Kadogosa: Safari za SGR kutoka Dar - Moro zimechelewa kwasababu ya hatuna Vichwa vya Treni

Vikitarajiwa kuletwa siku za karibuni, ili safari ya Dar es Salaam Morogoro ianze mara moja.
 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema ujenzi wa reli ya kisasa kipande cha Dar es salaam - Morogoro umekamilika kwa 100% na mabehewa zaidi ya 45 tayari yamewasili nchini lakini kilichosimamisha safari kuanza ni kuchelewa kwa vichwa vya treni ambapo hadi sasa kimefika kichwa kimoja huku vingine vikitarajiwa kuletwa siku za karibuni.

Akiongea leo Ikulu Dar es salaam wakati Viongozi mbalimbali wakitoa taarifa kwa Waandishi kuhusu ziara za Rais Dkt. Samia Morocco na Saudi Arabia, Kadogosa amesema;

“Ujenzi wa reli hususani Dar es salaam - Morogoro kwa sehemu kubwa tumekamilisha takribani 100%, kuna sehemu chache sana ambazo nafikiri hata nyinyi mtakuwa mnaziona pale Vingunguti, Nyerere na Banana kuna kumalizia, then kuna ujenzi wa kuingia Bandarini ambao hautuzuii sisi kuanza uendeshaji kwa maana ya Dar es salaam kwenda Morogoro.

“Kitu ambacho kimetusimamisha kwa muda ni kwasababu tulikuwa hatujapata vichwa hilo tu, sasa hii inaweza kuwa na maelezo mengi sana kwamba kwanini vichwa vimechelewa lakini tumekuwa na changamoto hiyo ya kutokupata vichwa vya treni, mabehewa yapo pale Pugu mengi zaidi ya 45 mapya yote lakini kichwa tulikuwa hatuna, kwa mara ya kwanza kichwa cha kwanza kimeingia hivi karibuni.

“Kwanza wanaoleta kichwa kwasababu ni kichwa kipya kabla hawajatupa lazima wakifanyie testing, wamekifanyia majaribio kwao kwenye reli yao na ujue reli sio zinafanana, ya kule tofauti na huku kwahiyo ni lazima afanye testing pia hapa kujihakikishia kile kichwa kinaenda KM 160 kwa saa na tutawaita Waandishi wa Habari mshuhudie hilo.”
Akamatwe na ashitakiwe " kwa sauti ya Mpina
 
Huyu poyoyo mhujumu uchumi kabisaaa......anafaa aende jela....
 
Endeleeni kupiga hizo chenji hadi 2025! Ni kitu gani kililerea hayo yote kufanyika? Je Ina maana vichwa vimeagizwa kwengineko tofauti na behewa?? Je vitaendana na hitaji?
Duuuh imeenda hiyo!!
 
Hiyo treni haitachukua muda, itahujumiwa tu vinginevyo wabinafsishe vile hakuna mtizii atakayeiendesha kwa maslahi ya Serikali.

Angalia mradi wa mabasi ya mwendokasi
Na ndicho kitakachotokea. Maana Vigogo wengi wa chama na serulikali, pamoja na wafanyabiashara wakubwa waliojificha kwenye kichaka cha CCM; ndiyo hao hao wanaomiliki mabasi ya abiria na pia malori ya mizigo.
 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema ujenzi wa reli ya kisasa kipande cha Dar es salaam - Morogoro umekamilika kwa 100% na mabehewa zaidi ya 45 tayari yamewasili nchini lakini kilichosimamisha safari kuanza ni kuchelewa kwa vichwa vya treni ambapo hadi sasa kimefika kichwa kimoja huku vingine vikitarajiwa kuletwa siku za karibuni.

Akiongea leo Ikulu Dar es salaam wakati Viongozi mbalimbali wakitoa taarifa kwa Waandishi kuhusu ziara za Rais Dkt. Samia Morocco na Saudi Arabia, Kadogosa amesema;

“Ujenzi wa reli hususani Dar es salaam - Morogoro kwa sehemu kubwa tumekamilisha takribani 100%, kuna sehemu chache sana ambazo nafikiri hata nyinyi mtakuwa mnaziona pale Vingunguti, Nyerere na Banana kuna kumalizia, then kuna ujenzi wa kuingia Bandarini ambao hautuzuii sisi kuanza uendeshaji kwa maana ya Dar es salaam kwenda Morogoro.

“Kitu ambacho kimetusimamisha kwa muda ni kwasababu tulikuwa hatujapata vichwa hilo tu, sasa hii inaweza kuwa na maelezo mengi sana kwamba kwanini vichwa vimechelewa lakini tumekuwa na changamoto hiyo ya kutokupata vichwa vya treni, mabehewa yapo pale Pugu mengi zaidi ya 45 mapya yote lakini kichwa tulikuwa hatuna, kwa mara ya kwanza kichwa cha kwanza kimeingia hivi karibuni.

“Kwanza wanaoleta kichwa kwasababu ni kichwa kipya kabla hawajatupa lazima wakifanyie testing, wamekifanyia majaribio kwao kwenye reli yao na ujue reli sio zinafanana, ya kule tofauti na huku kwahiyo ni lazima afanye testing pia hapa kujihakikishia kile kichwa kinaenda KM 160 kwa saa na tutawaita Waandishi wa Habari mshuhudie hilo.”
Wanajua hamna cha kuwafanya. Na hamna kweli
 
Kwa hiyo waliona waagize kwanza mabehewa hayo yote 45 bila kichwa hata kimoja. Walifikiri hayo mabehewa yatasafirije kwenye rail? Labda kwa upepo? Halafu anasema mradi umekamilika kwa takriban 100%. Baadaye anataja vitu kibao bado havijakamilika, na vichwa vya treni hakuna hata kimoja. Nabaki kujiuliza - hiyo ni project completeness ya 100% kweli? Drama on top of drama. Ukistaajabu ya Musa....
 
Nchi ngumu sana hii 😂
Yaani sababu za kijinga kabisa, unawezaje kupata behewa 40+ kwa wakati ushindwe pata kichwa kwa wakati? Halafu anakiri kuwa vingunguti bado reli haijamaliziwa so hicho kichwa bado hakiwezi fanya kazi
 
Kilometa 160 kwa saa, Aboud zitafute pa kwenda.
Watu ni wengi sana wapo watakaopenda treni na wapo watakaopenda bus na wapo watakaopenda ndege.Kuwalazimisha watu wote watumie usafiri wa aina moja ni utumwa.
 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema ujenzi wa reli ya kisasa kipande cha Dar es salaam - Morogoro umekamilika kwa 100% na mabehewa zaidi ya 45 tayari yamewasili nchini lakini kilichosimamisha safari kuanza ni kuchelewa kwa vichwa vya treni ambapo hadi sasa kimefika kichwa kimoja huku vingine vikitarajiwa kuletwa siku za karibuni.

Akiongea leo Ikulu Dar es salaam wakati Viongozi mbalimbali wakitoa taarifa kwa Waandishi kuhusu ziara za Rais Dkt. Samia Morocco na Saudi Arabia, Kadogosa amesema;

“Ujenzi wa reli hususani Dar es salaam - Morogoro kwa sehemu kubwa tumekamilisha takribani 100%, kuna sehemu chache sana ambazo nafikiri hata nyinyi mtakuwa mnaziona pale Vingunguti, Nyerere na Banana kuna kumalizia, then kuna ujenzi wa kuingia Bandarini ambao hautuzuii sisi kuanza uendeshaji kwa maana ya Dar es salaam kwenda Morogoro.

“Kitu ambacho kimetusimamisha kwa muda ni kwasababu tulikuwa hatujapata vichwa hilo tu, sasa hii inaweza kuwa na maelezo mengi sana kwamba kwanini vichwa vimechelewa lakini tumekuwa na changamoto hiyo ya kutokupata vichwa vya treni, mabehewa yapo pale Pugu mengi zaidi ya 45 mapya yote lakini kichwa tulikuwa hatuna, kwa mara ya kwanza kichwa cha kwanza kimeingia hivi karibuni.

“Kwanza wanaoleta kichwa kwasababu ni kichwa kipya kabla hawajatupa lazima wakifanyie testing, wamekifanyia majaribio kwao kwenye reli yao na ujue reli sio zinafanana, ya kule tofauti na huku kwahiyo ni lazima afanye testing pia hapa kujihakikishia kile kichwa kinaenda KM 160 kwa saa na tutawaita Waandishi wa Habari mshuhudie hilo.”
Ukweli ni kwamba kuna conflict of interest between decision makers
 
Kwa hiyo waliona waagize kwanza mabehewa hayo yote 45 bila kichwa hata kimoja. Walifikiri hayo mabehewa yatasafirije kwenye rail? Labda kwa upepo? Halafu anasema mradi umekamilika kwa takriban 100%. Baadaye anataja vitu kibao bado havijakamilika, na vichwa vya treni hakuna hata kimoja. Nabaki kujiuliza - hiyo ni project completeness ya 100% kweli? Drama on top of drama. Ukistaajabu ya Musa....
Ivi mabehewa 45 si ni almost treni 3 tu? Au hii treni ikoje? Kichwa kimoja kinabeba mabehewa mangapi?
 
Back
Top Bottom