This is...
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 5,050
- 5,204
100%WAKATOLIKI SI WAKRISTO NA HAWAJAWAHI KUWA WAKRISTO.HII ITABAKI KUWA NI DOLA YA KIRUMI.MAINJINIA WA NWO.Asante sana mkuu kwa kuongeza ufahamu mkubwa ndani yangu!!! Kuna prof Mmoja aliwahi kusema adui wa ukristo ni Roman Catholic, hawana muda na kuuishi ukristo bali mapokeo yao ambayo ni kivuli cha maovu
Wasabato wanapenda sana kuitangaza Roman
Hao nao naiona kama kweli yaani hawawezi kufundishana nini wafanye kwa muumba wao bali kutwa katorikiWasabato shetani wao ni wakatoliki, hawana shida na shetani halisi!!!
Hivi G White nae alizikwa Yerusalemu???
Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu naomba nami nichangie kidogo. Ukristu ni utaratibu wa maisha unaotusaidia kuwa kalibu na Mungu yaani kunda upya mausiano yetu na Mungu. Kutokana na zambi ya kukosa utii , wazazi wetu wa mwanzo walivunja hayo mausiano. Kwa hiyo Petro kufa kwake Roma au sehemu nyingine aimfanyi mtu flani awe mkristu, ama kama Petro alikuwa papa wa kwanza au la aimfanyi mtu kuwa mkristu. Mkristu ni kristu mwengine. Yaani yule aishie yale kilisto aliyoyafundisha . Unaweza sema utayajuaje yale Kristu aliyoyafundisha , kupitia Makanisa haya haya tulionayo . Biblia inasema Kayafa alitabili ni heri mtu mmoja afe kwa ajili ya wengi si kwa sababu alikuwa mtu mtakatifu, hapana bali kwa sababu alikuwa kuwani mkuuu . na kunasehemu nyingine inasema wao wamekaa katika viti vya Musa yaani makuani na makasisi, wasikilizeni wasemacho bali matendo yao msiyafuate . Mungu alimtumia Paul aliyekuwa mzambi kuwaokoa maelufu . Kwa hiyo amini unachoamini na usipambane na kuvuluga watu wengine wanavyo amini.Kwa zaidi ya maika 2000 watu wamekuwa wakiaminishwa kuwa Mtume Petro aliuwawa Roma na kuzikwa huko kwenye eneo lililojulikana kama tropaion. Tena imekuwa ikifundishwa na Kanisa Katoliki kuwa Petro ndiye alikuwa Papa wa kwanza lakini ukweli ni kwamba katika maisha yake yote Petro hakuwahi kabisa kuwa Papa achilia mbali kufika tu ROMA. Maisha yake yote Petro au Kefa kama wengine wanavyomwita hakuwahi kabisa kukanyaga ardhi ya Roma.
Mwaka 1958 huko Jerusalemu katika eneo lijulikanalo kama "Dominus Flevit" kwenye mlima wa Mizeituni ambapo kwa sasa hivi pamejengwa kanisa linaloitwa Franciscan Monastery yalichimbuliwa mabaki ya mifupa yaliyokuwa ndani ya boksi(ossuaries)na juu ya boksi hili kulikuwa na maandishi yaliyoandikwa kwa lugha ya Aramaic yakisomeka "Simon Bar Jona". Eneo ilipopatikana mifupa hiyo pia ilipatikana mifupa ya watu wengine ikiwa imehifadhiwa ndani ya maboksi hayo na juu yake yakiwa yameandikwa majina yao. Majina hayo ni pamoja na Mariam, Martha na Lazaro. Inaaminika kuwa Wakristo wa Mwanzo kabisa baada ya kupaa kwa MESSIAH kwenda mbinguni, walichagua kuzikana eneo hilo la Mlima wa Mizeituni, kwasababu imeandikwa kwenye Biblia kuwa siku MESSIAH atakaporudi tena duniani atasimama juu ya Mlima huo, soma ZEKARIA 14:3-4. Kutokana na imani waliyokuwa nayo, Wakristo hao waliamini kuwa itakuwa vema kama watazikwa eneo hilo ili siku ile BWANA YESU atakapokuja na kuwafufua, wawe wa kwanza kumlaki BWANA kwenye Mlima huo wa Mizeituni.
Franciscan "Terra Santa" Monastery, Jerusalem, mahali ambapo mifupa ya Petro ilipopatikana.Mifupa hiyo inayoaminika kuwa ni ya Petro, ilichimbuliwa na Archeologist wa Kiitaliano ambaye alikuwa ni Priest wa Kikatoliki akijulikana kama P.B. Bagatti. Baada ya kuichimbua mifupa hii na kujiridhisha yeye na wenzake aliokuwa nao, Bagatti alikwenda Vatican na kumjulisha Papa wa wakati ule aliyekuwa akiitwa Pius XII. Papa Pius XII alopoambiwa habari hizo na kuoneshwa ushahidi wote, alijibu tu kwa kusema; “inawezekana ikawa kweli hiyo ni mifupa ya PETRO, na inabidi tufanye marekebisho makubwa, lakini kwa sasa hivi kaeni kimya kabisa”. Bagatti akamuuliza Papa Pius XII, Je, unaamini itakuwa ni mabaki ya Petro? Papa Pius XII akamjibu kwa kusema; “kwa ushahidi ulionionesha, naamini itakuwa ni mifupa ya Petro”.
View attachment 669269
Cha ajabu ni kwamba mpaka Papa Pius XII anafariki dunia Octoba 9, 1958 hakuweka hadharani kabisa uvumbuzi huo uliofanywa na Archeologist Bagatti. Mwaka huo huo Bagatti ndipo akaamua kuandika kitabu akielezea kupatikana kwa mifupa ya Petro huko Jerusalem, kitabu hicho kinachoitwa, "Gli Scavi del Dominus Flevit", kilichochapishwa mwaka 1958. Kitabu hichi kiliandikwa na P. B. Bagatti akishirikiana na Archeologist mwenzake J. T. Milik, ambao wote walikuwa pia ni Ma-Priest wa Kanisa Katoliki. Bagatti anaonekana kuficha baadhi ya mambo na haelezei kwa undani hasa nini kilifanyika. Hii inadhihirisha wazi kabisa kuwa walifungwa mdomo na Kanisa Katoliki ili wasiweke kila kitu hadharani kwani kama wangefanya hivyo ingekuwa ni sawa na kulivua nguo kanisa, kwani kwa miaka yote kanisa Katoliki limekuwa likifundisha kuwa Petro aliishi Roma kwa miaka 24 na kuuawa na kuzikwa huko.
View attachment 669271
View attachment 669272
Maneno hayo hapo juu yanasomeka "Simoni Bar Yona"
Ushahidi mwingine unaoonesha wazi kabisa kuwa Petro hakuwahi kabisa kufika Roma, ni Biblia. Mtume Paulo katika Waraka zake zote hakuna mahali ameandika kuwa Petro alikwenda Roma na kuishi huko. Paulo alikuwa ni mtu anayependa sana kuandika kila kitu anachokutana nacho. Isingewezekana kabisa Petro ahamie Roma na kuishi huko kwa miaka 24 halafu Paulo asiandike, achilia mbali Petro mwenyewe asiandike kabisa Waraka wowote ule akielezea maisha yake akiwa Roma. Haiingii akilini hata kidogo mtu kama Petro eti akaishi mahali kwa miaka 24 akihubiri Injili, halafu jambo hilo lisiwemo kabisa ndani ya Biblia.
Isitoshe ukisoma Biblia utaona Paulo anaelezea wazi kabisa kuwa Petro alikuwa ni Mtume kwa ajili ya Wayahudi, soma WAGALATIA 2:7-8. Pia tukisoma Biblia tunaona BWANA anamtokea Anania kwenye maono na kumwambia aende akaonane na Sauli(Paulo), sababu yeye BWANA amemchagua SAULI(PAULO)kuwa Mtume wa Mataifa, soma MATENDO YA MITUME 9:10-15. Pia ukisoma Waraka wote wa Petro hakuna mahali popote Petro ameandika kuwa yupo Roma.
Kutokana na yote hayo na ushahidi wa mifupa iliyopatikana Jerusalem, ni kielelezo tosha kuwa Roman Catholic Church wanafundisha “uwongo” na wanafanya kila wawezalo kuuficha UKWELI. Kanisa hili limejaa mafundisho ya uwongo na kwa miaka mingi sana limewapotosha watu wengi sana. Kanisa hili lina intelijesia kali sana kiasi kwamba wanaweza kuficha habari yoyote ile isiwafikie watu, lakini kamwe hawawezi kushindana na MUNGU hasa pale anapoamua UKWELI lazima ujulikane.
Tokea mwaka 1958 ilipogundulika mifupa hii ya PETRO huko Jerusalem, Kanisa Katoliki limekuwa likificha uvumbuzi huu kwa kila namna. Eneo ambapo ilipatikana mifupa hii linamilikiwa na Kanisa hilo hivyo imekuwa rahisi wao kuuficha ukweli lakini pia ndani ya kanisa wapo baadhi ya Ma-Priest ambao huwa hawawezi kukaa kimya na wamekuwa wakivujisha siri hizi.
100%WAKATOLIKI SI WAKRISTO NA HAWAJAWAHI KUWA WAKRISTO.HII ITABAKI KUWA NI DOLA YA KIRUMI.MAINJINIA WA NWO.
Acha kabisa kujidanganya mkuu, UKRISTO siyo kuamini kila kitu hata kama ni uongo. Ukisoma vizuri kwenye Biblia kuna sehemu imeandikwa hivi;..... "lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyositirika, wala hatuenendi kwa hila wala kulichanganya neno la MUNGU na uongo, bali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikishuhudia mbele za MUNGU". 2 WAKORINTHO 4:2Ndugu naomba nami nichangie kidogo. Ukristu ni utaratibu wa maisha unaotusaidia kuwa kalibu na Mungu yaani kunda upya mausiano yetu na Mungu. Kutokana na zambi ya kukosa utii , wazazi wetu wa mwanzo walivunja hayo mausiano. Kwa hiyo Petro kufa kwake Roma au sehemu nyingine aimfanyi mtu flani awe mkristu, ama kama Petro alikuwa papa wa kwanza au la aimfanyi mtu kuwa mkristu. Mkristu ni kristu mwengine. Yaani yule aishie yale kilisto aliyoyafundisha . Unaweza sema utayajuaje yale Kristu aliyoyafundisha , kupitia Makanisa haya haya tulionayo . Biblia inasema Kayafa alitabili ni heri mtu mmoja afe kwa ajili ya wengi si kwa sababu alikuwa mtu mtakatifu, hapana bali kwa sababu alikuwa kuwani mkuuu . na kunasehemu nyingine inasema wao wamekaa katika viti vya Musa yaani makuani na makasisi, wasikilizeni wasemacho bali matendo yao msiyafuate . Mungu alimtumia Paul aliyekuwa mzambi kuwaokoa maelufu . Kwa hiyo amini unachoamini na usipambane na kuvuluga watu wengine wanavyo amini.
Kila kitu wanachofundisha Wakatoliki ambacho ni cha UWONGO nilishaandika humu. Ni mambo mengi sana, lakini kwa faida ya wengi nitaandika "uzi" kamili unaoonesha uwongo wote wa Kanisa Katoliki. Tega sikio mkuu na siku nikiandika nitaku-tag ili uwe wa kwanza kusoma. Wala usiwe na haraka, nitakuandikia kila kitu.
Waliwezaje kuuona kwa macho yao wakati unasema yamefichwa?Kwa taarifa yako hata mimi nilikuwa MKATOLIKI na baada yakufundishwa UWONGO, niliamua kuitafuta KWELI. Nilipoijua KWELI nikaona nisikae kimya wacha niwajulishe na wengine ili na wao waijue KWELI. Huwezi kuujua uchafu wa nyumba kama uko nje ya nyumba na hujawahi kuingia ndani.
Kwa taarifa yako Bagatti alihojiwa na akakiri kila kitu ingawa hakuandika kwenye kitabu chake. Kuna watu waliongea na akina Bagatti na wakaamua kwenda Jerusalemu kuutafuta UKWELI na wakauona kwa macho yao. Sasa wewe endelea kuogelea kwenye UWONGO wa Kanisa Katoliki. Hata baadhi ya Mapre wa Kanisa Katoliki wapo Jerusalemu na wanakuambia ni kweli Petro alifia Jerusalemu na kuzikwa huko. Lakini kamwe hawewezi kusimama hadharani na kuongea hivi vitu.
Uhakikishe unaweka na vifungu vya biblia, biblia ambayo imeandika na Wakatoliki unaosema ni waongo.Na sa tunaamini kuwa biblia imeandikwa kwa maongozi ya roho mt.Kila kitu wanachofundisha Wakatoliki ambacho ni cha UWONGO nilishaandika humu. Ni mambo mengi sana, lakini kwa faida ya wengi nitaandika "uzi" kamili unaoonesha uwongo wote wa Kanisa Katoliki. Tega sikio mkuu na siku nikiandika nitaku-tag ili uwe wa kwanza kusoma. Wala usiwe na haraka, nitakuandikia kila kitu.
Lkn biblia si iliandikwa na Wakatoliki?Sina haja ya kukutajia majina yao sababu hayatakusaidia kitu chochote kile. Wewe kama hata Biblia huiamini, utawaamini watu usiowajua? Biblia yenyewe inakuonesha wazi kabisa kuwa Petro au Kefa hakuwahi kufika Roma, lakini bado unabishana nayo. Bakia hivyo hivyo mkuu.
Bagatti ni mkatoliki au msabati?Kwa taarifa yako hata mimi nilikuwa MKATOLIKI na baada yakufundishwa UWONGO, niliamua kuitafuta KWELI. Nilipoijua KWELI nikaona nisikae kimya wacha niwajulishe na wengine ili na wao waijue KWELI. Huwezi kuujua uchafu wa nyumba kama uko nje ya nyumba na hujawahi kuingia ndani.
Kwa taarifa yako Bagatti alihojiwa na akakiri kila kitu ingawa hakuandika kwenye kitabu chake. Kuna watu waliongea na akina Bagatti na wakaamua kwenda Jerusalemu kuutafuta UKWELI na wakauona kwa macho yao. Sasa wewe endelea kuogelea kwenye UWONGO wa Kanisa Katoliki. Hata baadhi ya Mapre wa Kanisa Katoliki wapo Jerusalemu na wanakuambia ni kweli Petro alifia Jerusalemu na kuzikwa huko. Lakini kamwe hawewezi kusimama hadharani na kuongea hivi vitu.
Mkuu hebu amka kutoka kwenye usingizi uliolala, nani kakuambia Biblia iliandikwa na Wakatoliki? Hivi Paulo alikuwa Mkatoliki? Petro alikuwa Mkatoliki? Isaya alikuwa Mkatoliki? Ezekieli alikuwa Mkatoliki? Mathayo alikuwa Mkatoliki? Musa alikuwa Mkatoliki? Yohana alikuwa mkatoliki?????......... Hakuna hata mwandishi mmoja wa Biblia aliyekuwa Mkatoliki, isitoshe wakati Biblia inaandikwa hakukuwa na Kanisa la Katoliki.Uhakikishe unaweka na vifungu vya biblia, biblia ambayo imeandika na Wakatoliki unaosema ni waongo.Na sa tunaamini kuwa biblia imeandikwa kwa maongozi ya roho mt.
Na roho mt haishi wala kuwaongoza waongo
Sent using Jamii Forums mobile app