Kabla ya maisha kuwapiga Watu wengi Knockout, wengi walifikiri wakifika miaka 30 wangekuwa na nyumba na Gari

Kabla ya maisha kuwapiga Watu wengi Knockout, wengi walifikiri wakifika miaka 30 wangekuwa na nyumba na Gari

Baada ya mambo ya mzee wangu kuzingua mwaka 2009 nikiwa nasubiri kwenda chuo nikajisemea hapa sasa kazi imeanza. Tangu kipindi hicho sikuwahi kujiwekea time frame ya kufanikiwa wala kuumia sababu ya mafanikio ya ninaowafahamu hata nisio wafahamu. Mwaka 2012 kwa kuunga unga nilitakiwa niingie chuo IFM, tatizo likawa ada ikanibidi niahirishe masomo mpaka mwaka unaofuata.

Mwaka uliofuata nikasajiliwa nikaanza masomo, semister ya pili ikashindikana kuimaliza kwa jambo lile lile la ada, nikasimama tena na ndio ikawa nitolee mpaka leo. Sijawahi kujuta wala kumlaumu yeyote yule kwa hiki nilichokipitia na nimekuja kujikuta naishi maisha matamu sana, sijafanikiwa kupata pesa nyingi ila hivi vilaki mbili tatu havinipigi chenga.
 
Ahaaa 😁😁😁shusha madini
Gape ya maskin na tajiri ni calculative. Inawez kupunguzwa vizur kabisa bila ya uwepo wa mungu katikati.

So, mafanikio kwa namna Fulani yanawezekana hata below 20s. Lakin hii ni ngum kutokea kwa nchi hizi za third world mana mfumo ule ule wa kibepari huku umekuwa nganganga.

Sio talent, sio elimu Wala biashara hali huku ni tete. So, mifumo yenyew ilivyo tu si rafiki. Elimu utaiona invalid, inefficient na Haina uwezo wa kumvusha kijana walau kujitegemea tu bila nguvu ya ziada. Angalia pia kwenye talent na biashara. Kilimo nchi hii kwenye makaratas ni backbone lakin kiuhalisia ni neglected sectoral.

Kuna muda Hawa wanaoamin kwamba Afrika kuungana na kujitegemea ni suluhu la kuendelea kwa Afrika wako sahihi. Umaskin unaletwa na utegemez wa nje ndo huo unaochagiza umaskin wa mtu mmoja mmoja. Hili suala la mafanikio katika umri mdogo ninla mfumo zaidi .. nchi za ulaya ni tajiri na hizohizo Leo hii kijana wa miaka 21 tayari bilionea kutokana na kipaji chake tu. Hii haiwez kutokea kwa third world
 
Waafrika.
Tembea uone.
Wazungu walioamua kumwamini Mungu wanamwamini kweli kweli.
Kwani hakuna waafrika walio amua kumwamini Mungu kwelikweli?
Kinachotuponza waafrika ni kwamba, hata wale tunaomwamini Mungu, wengi wetu hatuna uthabiti wa Imani,
Kwani wazungu wote wanao mwamini mungu wana uthabiti wa imani?

Hivi huko shuleni ulienda kusomea ujinga?

Thinking capacity yako iko sawa kweli?
 
Gape ya maskin na tajiri ni calculative. Inawez kupunguzwa vizur kabisa bila ya uwepo wa mungu katikati.
NAKAZIA 📌🔨

Hawa wanao husanisha mungu na mafanikio ya watu hawafikirii sawasawa.

Hawaangalii sera mbovu, siasa uchwara na mazingira ya rushwa yaliyopo Afrika yanayo kwamisha fursa na usawa kwa vijana wengi.
So, mafanikio kwa namna Fulani yanawezekana hata below 20s. Lakin hii ni ngum kutokea kwa nchi hizi za third world mana mfumo ule ule wa kibepari huku umekuwa nganganga.

Sio talent, sio elimu Wala biashara hali huku ni tete. So, mifumo yenyew ilivyo tu si rafiki. Elimu utaiona invalid, inefficient na Haina uwezo wa kumvusha kijana walau kujitegemea tu bila nguvu ya ziada. Angalia pia kwenye talent na biashara. Kilimo nchi hii kwenye makaratas ni backbone lakin kiuhalisia ni neglected sectoral.

Kuna muda Hawa wanaoamin kwamba Afrika kuungana na kujitegemea ni suluhu la kuendelea kwa Afrika wako sahihi. Umaskin unaletwa na utegemez wa nje ndo huo unaochagiza umaskin wa mtu mmoja mmoja. Hili suala la mafanikio katika umri mdogo ninla mfumo zaidi .. nchi za ulaya ni tajiri na hizohizo Leo hii kijana wa miaka 21 tayari bilionea kutokana na kipaji chake tu. Hii haiwez kutokea kwa third world
 
Tembea uone.

Kwani hakuna waafrika walio amua kumwamini Mungu kwelikweli?

Kwani wazungu wote wanao mwamini mungu wana uthabiti wa imani?

Hivi huko shuleni ulienda kusomea ujinga?

Thinking capacity yako iko sawa kweli?
Ni wachache sana, ikilinganishwa na wazungu Kwa uwiano.

Sijawahi kusoma shule, ila thinking capacity yangu ni kubwa kuliko wewe uliesoma chuo Cha madrasa al nudha.
 
Sikubaliani na hoja kuwa mipango ya kimaisha ya vijana wengi inaharibika kwasabb hawamhusishi ama hawamuombi Mungu. Wapo walokole ama mashekhe promax wamefika 50 bado hawana hata kitanda.

Kila mtu ana FATE yake, yaani Kila mtu kachorewa roadmap ya maisha yake na mwenyezi Mungu. Ndiyo maana akina Laizer wanaokota tanzanite yenye thamani ya mabilioni wakati wengine hata mia mbovu hamuokoti.
Anaokota sio....yani mtu aokote Madini
 
Hasa hawa wanao jifanya kumtaja taja Mungu hapa kwenye huu uzi ndio life limewachapa vibaya mno.

Wako hapa kujifariji na umaskini wao kwamba ni mipango ya Mungu kwamba huenda kuna siku watafanikiwa.

Wanajifariji na fictional character Mungu...😄

Mtu yeyote anaye amini mafanikio ni "kudra za mwenyezi Mungu" huyo ni maskini wa akili na mali.

Hata akikosa kufanikiwa katika jambo fulani ata amini ni mungu ndiye kafanya hivyo kumbe ni mipango yake mibovu.
Ukifuatilia ktk historia dini zililetwa ili kuwapa watu waliojikatia tamaa tumaini la kuishi. Watu wengi humkimbilia mungu kama sehemu ya kutuliza moyo wakiamini anaweza kuwatoa kwenye kiza kinene walichopo. Ni kama madawa ya kulevya, muda unaoyatumia yanakuweka kwenye ulimwengu wa kufikirika, unajiona ukiwa ktk hali ambayo matatizo yako yote hayapo, baada ya kurudi ktk uhalisia ndiyo unakumbuka kuwa bado matatizo yako yapo palepale. Ndiyo kama ilivyo dhana ya dini na mungu, wengi wanajifariji kwa kumuachia mungu awaamulie hatima ya maisha yao matokeo yake wanaweza kwenda miaka nenda, miaka rudi hawapigi hatua yoyote ile kwenye maisha ila kwasababu upendo kwa mungu umeshakolea wataamini ndiyo maisha waliyopangiwa.

Mimi naamini ili mwanadamu uweze kufikia your full potential kuna mifumo ya kidunia unapaswa kupishana nayo, yaani usifuatane nayo. Mojawapo ni imani ktk mungu na dini, watu waliojinasua ktk imani hizi wanayatazama maisha kwa mlengo tofauti kabisa.
 
Ukifuatilia ktk historia dini zililetwa ili kuwapa watu waliojikatia tamaa tumaini la kuishi. Watu wengi humkimbilia mungu kama sehemu ya kutuliza moyo wakiamini anaweza kuwatoa kwenye kiza kinene walichopo. Ni kama madawa ya kulevya, muda unaoyatumia yanakuweka kwenye ulimwengu wa kufikirika, unajiona ukiwa ktk hali ambayo matatizo yako yote hayapo, baada ya kurudi ktk uhalisia ndiyo unakumbuka kuwa bado matatizo yako yapo palepale. Ndiyo kama ilivyo dhana ya dini na mungu, wengi wanajifariji kwa kumuachia mungu awaamulie hatima ya maisha yao matokeo yake wanaweza kwenda miaka nenda, miaka rudi hawapigi hatua yoyote ile kwenye maisha ila kwasababu upendo kwa mungu umeshakolea wataamini ndiyo maisha waliyopangiwa.

Mimi naamini ili mwanadamu uweze kutumia your full potential kuna mifumo ya kidunia unapaswa kupishana nayo, yaani usifuatane nayo. Mojawapo ni imani ktk mungu na dini, watu waliojinasua ktk imani hizi wanayatazama maisha kwa mlengo tofauti kabisa.
Kabisa mkuu.
 
Kwa ninachokijua mimi mpaka sasa...mafanikio ni jambo pana sana...kuwa na nyumba na gari ni sehemu tu ya mafanikio...wapo wenye magari na nyumba lkn hawana watoto, wapo wenye magari na mali nyingine nyingi, ila wanaumwa...wapo wenye watoto wengi na familia zenye furaha ila hawana hayo magari na huenda wamepanga.
Nadhani tafsiri sahihi ya mafanikio ilenge eneo husika...e.g mafanikio kielemu, mafanikio kifedha, mafanikio kwenye mahusiano na kufanikiwa ktk eneo moja kati ya hayo, haina maana kuwa utafanikiwa ktk eneo jingine.

Kwa wagonjwa kuwa na afya ndio mafanikio
 
Back
Top Bottom