Nadhani kuna vitu utakua unachanganya ukisikia neno Mkuu, imeelezwa hata hapo juu kuwa Tanzania kuna majimbo makuu (Archidiocesses) saba amabayo kila moja linaunda Ecclesiastical province kwenye mkutano wa TEC.
Kila Jimbo kuu linakua na majimbo yanayounda ukanda huo na linaongozwa na Askofu Mkuu.
Kuna Archidiocess za Arusha, Tabora, Mbeya, Dar es salaam, Mwanza, Songea na Dodoma.
Kuhusu Askofu Kilaini, aliondoka jimbo la Dar es salaam akiwa kama Askofu Msaidizi, Baba Mtakatifu kwa sababu zake (ofisi ya Vatican) haikuoni ulazima wa kumpa hadhi ya Askofu wa jimbo, bali akabaki askofu msaidizi na kuwa msimamizi wa jimbo hadi atakapopatikana askofu wa jimbo la Bukoba.
Nafasi ya msimamizi anaweza kupewa mtu yeyote, mfano baada ya kifo cha Askofu Banzi, jimbo la Tanga lilibaki chini ya usimamizi wa Padre Kiangio (ambae hakua askofu kwa wakati huo), baada ya Askofu Minde kuhamishiwa Moshi aliombwa kuendelea kubaki msimamizi wa jimbo la Kahama.