Kadogosa: Nauli ya Treni ya Mchongoko Dar - Dodoma itakuwa tsh 100,000 - 120,000

Kadogosa: Nauli ya Treni ya Mchongoko Dar - Dodoma itakuwa tsh 100,000 - 120,000

Hapana LATRA inadeal na usafiri wa nchi kavu tu yani both barabara na reli, EWURA ndio wanadeal na usafiri wa majini, zamani kipindi zimeungana ilikuwa inaitwa SUMATRA ila kwa sasa kila moja inajitegemea
Ewura ni energy and water utilities regulatory authority hii ni mambo ya petrol,gas nishati kwa ujumla na maji. Usafiri majini ni Tasac.
Sumatra ilivunjwa ikaundwa Latra na Tasac.
 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema bei za treni za mchongoko zitakuwa Tsh. 100,000 hadi 120,000 kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma ambapo treni hizo zitakuwa ni express ambazo hazitosimama kila kituo bali kutoka Dar es salaam zitasimama Morogoro kisha Dodoma .
Kwahiyo tutalipia mchongoko siyo huduma ya usafiri!!
 
Unapata huduma ipi kwenye Royal business na business ya kawaida? Sijui wana massage ndani yake.
 
Wabongo hamna jema juzi LATRA walitangaza bei kwa daraja la kwaida mkafurahi sana
Leo hii wenye tren yao wametangaza bei kwa madaraja ya juu mnalalamika sasa kama mtu hamudu bei kubwa ya daraja la juu si unapanda daraja la kawaida pana cha kulalamika apo ?
 
Wanasiasa wanajenga miradi wakijiwazia wao kama watumiaji wakuu, ndiyo ninachokiona hapa. Kwa nini uwe na train tofauti badala ya kuweka classes kwenye treni hiyo hiyo? Dar-Morogoro ilitakiwa isizidi 10K maana vituo vyake kwanza siyo rafiki, mtu kuungaunga mpaka ufike kwako gharama zinarudi zile za basi.

Barabara kuu za mikoani (Super Highways) zingepanuliwa zikawa kama ile ya Mbezi/Kimara njia tatu kila upande, ukawaachia watu wajinafasi Morogoro ni masaa 2 tu kwa gari na usingesikia viajali hivi vya kipuuzi. Badala yake wamejenga vibarabara vya mtaani kwa safari za masafa marefu wakati wao wakisafiri barabara zinafungwa ili wapae wanavyotaka.
Mlikuwa wapi kumwambia Jiwe? Si mlishangilia? Shangilieni na saizi
 
Mkurugenzi wa TRC Kadogosa amesema nauli ya Treni ya Mchongoko( Mjusi) itakuwa Kati ya tsh 100,000 - 120,000

Source: Swahili Times

Mlale Unono 😃😃
=========


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema bei za treni za mchongoko zitakuwa Tsh. 100,000 hadi 120,000 kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma ambapo treni hizo zitakuwa ni express ambazo hazitosimama kila kituo bali kutoka Dar es salaam zitasimama Morogoro kisha Dodoma .

Akiongea Jijini Dar es salama leo June 12,2024, Kadogosa amesema “LATRA wametangaza nauli za daraja za kawaida lakini tutakuwa na treni za aina tatu, treni za kawaida ambazo zinasimama kote, tutakuwa na treni za express ambayo ikitoka hapa inasimama Morogoro, Morogoro - Dodoma lakini pia tutakuwa na treni nyingine ambayo ni high class zaidi zile za mchongoko tumeshaanza kuifanyia majaribio lakini June 16,2024 tutapokea nyingine mbili”

“Mule ndani kuna class mbili economy na business lakini ile nyingine kuna business lakini pia kuna Royal business kuna sehemu wanakaa Watu 48 tu na nyingine wanakaa chini ya hao Watu, business tutaenda kwa Tsh. elfu 70, katika ile ya mchongoko Royal tutaenda kwa Tsh. 120000 na business ya kawaida laki 1 na itakuwa express”

“Tunafanya hivyo Ndugu Waandishi wa Habari naomba hili mliweke vizuri tunajaribu ku-accomodate Watu wote, kuna zile ambazo mmetangaziwa, najua Watu watalalamika lakini hatuwezi kuwa na mentality ileile”

Itakumbukwa hivi karibuni Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) ilitangaza maamuzi ya Bodi ya Wakurugenzi ya LATRA kuhusu nauli za abiria wa daraja la kawaida kwa Treni ya Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Makutupora baada ya kufanyia kazi maombi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na maoni ya Wadau wengine ambapo Dar es salaam hadi Morogoro (KM 192) nauli ni Tsh. 13000 na Dar es salaam hadi Dodoma (KM 444) nauli ni Tsh. 31000.
#MillardAyoUPDATES

Pia Soma: Hizi hapa Nauli Mpya za SGR: Dar - Moro Tsh. 13,000, Dar - Dodoma Tsh. 31,000
Hizi nauli za kupanga kwa ubutu na mchongoko badala ya gharama ya nishati na uendeshaji ni za uswahili, panga hivyo atakayeweza atapanda asiyeweza shauri yake.
 
Hapana LATRA inadeal na usafiri wa nchi kavu tu yani both barabara na reli, EWURA ndio wanadeal na usafiri wa majini, zamani kipindi zimeungana ilikuwa inaitwa SUMATRA ila kwa sasa kila moja inajitegemea
EWURA 😳😳

😂🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom