Kadhia ya Law School "Wasomi Nguli" wasikilizwe


Mapesa yamejaa sikia: Hii inapaswa kuwa 100% practical legal training na siyo 50% theoretical (semester 1) kisha 50% legal practical training na mwisho kufanya mtihani wa mwisho wa Theory Paper!! Waliofeli wamefele mtihani wa mwisho uliobase kwenye theory!!

Suluhisho: Semister zote mbili zihusishe field placement maeneo mbali mbali ambako sheria hufanya kazi kwa vitendo kama mahakamani, makampuni ya mawakili, ofisi za mawakili wa serikali, takukuru nk Kuwe na rotations huko na assessment ifanyikie huko na hiyo assessment ifanywe na mawakili na mahakimu walioko huko field na si walimu wa chuo ambao hawana uzoefu wowote wa vitendo wao ni nadharia tu.
 
Prof Costa anawajua wanafunzi wa chuo chake Uwezo wao.

Ukiwauliza wakuu wa chuo,wangependa nyomi Kutoka vyuo vyao wasikwame mbele ya safari bila kujalisha wameiva au la.
 
Nafikiri itafika wakati ukweli usemwe. mimi kiasi nakubaliana na walimu wa LST kuwa huenda kushindwa kunachangiwa na kuwachukuwa wanafunzi wa ushindi wa wa chini, lakini haiwezekani wanafunzi wote zaidi ya mia sita walioshindwa walipata ushindi wa D form six. Sanasaana wanafunzi wa ushindi wa D hawafiki 25%. LST ingetaka kutumia ushindi wa chini kama kigezo, basi wangetuambia katika hao zaidi ya 600 ni asili mia ngapi walikuwa na ushindi wa D, hapo mimi ningewaamini.

Nimesikia wakisema kuwa hao wanafunzi hawajui hata kunyoosha senteso. Bila shaka hapa wanaongelea kunyoosha sentoso ya kiingereza. Lakini LST inatakiwa kukumbuka kuwa mahakama zetu ziko katika kuondokana na uenedeshaji wa kesi na uandikaji wa hukumu kwa Kingereza kwenda Kiswahili. Je, LST imefikiria labda kufundisha na kutoa mitihani kwa Kiswahili? Kama wahusika watakuwa wanatumia Kiswahili kuendesha shughuli za kimahakama ikiwa ni pamoja na utetezi, usikiliwaji wa kesi, kwa nini wahangaike kefundisha na kutoa mitihani kwa Kingereza.

Najuwa kutumia Kiswahili kunaweza kupunguza fursa zetu kutumikia mashirika ya kimaitaifa, lakini wapo wenye uwezo wa Kingerezana hao watatuwakilisha kama nchi zingine zisizotumia Kingereza na Kifaransa zinavyofanya
 
Kiswahili ni kigumu kuliko kiingereza. Angalia hata ktk mada za humu kwenye JF zinazoandikwa kwa kiswahili utaona makosa makubwa Sana.

Neno "ndiyo" wanaandika "ndio"
Neno "hebu" wanaandika "embu"
Neno "yaliyomo" wanaandika "yaliomo"

Hii ni baadhi tu ya mifano ya makosa yanayofanywa wakati wa kuandika ktk kiswahili.
 
Hivi ni 'Law School of Tanganyika' au 'Law School of Tanzania'?.
Nadhani tuanzie hapo.
 
Hawa maoni Yao unayasikiliza lkn sion kuyachukua Kama ndo majibu Sahihi, kuna WAtu wanamakasiriko na WAtu wafanyao Kazi LST pia

Ila watu wenye makasiriko na wanafunzi hawapo?

CV ya Prof Mahalu haikuwekwa pale kwa ajali. Huyu anaongea anachokijua.

CV yako Iko wapi ewe Tom, Dick au Harry?

Wewe si kama mrusi wa Buza tu mkuu?
 
Mkuu brazaj, kwanza asante kwa hii!.
Pili mimi namkubali sana Prof. Rick Costa Mahalu, toka kitambo!, wakati Mahalu akiwa balozi wetu Italy, mimi nilikuwa Italy nikitafuta maisha!. Maisha yakanigombea nikapata msala fulani, kama sio Prof. Mahalu na ofisa balozi fulani wa ubalozi wetu Italy, Mr. Nchemwa, sijui ningekuwa wapi!.

Prof. Mahalu abarikiwe sana!.
P
 
 
9 October 2022
Wenzetu wako mbali sana kuhakikisha mambo yanakuwa ya viwango vinavyokybalika toka chini kabisa

National Rounds of the 2022 Schools Moot Court Competition Programme currently underway at the University of Pretoria




Source : Department of Basic Education ZA

13 October 2022

Dar es Salaam, Tanzania

HOJA MEZANI II Wadau wa sheria na ugumu wa shule ya sheria kwa vitendo

Source : azam tv
 
WENDA umesoma shule za china , Kama sivyo basi wewe sio mtu wakujichanganya, we sema Mie mwanafunzi kumbe wakuta Mie boss wako kila siku twapishana kwenye korido,

Lakini kuwa mwanafunzi sikatai maana elim haina mwisho,

Kaa na jamii ,piga story na jamii utajua mengi Kama sio kujifunza mengi,
 

Unaongelea kiingereza? Aliyekuwa waziri wa elimu uliwahi kumsikia akikisokota? Vipi mwendazake hukuwahi kumsikia pia?

Kina Tom, Dick na Harry kukaa kwa kutulia si chaguo baya.
 
Acheni kumnukuu Shivji out of context:

Prof. Shivji na maoni yake kuhusu kadhia ya Law School

Shivji yuko broader. Education system in Tanzania has collapsed. Humo wapo wote mpaka primary.

Usimuwekee Shivji maneno mdomoni.

Rejea mada kutambua alichosema Mahalu:

“Hata hapa Saut niliwakuta walimu wa aina hiyo. Tumefanya kazi kubwa kumaliza tatizo hilo,”

"Wapenda ngono na wachawi siyo kwenu tu, hata kwetu wapo." --SAM.
 
Wasomi watapeliwa kirahisi, mwanafunzi wa chuo cha elimu asimulia kadhia

NINI KINAFANYA JAMII KUBWA TANZANIA RAHISI KUWAHADAA

Ni elimu isiyo ruhusu wasomi kuhoji


Source: SimuliziNaSauti
 
-mkuu hujasoma hiyo habari ukaelewa kwa ufasaha mbona ni lugha rahisi tu sio kama maswali ya LST
-Prof shivji ameunga mkono kikichosemwa na LST kupitia prof lukumay, kwamba tatizo ni vyuo vya sheria LL.B Kwamba hawaandaliwi vizuri, matokeo yake LST wanapokea half cooked students
-tafsiri yake ni kwamba Prof shivji amekubali kwamba tatizo ni vyuo vya LL.B
 

Hujamwelewa Shivji. Kumwelewa Shivji si kwa kila Tom.

Shivji ana matatizo na watanzania wote ukiwamo wewe akiambatanisha matatizo hayo na ku collapse kwa educational system.

Matokeo yake ule u arsenal na Man U na umuhimu wa u. Yanga na Simba dhidi ya yenye maslahi zaidi ya nchi.
 

Wana mfumo wa ajabu. Kila chuo kinapaswa kuwa na law school yake. Na jukumu la law school sio kumuandaa mtu kufaulu mtihani wa uwakili. Bar exam has nothing to do with law school. Sio kila law student anataka kufanya bar exam!
 
Wana mfumo wa ajabu. Kila chuo kinapaswa kuwa na law school yake. Na jukumu la law school sio kumuandaa mtu kufaulu mtihani wa uwakili. Bar exam has nothing to do with law school. Sio kila law student anataka kufanya bar exam!
before haijaja law school kulikuwa ba Bar exams
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…