The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 4,249
- 11,592
Mtazameni na msikilizeni huyu kada wa CCM kisha tia neno unapata ujumbe gani kupitia kwake kuhusu kesi ya Tundu Lissu....
Anamtaka Mwenyekiti wake taifa - CCM, Bi Samia Suluhu Hassan kumwachia Tundu Lissu kwa sbb eti "..inatia doa uongozi wake bora..!!"
Kwa wajuvi wa mambo ya propaganda za kisiasa za serikali na CCM yao, wanaweza ku - sense kitu kimoja tu, kwamba, wameshaona kuwa walichemka vibaya katika kutengeneza movie drama yao na sasa hawana jinsi na hawaoni wafanye nini kwa makosa yao ya kijinga yaliyotengenezwa ktk ofisi za Afande Muliro na RC Chalamila wa DSM dhidi ya TL...
Sasa wanawatanguliza watu wa dizaini hii watengeneze njia ya kuachiwa kwa TL ili baadae wajihami kisiasa kwa kusema, CCM imemshauri na Rais akasikia na kufanya. Ili waseme ni nani kama mama au mama anaupiga mwingi...!
We don't care...
Lililo vyema ni kuwa, kwa mlango wa nyuma, tunaona kwa uwazi kabisa kuwa, CCM wanaungana na Bunge la Jumuiya ya Ulaya - EU kuzitaka mamlaka za serikali ya Tanzania kumwachia Tundu Lissu huru bila masharti kwa kuwa mashitaka dhidi yake ni ya kisiasa, yaliyopikwa/bumbwa tu na kwa hiyo ya uongo mtupu wa kisiasa...
Hapa anaongea ktk namna ya kejeli mfano anam - address Tundu Lissu kama "Msingida", lakini hata hivyo nadhani anaweza kuwa na akili kidogo kwa kuuona ukweli...