Kadogosa: Nauli ya Treni ya Mchongoko Dar - Dodoma itakuwa tsh 100,000 - 120,000

Kadogosa: Nauli ya Treni ya Mchongoko Dar - Dodoma itakuwa tsh 100,000 - 120,000

Mkurugenzi wa TRC Kadogosa amesema nauli ya Treni ya Mchongoko( Mjusi) itakuwa Kati ya tsh 100,000 - 120,000

Source: Swahili Times

Mlale Unono 😃😃
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema bei za treni za mchongoko zitakuwa Tsh. 100,000 hadi 120,000 kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma ambapo treni hizo zitakuwa ni express ambazo hazitosimama kila kituo bali kutoka Dar es salaam zitasimama Morogoro kisha Dodoma .

Akiongea Jijini Dar es salama leo June 12,2024, Kadogosa amesema “LATRA wametangaza nauli za daraja za kawaida lakini tutakuwa na treni za aina tatu, treni za kawaida ambazo zinasimama kote, tutakuwa na treni za express ambayo ikitoka hapa inasimama Morogoro, Morogoro - Dodoma lakini pia tutakuwa na treni nyingine ambayo ni high class zaidi zile za mchongoko tumeshaanza kuifanyia majaribio lakini June 16,2024 tutapokea nyingine mbili”

“Mule ndani kuna class mbili economy na business lakini ile nyingine kuna business lakini pia kuna Royal business kuna sehemu wanakaa Watu 48 tu na nyingine wanakaa chini ya hao Watu, business tutaenda kwa Tsh. elfu 70, katika ile ya mchongoko Royal tutaenda kwa Tsh. 120000 na business ya kawaida laki 1 na itakuwa express”

“Tunafanya hivyo Ndugu Waandishi wa Habari naomba hili mliweke vizuri tunajaribu ku-accomodate Watu wote, kuna zile ambazo mmetangaziwa, najua Watu watalalamika lakini hatuwezi kuwa na mentality ileile”

Itakumbukwa hivi karibuni Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) ilitangaza maamuzi ya Bodi ya Wakurugenzi ya LATRA kuhusu nauli za abiria wa daraja la kawaida kwa Treni ya Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Makutupora baada ya kufanyia kazi maombi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na maoni ya Wadau wengine ambapo Dar es salaam hadi Morogoro (KM 192) nauli ni Tsh. 13000 na Dar es salaam hadi Dodoma (KM 444) nauli ni Tsh. 31000.
#MillardAyoUPDATES
 
Kiranga Nyani Ngabu hivi ndugu zetu bei ya treni hizo za umeme zimekaaje huko duniani tupeni mifano ya sehemu yenye umbali kutoka dar mpaka dodoma na muda zinazotumia?

Linganisha huko duniani na bongo kwenye hivi vipengele utapata jibu:
  • Operating Costs.
  • Fuel/power Prices.
  • Train Type and Age.
  • Route Demand and Competition.
  • Seat Inventory Management.
  • Time of Booking.
  • Class of Service and Ancillary Fees.
  • Economic Conditions.
 
Linganisha huko duniani na bongo kwenye hivi vipengele utapata jibu:
  • Operating Costs.
  • Fuel/power Prices.
  • Train Type and Age.
  • Route Demand and Competition.
  • Seat Inventory Management.
  • Time of Booking.
  • Class of Service and Ancillary Fees.
  • Economic Conditions.
mkuu nashukuru kwa uchambuzi huu, kama unaweza kunielezea zaidi nielezee mkuu
Halafu mbona hii treni ni tofauti na zile za marekani, china na japan hii ya kwetu ina pua pana kama ya kinjekitilingwale embu ona hapa chini👇
 

Attachments

  • CDBDF1FC-7A16-4AD6-A417-1635D4AA3237.jpeg
    CDBDF1FC-7A16-4AD6-A417-1635D4AA3237.jpeg
    107.7 KB · Views: 4
Wanasiasa wanajenga miradi wakijiwazia wao kama watumiaji wakuu, ndiyo ninachokiona hapa. Kwa nini uwe na train tofauti badala ya kuweka classes kwenye treni hiyo hiyo? Dar-Morogoro ilitakiwa isizidi 10K maana vituo vyake kwanza siyo rafiki, mtu kuungaunga mpaka ufike kwako gharama zinarudi zile za basi.

Barabara kuu za mikoani (Super Highways) zingepanuliwa zikawa kama ile ya Mbezi/Kimara njia tatu kila upande, ukawaachia watu wajinafasi Morogoro ni masaa 2 tu kwa gari na usingesikia viajali hivi vya kipuuzi. Badala yake wamejenga vibarabara vya mtaani kwa safari za masafa marefu wakati wao wakisafiri barabara zinafungwa ili wapae wanavyotaka.
 
Kadogosa mdogo kama jina lake

Kwani hawakuwa na andiko la mradi business plan) kabla ya kuanza

Au wanataka wajifelishe tnen wahallalishe kuiuza reli kama ilivyo bandari
Mbali ya Kudogosha, Mkuu umeandika pointi moja kubwa sana.

Si mda mrefu, utaeleweka zaidi.

Wenye jicho la tatu tunaelewa.

Wana tuchanganya wananchi "Wanyonge" tuli ahidiwa sote tutaipanda.

Kodi nzima ya nyumba, pwaa, kwenda kutoa maoni Bungeni na kurudi tu. Sijalala, sijakula. na hivyo ndio washasema hakuna kubeba mihogo na juisi ya miwa, yaani chakula mule. Mama weee!

Muda utaongea.
 
Hii nchi kuna wapuuzi na wapumbavu wengi sana,sasa kwani amesema gharama za watu wote ni 10000‐120000?
Wewe jipange kwenye madaraja ya chini ya hapo,hata ndege ziko hivyo.
Yani unataka upande Royal class kwa bei ya common mwananchi?
Hata Shabiby ana gari ya 29000,35000 na 45000 kwenda the same point
Na mwisho tutafute hela tuache ujinga
 
Back
Top Bottom