Kaburi la Petro(Simoni bar-yona) lipo Jerusalem na siyo Roma

Kaburi la Petro(Simoni bar-yona) lipo Jerusalem na siyo Roma

Kanisa katoliki linazidi kuimarika duniani kote kwa Hawa wala makande wanaojiita wanatakatifu( mkasubirie miujiza ya kwenda ulaya bila nauli)
 
LOO!!!! Naona zile Ids zime charuka kama panya walio kuwa kwenye shimo halfu moto ukawashwa na wakafukiziwa moshi wa pilipili. Watavyo chomoka humo ndani!!!!

Hii uzi unazungumza habari ya Petro. Sasa tuone shetani na mawakala/wafuasi wake walivyo na hila tangu enzi za Adam na Hawa pale Eden.


Kama tulivyo sikia Shetani jinsi alivyotaka kupora maiti ya Nabii Musa. Na penginepo ni pale katika hekalu la Wana wa Israel Mwenyezi Mungu alilojengewa na mtumishi wake Mfalme Suleman kuliko na sinto fahamu mpaka leo hii.

Basi kisa kingine cha shetani ni hiki. Philipo mmoja wa wale mitume wa Yesu na mwenzake Stephano wakaipeleka Injili huko samaria. Kwa vile walikuwa wamejawa Roho Mtakatifu wakafanya miujiza mingi na mikubwa sana.

Hapo samaria alikuwepo sangoma/ mganga alimaarufu sana aitwaye Simioni mfwasi wa shetani haswa. Huyu Simioni alikuwa n,a maajabu makubwa kwa maana ya uganga wake (hata zama hizi wako). Huyu simioni mganga mkuu akavutiwa na ile miujiza ya Filipo na Stephano ambayo ilifunika na kupora kabisa umaarufu wake. Hivyo naye akaamua kubatizwa kama wengine huko wa livyo batizwa


Petro na Yohana wakatumwa kutoka Yerusalem waende kumuongezea nguvu Filipo maana Stephano alishauliwa kwa kupondwa mawe na wapinga Kristo.

Petro na Yohana walipofika kule samaria nao wakafanya miujiza mingi na mikubwa. Watu wa samaria wakawaleta wagonjwa hata waguswe tu na kivuli cha Petro maana waliponywa magonjwa yao kwa kuguswa na kivuli cha Petro.

Petro na Yohana walipo wawekea mikono yao wale wafuasi wao wa kule samaria wakajazwa Roho Mtakatifu. Simioni yule mganga maarufu aliye batizwa akajawa na wivu mkuu.

Ona jinsi shetani alivyo na hila, uganga wa simioni ulimpatia utajiri mkubwa. Akaenda akitaka kuwarubuni, ndio kuwalaghaii Petro na Yohana kwa kuwa ambia ni kiasi gani cha fedha awape ili waweze kumuuzia huo upako wao.

Ndipo Petro akamkemea Simioni mganga (kumbuka malaika mkuu wa vita Mikaeli alisha mkemea shetani wakati akiitaka maiti ya Nabii Musa) akisema, "May you and your money go to hell, for thinking that you can buy God's gift with money." Matendo ya Mitume 8:4-24.

Hivyo basi utendaji wa shetani kila siku umejaa hila na ulaghai tangu huko mwanzo hata milele.
Ni muhimu tujue wakina Simioni mganga wapo hata leo hii. Wapo wengi sana na hata humu jF hawakosi. Wataanzisha nyuzi nyingi tena watanukuu maandiko ya Biblia kumbe wamejawana na wivu kama Simioni mganga. Nia yao kuu ni kupotosha kuhusu Bwana wetu Yesu Kristo na Ukristo. Lakini wajue mwisho wa siku watashindwa tu..
 
Inashangaza kwakweli,unawatuhumu wakatoliki kuwa wanafundisha uongo lkn mafundisho unayoyaamini wewe kuwa Petro hakuzikwa Vatican yanatoka kwa haohao wakatoliki
Hahaha umemuweza
 
Hata wakisema alizikwa makaburi ya Njiro haisaidii chochote.
 
Kwani tangu lini Wasabato wakaamini historio ya Ukristo? Ikiwa hawaamini leo kwenye kujua wapi amezikwa petro imetoka wapi?

Je kujua wapi amezikwa ni mafundisho ya msingi ya kanisa au suala la kihistoria?
 
Biblia haikupangwa na Wakatoliki, Biblia ilipangwa kwa uwezo wa ROHO MTAKATIFU. Hakuna ambaye angeweza kuzuia Biblia isiwe ilivyo leo hii. Tena kuna vitabu feki Wakatoliki walijaribu kuviingiza kwenye Biblia lakini kwa nguvu ya ROHO MTAKATIFU walishindwa kufanya hivyo. Matokeo yake vitabu hivyo feki na Waraka feki vinatumiwa sasa hivi na kanisa Katoliki katika kuwapotosha waumini wake. Vipo vitabu vingi sana ambavyo ni feki na vinatumiwa na hilo Kanisa.

Ukisikia tunasimama watu kama sisi na kusema Kanisa Katoliki ni wakala wa Ibilisi na linafundisha UWONGO usifikiri tunabahatisha; tunajua tunachokisema na tunauhakika na kile tunachokiongea. Sisi hatuna chuki na Wakatoliki, sisi vita yetu ni kuupinga UWONGO wa IBILISI ili asiendelee kuwapoteza ndugu zetu.

Wale watakaotusikia na kuijua "KWELI", hiyo KWELI itawaweka huru na watajua namna ya kushika AMRI za MUNGU na imani ya YESU KRISTO na YESU KRISTO atawaokoa kutoka kwenye upotovu wa shetani. Wale watakao kataa kusikia, shauri yao; wacha wakae kwenye upotovu wao.
We unaongea kimbea sasa usiseme vingi vinatumiwa ujawahi sali catholic ebu tupe kimoja tu kama ukijui basi tafuta la kufanya ndo nyie mnaoamini mchungaji wenu kua mti ya kivuli ni mikosi kwel kazi sana ni vizur kama unasema dini ya mwenzio usiseme kinafki uwezi kudhibitisha unaongea kisa nabii wako amekwambia kaseme ivi ili apate waumini
 
Hizo barua zote mimi nazifahamu na wala hazina UKWELI wowote ule. Barua hizo ni za kutungwa tu baadhi ya watu. Mtu aliyeutengeneza UWONGO ni rahisi sana kwake kutengeneza UWONGO mwingine ili apate majibu ya kuwapatia watu wanaojaribu kuhoji. Kanisa Katoliki limetengeneza barua nyingi sana ambazo zote ni za uwongo. Barua zote hizi ama WARAKA hazipo ndani ya BIBLIA kabisa.

Mfano mzuri ni barua liliyoandikwa na Gaius kati ya mwaka 170 na 180. Barua hizi siyo za kweli hata kidogo. Maandiko mengine yanayohifadhiwa na Kanisa hilo ni kama The Apocryphal Acts of Peter. Kama maandiko haya yangekuwa Genuine yangejumuishwa kwenye Biblia. Nasema hivyo sababu wote tunajua kuwa vitabu vilivyojumuishwa kwenye Biblia vilijumuishwa kwa MWONGOZO wa ROHO MTAKATIFU. Kila andiko lililoachwa nje ya Biblia halikuwa sahihi kwa mafundisho ya KIKRISTO. MUNGU anatenda kazi sana na kuna watu wanafikiri ni rahisi tu kushindana naye. Kanisa katoliki linamilikiwa na Ibilisi na anafikiri atamshinda MUNGU, lakini kamwe hawezi kumshinda MUNGU.
Hv umesoma ukichoandika Sasa kama hizo barua kanisa katoliki wamezizuia unasemaje tena waongo
 
lete bandiko lingine linalosema petro alifia roma ili nijilizishe
 
Hii ndio ilikuwa nia yenu ovu ya kuuanzisha huu uzi wenu wewe na ids zako nyengine na wenzako. Lakini kinyume chake na nje ya matarajio yenu hapa tuna endelea kumjua Bwana Yesu zaidi na injili inachanja mbuga.
Tee tee tee!

Kwi kwi kwi

Naona mgalatia vyuma vimekukaza mpaka huoni pa kutokea.

Hatari sana unaanza kuchanganya watu na ID nyingine.

We endelea kupaluana magamba na mgalatia mwenzako akikushinda kachukue kikombe cha divai unywe tu ushushe koo.
 
Hivi chuki ya wasabato kwa wakatoriki chanzo chake ni nini? Maana historia inaeleza madhehebu mengi yametokana na ukatoriki, lakini huwezi mkuta msabato akikosoa warutheri.
 
Sisi hatuna vita na Wakatoliki, sisi tunapigana vita na IBILISI ambaye ndiye baba ya Wakatoliki, IBILISI ndiye baba ya UWONGO. Lengo letu ni watu waijue KWELI.

Mimi siyo MSABATO, mimi ni MKRISTO wa kweli ninayeishi kwa AMRI za MUNGU na IMANI ya YESU KRISTO.
Mkuu hapa umekosea.

Acha ngano na magugu yaote pamoja baadaye tutajua magugu na ngano.
 
Dhehebu la mama G White! Baada ya kupata anguko la kutabiri uongo mwisho wa dunia hawana kingine zaidi ya kutuhumu kanisa katoliki. But hawana impact.
 
Mi nachojua wasabato mtakimbia wenyewe huu uzi maana mnaendekeza uzushi.
 
Hivi bado kuna watu wanawaamini Roman catholic?
Watu waliodiriki kuificha bibilia kwa waumini aao mpaka miaka ya karibuni kidogo ndyo wamewaruhusu kuisoma.
Vinginevyo ni vimstari wamemega na kutengeneza misali yao.

Ndyo maana hata Amri ya kwanza wameifinya ili Wajinga waendelee kuabudu vinyago na masanamu.
Unavyoanza kusema Hao wakatoliki wakati wao ndo walifanya jitihada ya kukombine hiyo biblia. Yani walokole na wasabato utafikiri kunakipindi katika maisha yenu mlikaa chini mkafanya kama wakatoliki sometimes bora mwendele na Imani zenu muache kufuatilia mambo ya katoliki . Na mngejua kuwa wakatoliki hatupewi mafundisho ya kuhusu dini zingine ndo maana huwezi mkuta mkatoliki kaanzisha uzi kusema dhehebu lengine
 
Mimi sina dhehebu mkuu. Imeandikwa hivi; "Basi maana yangu ni hii, ya kwamba kila mtu wa kwenu husema, mimi ni wa Paulo, na mimi ni wa Apolo, na mimi ni wa Kefa, na mimi ni wa Kristo. Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulubiwa kwa ajili yenu? Au Je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo?" 1 WAKORINTHO 1:12-13

Wewe ukisema ni wa dhehebu fulani, Je! ulibatizwa kwa jina la dhehebu lako?? Nafikiri utakuwa umenielewa mkuu. Mimi sina dhehebu, mimi namwamini KRISTO na kuishi kwa kuzishika AMRI za MUNGU. Siyo kama sina dhambi au siyo kama sikosei, nakosea sana lakini, kwa IMANI nitaishi na kwa NEEMA za MUNGU wetu ninasamehewa makosa yangu.
Wala hakuna sehemu ya Biblia iliyotaja dini ya ukristo sasa kwanini wewe unajiita mkristo? Vivyo hivyo kwenye Biblia hakuna neno au dhehebu la katoliki, je ukristo ulipatikana vipi? Kumbuka kila mtu aliyekubali mafundisho ya Yesu aliitwa mkristo yaani mfuasi wa mpakwa mafuta lengo ni kurahisisha kujua watu fulani ni waumini wa imani fulani a.k.a dini/ dhehebu, mfano unaposema dini ya kiyahudi tunaelewa inamaanisha nini japo Ktk Bible hakuna dini ya kiyahudi. Vivyo hivyo katoliki limetokana na mtazamo uleule wa ukristo hii inathibitika kwa maana ya neno katoliki lenye maana ya mahali pote pote kwa yeyote yaani ukatoliki ni ukristo usio na mipaka wala ubaguzi kwahiyo ukatoliki haukufanyi wewe usiwe mfuasi wa kristo wala kukutenganisha na kristo. Documents nyingi za kiimani na mafundisho ya mitume yalitunzwa na wakatoliki na vyanzo vya madhehebu yote ya kikristo yalitokana na ukatoliki. Kifupi tu niseme mtu wenye matunda mazuri daima utaendelea kupopolewa na mawe. Wamisionari wa kikatolki ndiyo wameujenga na kuutetea ukristo hivyo ukatoliki unahitaji heshima yake siyo kebehi, inawezekana kuna mapungufu ktk ukatoliki kwakuwa ni wanadamu nasiyo malaika. Yesu alishaweka jiwe moja tu la msingi kila mkristo aweke tofali hapo sasa wengine wanakwenda kujenga sehemu nyingine ambapo Yesu hakuweka jiwe hapo. Binafsi sijawahi ona mafundisho yoyote ya kikatoliki yakipinga waprotestanti wakiwamo wasabato wala kuwakebei kwakuwa wanajua hadui yao mkuu siyo hao
 
Ngalia usipaliwe.

Tee tee tee!

Kwi kwi kwi

Naona mgalatia vyuma vimekukaza mpaka huoni pa kutokea.

Hatari sana unaanza kuchanganya watu na ID nyingine.

We endelea kupaluana magamba na mgalatia mwenzako akikushinda kachukue kikombe cha divai unywe tu ushushe koo.
 
Back
Top Bottom