Ukifuatilia ktk historia dini zililetwa ili kuwapa watu waliojikatia tamaa tumaini la kuishi. Watu wengi humkimbilia mungu kama sehemu ya kutuliza moyo wakiamini anaweza kuwatoa kwenye kiza kinene walichopo. Ni kama madawa ya kulevya, muda unaoyatumia yanakuweka kwenye ulimwengu wa kufikirika, unajiona ukiwa ktk hali ambayo matatizo yako yote hayapo, baada ya kurudi ktk uhalisia ndiyo unakumbuka kuwa bado matatizo yako yapo palepale. Ndiyo kama ilivyo dhana ya dini na mungu, wengi wanajifariji kwa kumuachia mungu awaamulie hatima ya maisha yao matokeo yake wanaweza kwenda miaka nenda, miaka rudi hawapigi hatua yoyote ile kwenye maisha ila kwasababu upendo kwa mungu umeshakolea wataamini ndiyo maisha waliyopangiwa.
Mimi naamini ili mwanadamu uweze kutumia your full potential kuna mifumo ya kidunia unapaswa kupishana nayo, yaani usifuatane nayo. Mojawapo ni imani ktk mungu na dini, watu waliojinasua ktk imani hizi wanayatazama maisha kwa mlengo tofauti kabisa.