Kuna watu wana Upendo wa asili kwa Watoto, siongelei kuwabaka, kwahiyo usichanganye mafaili.
Hata mimi ninao, Mimi nakaa kwenye appartment, kila nikiteremka mara nyingi nakuta watoto wanacheza, au wanalishwa etc, nje.
Huwa nawasalimia, naweza mshika mkono akiwepo mlezi namwambia twende, katacheka, nitatembea hatua 2 then nakarudisha kwa mlezi, ni eneo la uwazi na kawaida.
1. Sitegemei mtu aingize mtoto wa mtu kwake hata kama ana nia nzuri au anapenda watoto, huu ni ujinga kabisa.
2. Sitegemei mtu, bachelor au asiyeishi na mke aingize mtoto wangu kwake hata wa miaka 18 nikaona, tutauana, lipo wazi.
Ni lazima mtu mzima ajue mipaka yake, sio akwepe kesi, ajue, hizi ni logical limits za mie kucheza na watoto wa watu.