Kadinali Rugambwa ampokea Rais Samia Tabora

Kadinali Rugambwa ampokea Rais Samia Tabora

Kazi zingine za ajabu sana, Rais anaongea na Kardinali walinzi bado wako matakoni, wanahisi kajifunga mabomu ndani ya kanzu nini?
Kwanini wasitumie common-sense.
saa nyingine walinzi huwa kituko, juzi kwenye mkutano wa hadhara kwenye moja ya mkoa alioutembelea mlinzi mmoja aliyekuwa kwenye lango la ukaguzi kwa wanaongia uwanjani alimkemea vibaya mtoto mdogo aliyekuwa hafuati foleni ili akaguliwe ndio aingie. Mtoto hakuelewa kama kuna foleni ya kupekuliwa na kukaguliwa. Mi mwenyewe sikupenda ule ukaguzi nilipoambiwa nipandishe suruali na na kuacha tumbo wazi kana kwamba mlinzi alikuwa hana scanner. Hawa walinzi wako nyuma sana katika ulinzi hata USA hawako hivyo katika ulinzi wa rais wao wanamuachia faragha zake aongee na wenzake
 
Hiyo ni semantics tuu...kwa mfano ukisema Mbunge wa JMT au US Senator...mleta mada anaweza asiwe na uelewa mkubwa wa hierarchies za RC , lakini uwakilishaji wake hajakosea sana...Rugambwa ni Askofu Mkuu wa kanisa katoliki Nchini TZ ambaye kituo chake cha Kazi ni Tabora, kama mnakumbuka Ruwaichi alikua Mwanza akahamishiwa Dar...pia Protase ni kardinal ambaye kituo chake cha Kazi ni Tanzania...wenye kumbukumbu kuna interview alifanya Askofu kilaini na akasema kanisa katoliki TZ lina bahati kubwa sana kuwa na makadinali wawili ambao wanauwezo wa kumchagua Pope ,ikitokea vacancy...

Na kwa ranks ya kanisa ilivyo Rugambwa sio Askofu Mkuu wa kawaida..yeye ndie mshauri Mkuu wa pope kutokea kanisa katoliki Nchini Tanzania...

Huwezi kumwita PM Majaliwa au Mawaziri eti ni wabunge tuu kama kina kibajaji,Msukuma na wengine wa aina yao.
Hakuna mbunge wa JMTbali kuna bunge la jamhuri ya Muungano ambalo huundwa na wabunge na Rais.
 
Hivi protocol akiwepo Ruwaichi Askodu Mkuu Jimbo kuu Dar.Rugambwa Cardinal na Mkuu wa Jimbo kuu Tabora,Nyaihoza Chairman Tec. Kwenye utambulisho naanua na nani? Fuatilia hotuba ya waziri mkuu akiwa Tanga kumsimika Askodu wa Tanga.
Askodu Ruwaichi ndo Mkuu wa kanisa hata hivyo Kuna chombo kinaitwa Baraza la Maaskofu Chairman ni Nyaiongwa
Hii umeitoa wapi mkuu
 
Askofu Mkuu wa Kanisa katoliki nchini Tanzania, Kadinali Protase Rugambwa amekutana na Mhe Rais Samia Suluhu Hassan mkoani Tabora ikiwa ni mara ya kwanza tangu kuapishwa kwake.

Mara baada ya kuwasili Kadinali Rugambwa alimuombea Rais Samia sala maalum kumtakia heri katika uongozi wake.

Tabora ni nyumbani! Karibu sana Mama wa Taifa

Wale wanaosema Mama ana shida na TEC bado mko na msimamo wenu au?

Mwezi huu itakuja habari ambayo wengi wenu hamtoipenda, habari hiyo itakuja kabla ya maandamao yetu ya mchongo ya akina Mwabukusi. #MamaYukoKazini

Rais Samia Suluhu chuma hiki kimeaga kwao Kizimkazi.

View attachment 2785654
View attachment 2785655
View attachment 2785656
View attachment 2785657
View attachment 2785658
View attachment 2785659

Safi sana
 
Punguza ukali wa maneno.
Muadhama Protase Kardinali Rugambwa ni Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu la Tabora.
Hapa, neno 'Mwandamizi' maana yake ni "mwenye haki ya kurithi" cheo cha Uaskofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Tabora, pindi cheo hicho kitakapokuwa 'wazi'.
Cheo hicho kitakuwa wazi baada ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Tabora, Mhashamu Askofu Mkuu Paulo Ruzoka atakapofikisha umri wa miaka 75.
Kwa hiyo Muadhama Protase Kardinali Rugambwa ni "Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Tabora ' in waiting' till the day Archbishop Paul Ruzoka celebrates his 75th birthday.
Period.
Hapa 'kibinadam' lazma kuna shida mahali real or perceived.

Maana apo uyo cardinal ni mkubwa kwa 'perception' (sisi uku kitaani tunajua ivo na naamini hata serikali inajua ivyo ndo maana ata samia kaenda hapo).

lakini kiuhalisia uyo cardinal ni mdogo kwa huyo Askofu wa hapo kimamlaka (ndomaana hata kwene izo picha samia kaongozana na Askofu wa apo na sio uyo cardinal aliyemtembelea. kiutawala hii lazma itasumbua sana adi uyo cardinal atakapopewa ilo jimbo.
 
Kuna wakati ifike tuwe tunaona mambo katika uhalisia. Raisi yupo Tabora kwenye ziara zake za kikazi na baba kadinali yupo Tabora kwa hiyo raisi kwenda kumtembelea na kumsalimia baba kadinali sidhani kama ni ishu kubwa hasa ikizingatiwa kuwa ni hivi karibuni tu baba kadinali ndio kapata uteuzi. Na kwa watanzania kujuliana hali ni jambo la kawaida sana.
 
Hivi protocol akiwepo Ruwaichi Askodu Mkuu Jimbo kuu Dar.Rugambwa Cardinal na Mkuu wa Jimbo kuu Tabora,Nyaihoza Chairman Tec. Kwenye utambulisho naanua na nani? Fuatilia hotuba ya waziri mkuu akiwa Tanga kumsimika Askodu wa Tanga.
Kwanza kabisa hakuna protocal ya utambulisho kikanisa (masuala ya itifaki ni kwenye siasa),
kwa kuzingatia Hierarchy basi inapotokea ndani ya Jimbo Kuu la Tabora hivyo inabidi aanze kutambulishwa Bishop Ruzoka (maana ndie mwenyeji na Mkuu wa Kanisa mahalia), halafu Cardinal Rugambwa ndipo watafuata hao wengine kwa mlolongo wowote.

Unaweza kwenda Youtube kutazama utambulisho siku ya sherehe za miaka 125 ya Jimbo kuu Songea.
 
Hapa 'kibinadam' lazma kuna shida mahali real or perceived.

kiutawala hii lazma itasumbua sana adi uyo cardinal atakapopewa ilo jimbo.

Kibinadamu na mtazamo wa kimtaa upo sahihi kwamba sisi tunakua tunauelewa tofauti na hivyo kudhani H.E Cardinal Rugambwa anamamlaka makubwa kuliko H.E Archbishop Ruzoka.

Lakini hapo unapoongelea kiutawala kwamba itasumbua sio kweli, utawala wao ni kwa kanisa na waumini wake, hakuna mahali Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa atatoa maamuzi binafsi kama hajapewa mamlaka hayo na Mhashamu Askofu Mkuu Rugambwa.

Mfano sahihi tunaupata katika jimbo kuu la Dar es salaam, Askofu Mkuu Ruwaichi alitoka Mwanza akiwa na mamlaka kamili ya Askofu Mkuu, lakini alipofika DSM akawa Askofu Mkuu mwandamizi, chini ya Kardinali Pengo.
Hakuwahi kufanya jambo lolote la maamuzi bila maelekezo ya Kardinali Pengo aliekua bado ni Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la DSM, ambalo lingeweza kuleta mkanganyiko.

Baada ya Kardinali Pengo kustaafu na kuachia rasmi Jimbo Kuu la DSM, ameendelea kubaki Kardinali (Cheo sawa na kile alichonacho Kardinali Rugambwa) lakini kimamlaka kwa jimbo kuu la DSM yupo chini ya Askofu Mkuu Ruwaichi, hawezi kufanya jambo lolote la kimaamuzi wala kiuchungaji isipokua kwa maelekezo kutoka kwa Askofu Mkuu Ruwaichi.
 
Watu
Usichukulie poa nguvu ya Kadinali wa kanisa katoliki,eti ceremonial.Huyo anaongea moja kwa moja na papa,ni mshauri wake,anaingia kwenye papal conclave.
Anao uwezo wa kuwasagia kunguni maaskofu wengine kwa papa
Muulize Kilaini kilichompata aliposema Kikwete chaguo la Mungu

Hakuna mbunge wa JMTbali kuna bunge la jamhuri ya Muungano ambalo huundwa na wabunge na Rais.
Kama unafikiria ndani ya mipaka Fulani, utadhani hivyo....but hapa tunaongelea dude kubwa hapa Duniani..ndio maana baadhi yetu tuna-base argument zetu katika uwanda huo.
 
Usichukulie poa nguvu ya Kadinali wa kanisa katoliki,eti ceremonial.Huyo anaongea moja kwa moja na papa,ni mshauri wake,anaingia kwenye papal conclave.
Anao uwezo wa kuwasagia kunguni maaskofu wengine kwa papa
Muulize Kilaini kilichompata aliposema Kikwete chaguo la Mungu
Si kweli. Hana hiyo nguvu. Someni basi Church hierarchy. Navoandika ninaifahamu vizuri ndio maana nawashangaa mpaka wakatoliki hawajui.
 
Punguza ukali wa maneno.
Muadhama Protase Kardinali Rugambwa ni Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu la Tabora.
Hapa, neno 'Mwandamizi' maana yake ni "mwenye haki ya kurithi" cheo cha Uaskofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Tabora, pindi cheo hicho kitakapokuwa 'wazi'.
Cheo hicho kitakuwa wazi baada ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Tabora, Mhashamu Askofu Mkuu Paulo Ruzoka atakapofikisha umri wa miaka 75.
Kwa hiyo Muadhama Protase Kardinali Rugambwa ni "Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Tabora ' in waiting' till the day Archbishop Paul Ruzoka celebrates his 75th birthday.
Period.
I agree. Na jurisdiction yake mwisho ni hapo hapo Tabora sio nchi nzima. Ndio kitu wanasiasa na lay people don't get.
 
Kibinadamu na mtazamo wa kimtaa upo sahihi kwamba sisi tunakua tunauelewa tofauti na hivyo kudhani H.E Cardinal Rugambwa anamamlaka makubwa kuliko H.E Archbishop Ruzoka.

Lakini hapo unapoongelea kiutawala kwamba itasumbua sio kweli, utawala wao ni kwa kanisa na waumini wake, hakuna mahali Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa atatoa maamuzi binafsi kama hajapewa mamlaka hayo na Mhashamu Askofu Mkuu Rugambwa.

Mfano sahihi tunaupata katika jimbo kuu la Dar es salaam, Askofu Mkuu Ruwaichi alitoka Mwanza akiwa na mamlaka kamili ya Askofu Mkuu, lakini alipofika DSM akawa Askofu Mkuu mwandamizi, chini ya Kardinali Pengo.
Hakuwahi kufanya jambo lolote la maamuzi bila maelekezo ya Kardinali Pengo aliekua bado ni Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la DSM, ambalo lingeweza kuleta mkanganyiko.
Baada ya Kardinali Pengo kustaafu na kuachia rasmi Jimbo Kuu la DSM, ameendelea kubaki Kardinali (Cheo sawa na kile alichonacho Kardinali Rugambwa) lakini kimamlaka kwa jimbo kuu la DSM yupo chini ya Askofu Mkuu Ruwaichi, hawezi kufanya jambo lolote la kimaamuzi wala kiuchungaji isipokua kwa maelekezo kutoka kwa Askofu Mkuu Ruwaichi.
Mkuu hayo mambo sio rahisi kama unavoandika hapa kumbuka hawa ni binadam tena ni binadam wa ngozi nyeusi! wana feelings pia kama binadam mwingine yyote.

unakumbuka yaliyotolewa wakati ruwaichi amehamia apo dar?
 
Kwahiyo sasa topic ni who is who kwenye system ya Roman Catholic church!? Nilidhani mtoa mada alikusudia kutufahamisha kuhusu ugeni wa Rais kwa Kardinali Rugambwa na jinsi alivyotafuta nafasi katika ratiba yake ngumu kupata fursa ya kumtembelea na kumpa Pongezi za kuteuliwa kwake kuwa Kardinali. Ningependa kupata maoni ya wadau kuhusu tukio Hilo, unless interest zenu ni kwenye vyeo vyao na nani ni nani katika uongozi wa kanisa katoliki Nchini Tanzania.
 
Askofu Mwandamizi Jimbo kuu la Tabora, Kadinali Protase Rugambwa amekutana na Mhe Rais Samia Suluhu Hassan mkoani Tabora ikiwa ni mara ya kwanza tangu kuapishwa kwake.

Mara baada ya kuwasili Kadinali Rugambwa alimuombea Rais Samia sala maalum kumtakia heri katika uongozi wake.

Tabora ni nyumbani! Karibu sana Mama wa Taifa

Wale wanaosema Mama ana shida na TEC bado mko na msimamo wenu au?

Mwezi huu itakuja habari ambayo wengi wenu hamtoipenda, habari hiyo itakuja kabla ya maandamao yetu ya mchongo ya akina Mwabukusi. #MamaYukoKazini

Rais Samia Suluhu chuma hiki kimeaga kwao Kizimkazi.

View attachment 2785654
View attachment 2785655
View attachment 2785656
View attachment 2785657
View attachment 2785658
View attachment 2785659
Hijab imempendezesha sana mama
 
Si kweli. Hana hiyo nguvu. Someni basi Church hierarchy. Navoandika ninaifahamu vizuri ndio maana nawashangaa mpaka wakatoliki hawajui.
Hana nguvu ya kuongea na papa?
Hana nguvu ya kuingia papal conclave?
Unapinga nini hapa?
Acha kukariri formalities za vitabuni
 
Back
Top Bottom