Kibinadamu na mtazamo wa kimtaa upo sahihi kwamba sisi tunakua tunauelewa tofauti na hivyo kudhani H.E Cardinal Rugambwa anamamlaka makubwa kuliko H.E Archbishop Ruzoka.
Lakini hapo unapoongelea kiutawala kwamba itasumbua sio kweli, utawala wao ni kwa kanisa na waumini wake, hakuna mahali Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa atatoa maamuzi binafsi kama hajapewa mamlaka hayo na Mhashamu Askofu Mkuu Rugambwa.
Mfano sahihi tunaupata katika jimbo kuu la Dar es salaam, Askofu Mkuu Ruwaichi alitoka Mwanza akiwa na mamlaka kamili ya Askofu Mkuu, lakini alipofika DSM akawa Askofu Mkuu mwandamizi, chini ya Kardinali Pengo.
Hakuwahi kufanya jambo lolote la maamuzi bila maelekezo ya Kardinali Pengo aliekua bado ni Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la DSM, ambalo lingeweza kuleta mkanganyiko.
Baada ya Kardinali Pengo kustaafu na kuachia rasmi Jimbo Kuu la DSM, ameendelea kubaki Kardinali (Cheo sawa na kile alichonacho Kardinali Rugambwa) lakini kimamlaka kwa jimbo kuu la DSM yupo chini ya Askofu Mkuu Ruwaichi, hawezi kufanya jambo lolote la kimaamuzi wala kiuchungaji isipokua kwa maelekezo kutoka kwa Askofu Mkuu Ruwaichi.