Kabla ya maisha kuwapiga Watu wengi Knockout, wengi walifikiri wakifika miaka 30 wangekuwa na nyumba na Gari

Kabla ya maisha kuwapiga Watu wengi Knockout, wengi walifikiri wakifika miaka 30 wangekuwa na nyumba na Gari

Shida tupo kwenye mifumo ambayo inataka watu watumie akili zaidi kuliko nguvu mafanikio kwa sasa hayawafuati watu wanaojituma wenye skills ndio wanaotoboa mfano ingia playstore mtu kajifungi geto anatengeneza App inayoenda kutengeneza mabilioni ya pesa kazi ndogo matokeo makubwa

Kitu kingine hauhitaji kujipa stress kuchelewa kujenga ama kuwa na gari jambo msingi swala la mafanikio kwenye maisha ni kujikita kutafuta njia zitakazo kupa matokeo makubwa na sio kuonekana unafanya vitu kwa wakati
Sidhani na sina uhakika kuwa kutengeneza App ni kazi ndogo...lazima ujiandae vyakutosha!
 
Okay..ujionavyo ndivyo huwa!. Am different from your perspectives
Mimi nikiwa nina urefu wa 6,3ft nikajiona mbilikimo, kujiona kwangu hakutanipunguzia height kuwa size ya mbilikimo.

Mimi nikiwa masikini, nikijiona tajiri, kujiona kwangu tajiri, hakutanifanya niwe millionaire.

Kuna facts na opinions.

Mimi kutokuwa na same ground na riz1 ni fact sio opinion.
 
Mimi nikiwa nina urefu wa 6,3ft nikajiona mbilikimo, kujiona kwangu hakutanipunguzia height kuwa size ya mbilikimo.

Mimi nikiwa masikini, nikijiona tajiri, kujiona kwangu tajiri, hakutanifanya niwe millionaire.

Kuna facts na opinions.

Mimi kutokuwa na same ground na riz1 ni fact sio opinion.
Pole kwa mara nyingine tena mkuu
 
Habari za Jumapili!

Maisha sio Pouwa! Nakubaliana na wale wanaosema Maisha ni majaliwa. Na jitihada hazizidi kudura.

Wapo waliosoma kwa bidii mila hiyo na waliona taa ya matumaini kulingana na matokeo ya darasani waliyokuwa wakiyapata. Waliamini kuwa maisha yao na hatma yao ipo mikononi mwao kumbe sivyo.

Ilifika hatua wakawa wanadharau wale ambao walikuwa wanaonekana hawana mipango na mikakati kutokana na kutoipenda shule.

Wengi walifikiri kuwa kabla ya miaka 30 tayari wangekuwa wamekomesha jeuri na kiburi cha Umaskini katika maisha yao.
Tayari kichwani walikuwa na picha za jumba kubwa la kifahari ambalo walijua ndio watakayoishi. Bongo zao zilishakuwa na miundombinu ya flyover ambapo gari yao ilikuwa ikipita juu yake huku ndani akiwa yeye na Pisikali moja matata ambayo ndio mkewe.

Kwa wasichana, wao nao walikuwa na maisha yao mazuri katika vichwa vyao. Wanaume Handsome, warefu na wenye vipato na Watanashati walikuwa katika fikra zao.

Sasa miaka imekimbia, hawaelewi nini kimetokea. Matumaini yameyoyoma, ngumi ya matumpa upper cut moja matata imepiga kidevu vijana chali.
Hata zile ramani za majengo na magari walizokuwa nazo miaka hiyo zimefutika.

Yule Mwanamke mrembo akilini waliyemfikiria wangekuja kumuoa wanawaona kwenye magazeti, filamu na kwenye riwaya. Hakuna faraja tena, tumaini limeota mbawa. Wamejiunga kwenye chama cha faraja ya mpito cha Kataa Ndoa.
Hawakumbiki tena ndoto ya kuwa na familia bora baada ya kuyapata maisha mazuri yanayotamanika.
Ni Tekniko Knockout.

Hawakujua kuwa maisha yanakupa yale ambayo hujayaomba na yale ambayo huyataki. Tena maisha hukupa yale ambayo hukudhania kwamba ungekuwa nayo. Kwa sababu maisha ni Nasibu, maisha ni bahati tuu.

Sasa mipango imevurugwa na kuvurugika. Kila kitu pangala pangala! Hata kupanga hawataki kupanga tena. Hata wakisema wapange wanaona wanapoteza muda wao. Sasa ni bora liende túu! Wapo tayari kwa lolote na huo ndio mfumo wa maisha unavyotaka.

Mtu ambaye alipanga kabla ya miaka 30 awe na jumba na gari leo hii hata kodi ya chumba cha laki moja hawezi kuhimili. Unaweza kuona pigo alilopigwa ni zito kwa kiwango kipi.

Kijana, unapopanga mipango yako. Muombe Mungu

Suleiman aliwahi kusema;

Mhubiri 9:11 NEN​

Nimeona kitu kingine tena chini ya jua: Si wenye mbio washindao mashindano au wenye nguvu washindao vita, wala si wenye hekima wapatao chakula au wenye akili nyingi wapatao mali, wala wenye elimu wapatao upendeleo, lakini fursa huwapata wote.


Acha Nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Tz kila kitu bahati nasibu. Walioendelea duniani huko, mtoto wa miaka 18 ana gari.
 
Je, unaijua kesho yako itakuaje ?..

Je, unaweza kuamua kesho utakutana na nani au lipi ?...

Kama nikikurudisha 5 years back, je hapo ulipo ndipo ulipotaka kuwa kwa kitu ukifanyacho na kwa level uliyoifikia ?..

What I know, binadamu tuna control mchakato tu ili tuweze influence results ila hatuna UBAVU wa kutengeneza matokeo vile tunavyotaka sisi na kama ingekuwa hivyo, bhasi zaidi ya 80% ya biashara za Tanzania zisingekufa kabla ya kufikisha miaka 5 maana sidhani kama kuna mtu anaeanzisha biashara ili ife...

One thing nachoweza kukubaliana nawe ni kuwa kila kinachotokea mara nyingi hutokana na maamuzi tunayofanya ila sababu za kupelekea kufanya uamuzi fulani, kuna zile tunazoweza kuzicontrol na zile tusizoweza

Personally, huwa naamini sana katika jitihada sana na strategy za kufanya mambo lakini huwa sipuuzi uwepo wa circumstances ambazo zipo nje ya uwezo wangu, japo sizipi uzito sana ili nibaki persistent
Dude you killed this shit as none
Nakumbuka 10yrs back my monthly income ilisababisha nipige hesabu kuwa by now ningekuwa nikiruka juu kidogo kama vile unacheza dama basi lazima nigonge ile roof ya 500M. Laiti ningejua kuwa 2024 itanikuta ninahangaika kuidhibiti 200k per month na nimetulia.
Nyie acheni tu.
 
Dude you killed this shit as none
Nakumbuka 10yrs back my monthly income ilisababisha nipige hesabu kuwa by now ningekuwa nikiruka juu kidogo kama vile unacheza dama basi lazima nigonge ile roof ya 500M. Laiti ningejua kuwa 2024 itanikuta ninahangaika kuidhibiti 200k per month na nimetulia.
Nyie acheni tu.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] firimasoni kwema
 
Back
Top Bottom