Ndugu naomba nami nichangie kidogo. Ukristu ni utaratibu wa maisha unaotusaidia kuwa kalibu na Mungu yaani kunda upya mausiano yetu na Mungu. Kutokana na zambi ya kukosa utii , wazazi wetu wa mwanzo walivunja hayo mausiano. Kwa hiyo Petro kufa kwake Roma au sehemu nyingine aimfanyi mtu flani awe mkristu, ama kama Petro alikuwa papa wa kwanza au la aimfanyi mtu kuwa mkristu. Mkristu ni kristu mwengine. Yaani yule aishie yale kilisto aliyoyafundisha . Unaweza sema utayajuaje yale Kristu aliyoyafundisha , kupitia Makanisa haya haya tulionayo . Biblia inasema Kayafa alitabili ni heri mtu mmoja afe kwa ajili ya wengi si kwa sababu alikuwa mtu mtakatifu, hapana bali kwa sababu alikuwa kuwani mkuuu . na kunasehemu nyingine inasema wao wamekaa katika viti vya Musa yaani makuani na makasisi, wasikilizeni wasemacho bali matendo yao msiyafuate . Mungu alimtumia Paul aliyekuwa mzambi kuwaokoa maelufu . Kwa hiyo amini unachoamini na usipambane na kuvuluga watu wengine wanavyo amini.