Simoni Petro alikuwa Myahudi wakarne ya 1, mfuasi wa Yesu Kristo, tena kati ya wandani wake.
Baada ya Yesu, ndiye mtu anayejulikana zaidi katika Injili zotenne.
Katika orodha zote nne za mitume12 wa Yesu zinazopatikana katikaBiblia ya Kikristo anashika nafasi ya kwanza (tofauti na wenzake wengi ambao wanabadilishana nafasi, na kinyume cha Yuda Iskarioti, msaliti anayepewa daima nafasi ya mwisho); isitoshe Math10:2 inasisitiza: "Wa kwanza Simoni aliyeitwa Petro".
Wakristo wengi, hasa Wakatoliki naWaorthodoksi, wanamheshimu kama mtakatifu tena kama papa wa kwanza wa Roma hadi kifodinichake kati ya miaka 64 na 67, wakati wa dhuluma ya Dola la Roma dhidi ya Ukristoiliyoanzishwa na Kaisari Nero.
Sikukuu yake inaadhimishwa kila tarehe 29 Juni pamoja na yaMtume Paulo.