Hili nimejifunza kwa watu wangu wengi wa karibu walikuja kuinuliwa na watu

Hapa ndipo nilijifunza kwa udhiirisho kwamba mtu huinuliwa na mtu kupitia ukuu wa Mungu.


Hata mtu unae muona leo ana maisha mazuri ukifuatilia utakuta alikuwa kwnye harakati zake ghafla akatokea mtu akamshirikisha ndio ukawa mwanzo wa kutoka.

Kadhalika wahalifu nao hupiga tukio moja tu na kupitia hapo ndio mwanzo wa kutoka.

So pambana lift itakukuta njiani.
 
Kuwa Mlokole au mwenye haki hakukufanyi ufanikiwe.
Unafanikiwa kwa sababu Mungu ndiye ameamua ufanikiwe.
Waliofanikiwa wengi wao wanakiri kuwa hawakutegemea kama wangefanikiwa. Yaani wanaita ni bahati.

Wengi wanaofeli wanafeli kwa sababu wanaamini katika uwezo wao wenyewe.

Tafuta waliofanikiwa wote wanafanana katika jambo moja. Kuamini kuwa mafanikio ni majaliwa ya Mungu
For sure
Wakati wa Mungu ukifika hakuna wa kuzuia haijalishi wewe unakesha kanisani au lah!

Mimi nimeshuhudiwa watu ambao hawamjui Mungu kwa kiwango nilichonacho lakini wamefanikiwa na imani yao hiyo hiyo.
 
Back
Top Bottom