Kadogosa: Nauli ya Treni ya Mchongoko Dar - Dodoma itakuwa tsh 100,000 - 120,000

Nauli ya bus Shabibu, kwenda Dom ni kiasi gani? Ili tulinganishe. Ili shirika lao likikosa abiria wasianze kutafuta visingizio 🤔
 
Kwa hiyo mnaweka nauli kubwa ili mabasi yaendelee duuh
 
Kwani serikali ina lengo gani hasa mpaka imeamua kuweka nauli kubwa kiasi hicho? Au wana nia ya kuihujumu ili kuyalinda mabasi na malori yao yaliyotapakaa kote nchini!!
 
tutaendelea kubaki na akina kimbinyiko, shabiby,ABC,ngasere na abood
 
mkuu nashukuru kwa uchambuzi huu, kama unaweza kunielezea zaidi nielezee mkuu
Halafu mbona hii treni ni tofauti na zile za marekani, china na japan hii ya kwetu ina pua pana kama ya kinjekitilingwale embu ona hapa chini👇

Ya Marekani ipoje tuma picha? Zingatia Marekani
 
Ewura ni energy and water utilities regulatory authority hii ni mambo ya petrol,gas nishati kwa ujumla na maji. Usafiri majini ni Tasac.
Sumatra ilivunjwa ikaundwa Latra na Tasac.
Duuh hivi kumbe niliandika EWURA, asee sijui hata akili ilikuwa wapi yani wewe ndio umenishitua, shukrani mkuu nilimaanisha TASAC nikajikuta nimewaandika hao wapanga bei za mafuta
 
Speech ya Masanja nimeipenda.
Treni za umeme hazijaja kuchukua nafasi ya mabasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…