Kaburi la Petro(Simoni bar-yona) lipo Jerusalem na siyo Roma

Kaburi la Petro(Simoni bar-yona) lipo Jerusalem na siyo Roma

Ukisoma ZAKARIA 14:3-4 akuna koneksheni na ulichosema alf hy ni agano la kale Yesu bd akufika,onyo usisome Biblia nusu mstari kutoa ushuhuda.
 
Kwa zaidi ya maika 2000 watu wamekuwa wakiaminishwa kuwa Mtume Petro aliuwawa Roma na kuzikwa huko kwenye eneo lililojulikana kama tropaion. Tena imekuwa ikifundishwa na Kanisa Katoliki kuwa Petro ndiye alikuwa Papa wa kwanza lakini ukweli ni kwamba katika maisha yake yote Petro hakuwahi kabisa kuwa Papa achilia mbali kufika tu ROMA. Maisha yake yote Petro au Kefa kama wengine wanavyomwita hakuwahi kabisa kukanyaga ardhi ya Roma.

Mwaka 1958 huko Jerusalemu katika eneo lijulikanalo kama "Dominus Flevit" kwenye mlima wa Mizeituni ambapo kwa sasa hivi pamejengwa kanisa linaloitwa Franciscan Monastery yalichimbuliwa mabaki ya mifupa yaliyokuwa ndani ya boksi(ossuaries)na juu ya boksi hili kulikuwa na maandishi yaliyoandikwa kwa lugha ya Aramaic yakisomeka "Simon Bar Jona". Eneo ilipopatikana mifupa hiyo pia ilipatikana mifupa ya watu wengine ikiwa imehifadhiwa ndani ya maboksi hayo na juu yake yakiwa yameandikwa majina yao. Majina hayo ni pamoja na Mariam, Martha na Lazaro. Inaaminika kuwa Wakristo wa Mwanzo kabisa baada ya kupaa kwa MESSIAH kwenda mbinguni, walichagua kuzikana eneo hilo la Mlima wa Mizeituni, kwasababu imeandikwa kwenye Biblia kuwa siku MESSIAH atakaporudi tena duniani atasimama juu ya Mlima huo, soma ZEKARIA 14:3-4. Kutokana na imani waliyokuwa nayo, Wakristo hao waliamini kuwa itakuwa vema kama watazikwa eneo hilo ili siku ile BWANA YESU atakapokuja na kuwafufua, wawe wa kwanza kumlaki BWANA kwenye Mlima huo wa Mizeituni.

Franciscan "Terra Santa" Monastery, Jerusalem, mahali ambapo mifupa ya Petro ilipopatikana.
View attachment 669269
Mifupa hiyo inayoaminika kuwa ni ya Petro, ilichimbuliwa na Archeologist wa Kiitaliano ambaye alikuwa ni Priest wa Kikatoliki akijulikana kama P.B. Bagatti. Baada ya kuichimbua mifupa hii na kujiridhisha yeye na wenzake aliokuwa nao, Bagatti alikwenda Vatican na kumjulisha Papa wa wakati ule aliyekuwa akiitwa Pius XII. Papa Pius XII alopoambiwa habari hizo na kuoneshwa ushahidi wote, alijibu tu kwa kusema; “inawezekana ikawa kweli hiyo ni mifupa ya PETRO, na inabidi tufanye marekebisho makubwa, lakini kwa sasa hivi kaeni kimya kabisa”. Bagatti akamuuliza Papa Pius XII, Je, unaamini itakuwa ni mabaki ya Petro? Papa Pius XII akamjibu kwa kusema; “kwa ushahidi ulionionesha, naamini itakuwa ni mifupa ya Petro”.

Cha ajabu ni kwamba mpaka Papa Pius XII anafariki dunia Octoba 9, 1958 hakuweka hadharani kabisa uvumbuzi huo uliofanywa na Archeologist Bagatti. Mwaka huo huo Bagatti ndipo akaamua kuandika kitabu akielezea kupatikana kwa mifupa ya Petro huko Jerusalem, kitabu hicho kinachoitwa, "Gli Scavi del Dominus Flevit", kilichochapishwa mwaka 1958. Kitabu hichi kiliandikwa na P. B. Bagatti akishirikiana na Archeologist mwenzake J. T. Milik, ambao wote walikuwa pia ni Ma-Priest wa Kanisa Katoliki. Bagatti anaonekana kuficha baadhi ya mambo na haelezei kwa undani hasa nini kilifanyika. Hii inadhihirisha wazi kabisa kuwa walifungwa mdomo na Kanisa Katoliki ili wasiweke kila kitu hadharani kwani kama wangefanya hivyo ingekuwa ni sawa na kulivua nguo kanisa, kwani kwa miaka yote kanisa Katoliki limekuwa likifundisha kuwa Petro aliishi Roma kwa miaka 24 na kuuawa na kuzikwa huko.
View attachment 669271
View attachment 669272
Maneno hayo hapo juu yanasomeka "Simoni Bar Yona"​

Ushahidi mwingine unaoonesha wazi kabisa kuwa Petro hakuwahi kabisa kufika Roma, ni Biblia. Mtume Paulo katika Waraka zake zote hakuna mahali ameandika kuwa Petro alikwenda Roma na kuishi huko. Paulo alikuwa ni mtu anayependa sana kuandika kila kitu anachokutana nacho. Isingewezekana kabisa Petro ahamie Roma na kuishi huko kwa miaka 24 halafu Paulo asiandike, achilia mbali Petro mwenyewe asiandike kabisa Waraka wowote ule akielezea maisha yake akiwa Roma. Haiingii akilini hata kidogo mtu kama Petro eti akaishi mahali kwa miaka 24 akihubiri Injili, halafu jambo hilo lisiwemo kabisa ndani ya Biblia.

Isitoshe ukisoma Biblia utaona Paulo anaelezea wazi kabisa kuwa Petro alikuwa ni Mtume kwa ajili ya Wayahudi, soma WAGALATIA 2:7-8. Pia tukisoma Biblia tunaona BWANA anamtokea Anania kwenye maono na kumwambia aende akaonane na Sauli(Paulo), sababu yeye BWANA amemchagua SAULI(PAULO)kuwa Mtume wa Mataifa, soma MATENDO YA MITUME 9:10-15. Pia ukisoma Waraka wote wa Petro hakuna mahali popote Petro ameandika kuwa yupo Roma.

Kutokana na yote hayo na ushahidi wa mifupa iliyopatikana Jerusalem, ni kielelezo tosha kuwa Roman Catholic Church wanafundisha “uwongo” na wanafanya kila wawezalo kuuficha UKWELI. Kanisa hili limejaa mafundisho ya uwongo na kwa miaka mingi sana limewapotosha watu wengi sana. Kanisa hili lina intelijesia kali sana kiasi kwamba wanaweza kuficha habari yoyote ile isiwafikie watu, lakini kamwe hawawezi kushindana na MUNGU hasa pale anapoamua UKWELI lazima ujulikane.

Tokea mwaka 1958 ilipogundulika mifupa hii ya PETRO huko Jerusalem, Kanisa Katoliki limekuwa likificha uvumbuzi huu kwa kila namna. Eneo ambapo ilipatikana mifupa hii linamilikiwa na Kanisa hilo hivyo imekuwa rahisi wao kuuficha ukweli lakini pia ndani ya kanisa wapo baadhi ya Ma-Priest ambao huwa hawawezi kukaa kimya na wamekuwa wakivujisha siri hizi.
I'm proud to be Catholic whatever the situation is!?
 
Tuandikiea hapa kifungu kwa kifungu ukituonesha kwenye kitabu cha UFUNUO WA YOHANA palipoandikwa namna Emperor Nero alivyokuwa mdhalimu. Tuoneshe hapa ni mstari gani kwenye kitabu cha UFUNUO WA YOHANA pameandikwa jinsi Petro alivyouliwa akiwa Roma.

Mimi nimekisoma kitabu chote cha UFUNUO WA YOHANA, tena siyo mara moja, mara nyingi sana na sijaona mahali popote palipoandikwa kuwa PETRO alikuwa Roma.

Kuhusu PAULO mimi sijasema PAULO alifia wapi wala sijaandika kama PAULO hakufika Roma. Najua fika kwamba PAULO alikwenda Roma hata Biblia inasema wazi kabisa kuwa PAULO alikwenda Roma.

Acha kuchanganya mada wewe mdanganyifu wa kanisa Katoliki. Kama wewe Otorong'ong'o umedanganywa na Mafundisho ya kanisa katoliki na ukakubali kudanganywa usifikiri kila mtu ana akili kama zako za kudanganyika kirahisi. Wengine hatukubali kudanganyika, tunaitafuta KWELI nayo hiyo KWELI inatuweka huru kweli kweli.
Tusipende sana kushabikia madhehebu yetu, maana hatutaweza kuijua kweli ya Mungu tukiegemea sana kwenye madhehebu yetu. Maana kila kiongozi uvutia upande wake. Hivyo ni vyema kujifunza biblia, lkn pia kuwa waombaji sana ili Roho wa Bwana na atufunulie.
 
Hivi sisi Waafrika tuna nini hasa na hizi imani za kimapokeo? Tunalumbana wee wenye dini zao wanakunywa chai pamoja!
 
Tuandikiea hapa kifungu kwa kifungu ukituonesha kwenye kitabu cha UFUNUO WA YOHANA palipoandikwa namna Emperor Nero alivyokuwa mdhalimu. Tuoneshe hapa ni mstari gani kwenye kitabu cha UFUNUO WA YOHANA pameandikwa jinsi Petro alivyouliwa akiwa Roma.

Mimi nimekisoma kitabu chote cha UFUNUO WA YOHANA, tena siyo mara moja, mara nyingi sana na sijaona mahali popote palipoandikwa kuwa PETRO alikuwa Roma.

Kuhusu PAULO mimi sijasema PAULO alifia wapi wala sijaandika kama PAULO hakufika Roma. Najua fika kwamba PAULO alikwenda Roma hata Biblia inasema wazi kabisa kuwa PAULO alikwenda Roma.

Acha kuchanganya mada wewe mdanganyifu wa kanisa Katoliki. Kama wewe Otorong'ong'o umedanganywa na Mafundisho ya kanisa katoliki na ukakubali kudanganywa usifikiri kila mtu ana akili kama zako za kudanganyika kirahisi. Wengine hatukubali kudanganyika, tunaitafuta KWELI nayo hiyo KWELI inatuweka huru kweli kweli.
Kila kitabu kiliandikwa kwa makusudi flani. Kasome historia ya mwandishi wa kitabu cha ufunuo. Tatizo hata source zenyewe mnategemea za wazushi. Ufunuo kiliandikwa kwa codes tupu. Ni kama unavyoona leo watu wakitaka kuusema utawala wa JPM inavyobidi watumie codes kama dikteta uchwara n.k kufikisha meseji. Jifunze lengo la mwandishi wa Ufunuo utajua kwanini alitumia mafumbo kwenye uandishi wake. Ndio maana leo wengine mnabeba codes za nyakati zile zikiongelea dola ya Rumi mnasema ni Kanisa Katoliki.
 
Hakunipunguzii chochote hata kama ni kweli Petro hakuzikwa Roma. Kanisa limenifundisha imani yake i katika Kristo msulubiwa na akafufuka siku ya 3 ili kuukomboa ulimwengu. Hiyo ndo msingi wa imani katoliki. Sasa kama hii imani kwako ni uzushi na uongo then wewe ni anti-christ...
Unatakiwa kuvutwa na MUNGU ili kujua uchafu wa Kanisa Katoliki. Siyo kila kitu kinachofundishwa na Kanisa Katoliki ni cha uwongo, isipokuwa kinachofanyika ni wamechanganya KWELI kidogo na UWONGO kiasi. Sasa hebu fikiria mfano huu; hivi ukichukua maji safi ya kunywa ukadondoshea humo matone kidogo ya sumu ya panya, Je! hayo maji yatakuwa salama kwa kunywa? Je! wewe utakuwa tayari kunywa hayo maji?

Vivyo hivyo ndivyo Kanisa Katoliki limefanya, limechukua baadhi ya mafundisho ya KWELI na kuyachanganya na UWONGO ambao ni kama sumu, hata ikiwa kidogo namna gani lazima itaua tu. Na ndiyo imeandikwa hivi; "Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote. Kwa maana aliyesema usizini, pia alisema usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, ila umeua umekuwa mvunja sheria" YAKOBO 2:10-11, MATHAYO 5:19

Mfano mzuri ni Kanisa Katoliki linakufundisha imani ya YESU KRISTO, lakini kanisa hilo hilo linakufundisha kusali huku ukiwa umeshika sanamu mkononi(ROSARI), tena kanisa hilo hilo linachonga sanamu na kuzitumikia, Soma KUTOKA 20:4-6.

Je! YESU KRISTO alikufundisha kusali na kumwomba mama yake Mariam? YESU alikufundisha kusali na kuwaomba wafu?? Je! YESU hakusema tukisali tumwombe MUNGU peke yake ambaye ndiye BABA yetu?? Soma MATHAYO 6:5-8.

Ukitafakari kwa makini utaona ni jinsi gani Kanisa Katoliki linawapoteza bila ninyi wenyewe kuwa na ufahamu. Huwezi ukabakia salama kwa kuyashika mafundisho ya Kanisa Katoliki.
sanamu 1.jpg

"Imeandikwa, usijifanyie sanamu, usiisujudie wala usiitumike" KUTOKA 20:4-6
 
Nimejuwa kitu ambacho nisingekaa nikakijuwa.

Pia nimependa hii ya kuandika jina ndani ya box lenye mabaki.
 
M
Ngoja nikusaidie kuivunjavunja. Soma hii then tumia hizo Bible quote as reference ndio turudi kwenye mjadala....

There is, in the greeting at the end of the first epistle: “The Church here in Babylon, united with you by God’s election, sends you her greeting, and so does my son, Mark” (1 Pet. 5:13, Knox). Babylon is a code-word for Rome. It is used that way multiple times in works like the Sibylline Oracles (5:159f), the Apocalypse of Baruch (2:1), and 4 Esdras (3:1). Eusebius Pamphilius, in The Chronicle, composed about A.D. 303, noted that “It is said that Peter’s first epistle, in which he makes mention of Mark, was composed at Rome itself; and that he himself indicates this, referring to the city figuratively as Babylon.”

Consider now the other New Testament citations: “Another angel, a second, followed, saying, ‘Fallen, fallen is Babylon the great, she who made all nations drink the wine of her impure passion’” (Rev. 14:8). “The great city was split into three parts, and the cities of the nations fell, and God remembered great Babylon, to make her drain the cup of the fury of his wrath” (Rev. 16:19). “[A]nd on her forehead was written a name of mystery: ‘Babylon the great, mother of harlots and of earth’s abominations’” (Rev. 17:5). “And he called out with a mighty voice, ‘Fallen, fallen is Babylon the great’” (Rev. 18:2). “[T]hey will stand far off, in fear of her torment, and say, ‘Alas! alas! thou great city, thou mighty city, Babylon! In one hour has thy judgment come’” (Rev. 18:10). “So shall Babylon the great city be thrown down with violence” (Rev. 18:21).

These references can’t be to the one-time capital of the Babylonian empire. That Babylon had been reduced to an inconsequential village by the march of years, military defeat, and political subjugation; it was no longer a “great city.” It played no important part in the recent history of the ancient world. From the New Testament perspective, the only candidates for the “great city” mentioned in Revelation are Rome and Jerusalem.

“But there is no good reason for saying that ‘Babylon’ means ‘Rome,’” insists Boettner. But there is, and the good reason is persecution. The authorities knew that Peter was a leader of the Church, and the Church, under Roman law, was considered organized atheism. (The worship of any gods other than the Roman was considered atheism.) Peter would do himself, not to mention those with him, no service by advertising his presence in the capital—after all, mail service from Rome was then even worse than it is today, and letters were routinely read by Roman officials. Peter was a wanted man, as were all Christian leaders. Why encourage a manhunt? We also know that the apostles sometimes referred to cities under symbolic names (cf. Rev. 11:8).

In any event, let us be generous and admit that it is easy for an opponent of Catholicism to think, in good faith, that Peter was never in Rome, at least if he bases his conclusion on the Bible alone. But restricting his inquiry to the Bible is something he should not do; external evidence has to be considered, too.

Early Christian Testimony

William A. Jurgens, in his three-volume set The Faith of the Early Fathers, a masterly compendium that cites at length everything from the Didache to John Damascene, includes thirty references to this question, divided, in the index, about evenly between the statements that “Peter came to Rome and died there” and that “Peter established his See at Rome and made the bishop of Rome his successor in the primacy.” A few examples must suffice, but they and other early references demonstrate that there can be no question that the universal—and very early—position (one hesitates to use the word “tradition,” since some people read that as “legend”) was that Peter certainly did end up in the capital of the Empire.
Mkuu MTAZAMO hii hoja nilishakujibu, pitia "reply" zangu kwako utaona, tusirudie rudie kitu ambacho nimeshakijibu ni kupotezeana muda tu. Nimekuandikia kuwa Petro aliposema yupo Babiloni ni kweli kabisa alikuwa kwenye mji uliokuwa unaitwa Babiloni wakati ule. Na mji huo ulikuwa Misri. Ndiyo utashangaa kwamba Misri kuna Mji ulikuwa unaitwa Babiloni. Mji huo ulikuwepo na sasa hivi unajulikana kama Old Cairo au Coptic Cairo. Petro na Marko ndipo walikuwapo mahali hapa wakati ule Petro anaandika ule Waraka wake wa Kwanza. WARAKA WA KWANZA WA PETRO 5:13

Huu ni ushahidi tosha kwako kuwa PETRO hakufika Roma. Wala tafsiri ya mji huu Babeli siyo Roma. Tafsiri ya Roma ni BABELI MKUU. Unapaswa kujua tofauti kati ya neno BABELI na BABELI MKUU. Soma UFUNUO 17:5 na 18:21

Petro alisema yupo "Babeli" na hakusema yupo "Babeli ule mkuu", kuna tofauti kubwa sana ya hayo maneno. Soma hii; link, Babylon Fortress - Wikipedia
 
Hili ndio tatizo lenu...ubishi na kutopenda kusoma kweli zaidi ya kuwaamini wazushi. Naamini quote kutoka Catholic Answers hujaisoma au umeparaza tu. Huyu jamaa yako analeta stori za Wikipedia ulinganishe na watu walioweka facts kutoka kwenye Bible kuonesha Babylon ilikuwa ni code word ya Roma. Rudi usome upya ukuze maarifa acha kurukia vitu virahisi. Nataka utoe challenge kwenye hilo bandiko na si kuleta stori za Wikipedia.
Nimeshakujibu kuhusu tafsiri ya neno BABELI.
 
Ninaanza kukuamini! Lakini kabla sijaamini kabisa naomba uniambie dhehebu lako, najua watu wa Mungu huwa hawadanganyi kisha nitaomba tubadilishane uelewa kidogo.
Hapa JF katumia jina bandia,acha fikara za kuwa anaweza akawa mkweli kutaja dhehebu lake
 
Son of Gamba wewe ni "Mpumbavu""Mpumbavu"
Asante mkuu kwa kuniita MPUMBAVU. Lakini mimi nafikiri MPUMBAVU ni mtu yule anayevunja AMRI za MUNGU kwa makusudi kabisa. Mpumbavu ni mtu yule anayeisujudia sanamu na kuitumikia badala ya kumsujudia MUNGU na kumtumikia.
sanamu 1.jpg

sanamu2.jpg

KUTOKA 20:4-6 "Usijifanyie sanamu ya kuchonga wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia".
 
Ubarikiwe sana, nilichogundua ni kuwa hizi ID fake Zinatuficha sana Waadventista hatufahamiani,, ila kupitia huu Uzi nimekufaham, wakondya sana wasu
 
Kila kitabu kiliandikwa kwa makusudi flani. Kasome historia ya mwandishi wa kitabu cha ufunuo. Tatizo hata source zenyewe mnategemea za wazushi. Ufunuo kiliandikwa kwa codes tupu. Ni kama unavyoona leo watu wakitaka kuusema utawala wa JPM inavyobidi watumie codes kama dikteta uchwara n.k kufikisha meseji. Jifunze lengo la mwandishi wa Ufunuo utajua kwanini alitumia mafumbo kwenye uandishi wake. Ndio maana leo wengine mnabeba codes za nyakati zile zikiongelea dola ya Rumi mnasema ni Kanisa Katoliki.
Acha porojo dogo, nimesema niandikieni hapa hiyo mistari ya kwenye kitabu cha UFUNUO hata kama ni CODES wewe andika tuone. Mbona mnakuwa kama watoto wa darasa la chekechea? Unashindwa nini kuandika hiyo mistari kutoka kwenye UFUNUOA kama kweli ipo?

Mimi nasubiri kwa hamu kuona hiyo mistari ya kwenye kitabu cha UFUNOA WA YOHANA inayosema eti Petro alikwenda Roma na kuuwa akiwa Roma. Tuandikieni ili na sisi tuisome, hata kama hatutaelewa wewe tuandikie tu.

Usiniletee porojo za JPM, mimi nataka kuona maandiko kutoka kwenye kitabu cha UFUNUO basi.
 
Unatakiwa kuvutwa na MUNGU ili kujua uchafu wa Kanisa Katoliki. Siyo kila kitu kinachofundishwa na Kanisa Katoliki ni cha uwongo, isipokuwa kinachofanyika ni wamechanganya KWELI kidogo na UWONGO kiasi. Sasa hebu fikiria mfano huu; hivi ukichukua maji safi ya kunywa ukadondoshea humo matone kidogo ya sumu ya panya, Je! hayo maji yatakuwa salama kwa kunywa? Je! wewe utakuwa tayari kunywa hayo maji?

Vivyo hivyo ndivyo Kanisa Katoliki limefanya, limechukua baadhi ya mafundisho ya KWELI na kuyachanganya na UWONGO ambao ni kama sumu, hata ikiwa kidogo namna gani lazima itaua tu. Na ndiyo imeandikwa hivi; "Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote. Kwa maana aliyesema usizini, pia alisema usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, ila umeua umekuwa mvunja sheria" YAKOBO 2:10-11, MATHAYO 5:19

Mfano mzuri ni Kanisa Katoliki linakufundisha imani ya YESU KRISTO, lakini kanisa hilo hilo linakufundisha kusali huku ukiwa umeshika sanamu mkononi(ROSARI), tena kanisa hilo hilo linachonga sanamu na kuzitumikia, Soma KUTOKA 20:4-6.

Je! YESU KRISTO alikufundisha kusali na kumwomba mama yake Mariam? YESU alikufundisha kusali na kuwaomba wafu?? Je! YESU hakusema tukisali tumwombe MUNGU peke yake ambaye ndiye BABA yetu?? Soma MATHAYO 6:5-8.

Ukitafakari kwa makini utaona ni jinsi gani Kanisa Katoliki linawapoteza bila ninyi wenyewe kuwa na ufahamu. Huwezi ukabakia salama kwa kuyashika mafundisho ya Kanisa Katoliki.
View attachment 669670
"Imeandikwa, usijifanyie sanamu, usiisujudie wala usiitumike" KUTOKA 20:4-6
Mengi ya unayoyaandika umesimuliwa na hufahamu msingi wa imani katoliki. Labda tuanze na hili kuabudu ni nini? Na kama hivo ulivoandika ina maana Mungu aliwafundisha wana wa Israel kuabudu sanamu? Soma Hesabu 21 mstari wa 8 na wa 9. Pia soma Yohana 3 mstari wa 14 mpaka wa 15.
Wakatoliki wengi huwa hawajibu watu kwa mistari ya biblia sio kwamba hawajui. Wakati mwingine haina maana unapobishana na mtu asiyeelewa jambo yeye amekaririshwa tu na kuanza kushambulia wakatoliki.
Kiufupi unapoongelea mambo ya kuabudu sanamu unanifanya nikuhoji kama unaelewa habari ya hema ya kukutania na habari ya sanduku la agano. Maelekezo ya kuliunda na namna ya kumwabudu Mungu mbele ya sanduku la agano.
Ningelikuwa na muda nimekujibu hoja kwa hoja na kwa kutumia hiyo hiyo bible.
Acha kushutumu ndugu zako katika Kristo zaidi ningekushauri ujikite katika kueneza enjili ya bwana na kumtukuza Mungu aliye muumba wetu.
 
Tusipende sana kushabikia madhehebu yetu, maana hatutaweza kuijua kweli ya Mungu tukiegemea sana kwenye madhehebu yetu. Maana kila kiongozi uvutia upande wake. Hivyo ni vyema kujifunza biblia, lkn pia kuwa waombaji sana ili Roho wa Bwana na atufunulie.
Biblia ndiyo inabeba UKWELI wote na siyo vinginevyo. Tukiisoma BIBLIA na kuamini, tutaijua KWELI ya MUNGU.

Baadhi ya madhehebu yanafundisha "hadithi za wanadamu" na siyo NENO la MUNGU kama ipasavyo. Moja ya madhehebu hayo ni KANISA KATOLIKI LA MITUME. Kanisa hili linafundisha "hadithi za wanadamu" na mapokeo ya UWONGO.

Tuko pamoja mkuu jmwanse , nakubaliana na wewe kabisa. Lakini UKWELI ni lazima tuuongee ili na wengine waijue hiyo KWELI.
 
I'm proud to be Catholic whatever the situation is!?
GOD created man and gave him "free will" to choose from GOOD or EVIL. But remember, the day is coming when you will be brought in-front of the KING and GOD shall bring every work into judgement, with every secret thing, whether it be good or whether it be evil.
 
Mengi ya unayoyaandika umesimuliwa na hufahamu msingi wa imani katoliki. Labda tuanze na hili kuabudu ni nini? Na kama hivo ulivoandika ina maana Mungu aliwafundisha wana wa Israel kuabudu sanamu? Soma Hesabu 21 mstari wa 8 na wa 9. Pia soma Yohana 3 mstari wa 14 mpaka wa 15.
Wakatoliki wengi huwa hawajibu watu kwa mistari ya biblia sio kwamba hawajui. Wakati mwingine haina maana unapobishana na mtu asiyeelewa jambo yeye amekaririshwa tu na kuanza kushambulia wakatoliki.
Kiufupi unapoongelea mambo ya kuabudu sanamu unanifanya nikuhoji kama unaelewa habari ya hema ya kukutania na habari ya sanduku la agano. Maelekezo ya kuliunda na namna ya kumwabudu Mungu mbele ya sanduku la agano.
Ningelikuwa na muda nimekujibu hoja kwa hoja na kwa kutumia hiyo hiyo bible.
Acha kushutumu ndugu zako katika Kristo zaidi ningekushauri ujikite katika kueneza enjili ya bwana na kumtukuza Mungu aliye muumba wetu.
Hata sasa ninaeneza INJILI ya BWANA, INJILI safi isiyogoshiwa, wala kuchakachuliwa. Hivi unafahamu kwamba kuna INJILI iliyogoshiwa na INJILI isiyogoshiwa?

Sasa Wakatoliki wanahubiri injili ile iliyoghoshiwa. Soma WAGALATIA 1:6-9
 
Tatizo hapa tutaishia kubishana na watu wanaotaka kujua historia kupitia Biblia pekee utafikiri kile ni kitabu cha historia. Kanisa Katoliki ni tajiri kimafundisho sababu imetunza nyaraka, barua na mafundisho ya mababa wa Kanisa hadi sasa. Zipo barua zimetunzwa karne nyingi zinazosimulia kuanzia uinjilishaji wa Petro na Paul huko Roma hadi vifo vyao. Mlisikia barua kama ile iliyotolewa na baraza la maaskofu kuelekea uchaguzi wa 2010. Ile barua itaishi vizazi na vizazi na wapo wataopinga kuwa barua hizo ni feki nyakati hizo! Kama unataka kujua kweli safari ya Petro huko Roma ingia kwenye site ya Catholic Answers utapata shule nzuri tu.

Nimemis colabo ya nyaraka za CPT na TEC wako kimya sana nyakati hizi sijui nini kimewakumba
 
Hivi bado kuna watu wanawaamini Roman catholic?
Watu waliodiriki kuificha bibilia kwa waumini aao mpaka miaka ya karibuni kidogo ndyo wamewaruhusu kuisoma.
Vinginevyo ni vimstari wamemega na kutengeneza misali yao.

Ndyo maana hata Amri ya kwanza wameifinya ili Wajinga waendelee kuabudu vinyago na masanamu.
 
Back
Top Bottom