Kafulila: 2008 SYNOVATE walisema tatizo namba moja la Watanzania ni maji

Kafulila: 2008 SYNOVATE walisema tatizo namba moja la Watanzania ni maji

Sisi vijana wa zamani kidogo tulichota maji kwenye visima sijui ka.a watoto wetu wanafahamu visima
 
View attachment 3027430

Katika Ukurasa wake wa ( X ) zamani tweeter Mkurugenzi wa PPP-Cetre Tanzania Bw David Kafulila amesema kuwa utafiti uliofanywa na taasisi ya kitafiti ya Steadman au SYNOVETe mwaka 2008 ulibaini kuwa tatizo namna moja la Watanzania ni maji safi na Salama.

Kafulila amesema kuwa Rais Samia katika kukabiliana na tatizo hili namba moja la Watanzania amekuwa akitoa pesa nyingi pengine kuliko Marais wote tangu Uhuru wa nchi hii.

Kafulila anasema, kabla ya mwisho wa mwaka wa Fedha wa Kila mwaka na katika miaka mitatu ya Rais Samia bajeti ya maji imetekelezwa kwa zaidi ya asilimia 75 na 92 miezi minne kabla ya wakati uliokusudiwa.

Mkurugenzi huyo pia ananakili baadhi ya miaka ya Fedha huko nyuma kabla ya Rais Samia bajeti ya maji ilitekelezwa kwa chini ya asilimia 40.

Hii ndio tofauti ya Rais Samia na Wengine ndio maana Mzee Kikwete ametamka wazi kuwa Rais Samia katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo hakamatiki.

Hata hivyo takwimu zinaonesha upatikanaji wa Maji vijijini umepanda kutoka 70.1% mpaka 89.6% wakati upatikanaji wa Maji mjini umeongezeka kutoka 85% mpaka 90%.

#Mama Samia hakamatiki​
Kafulila ni Mwamba sana kwa hoja hata hivyo,
 
Ni wakati Muafaka wa Mheshimiwa Kafulila kupewa jimbo na wananchi hapo Mwakani maana ni hazina kwa Taifa.
 
Hao watafiti hawasemi ukweli, tatizo kubwa la Watanzania ni ujinga.
 
Mama Samia kapeleka magari ya kuchimbia visima kila mkoa Tanzania, tushindwe wenyewe tu.
Umeongea ukweli kabisa na huo ndio uhalisia wenyewe na kila mtu anaona juhudi kubwa za Mheshimiwa Rais wetu katika kumaliza tatizo la maji hapa Nchini.
 
Umasikini mbaya kuliko wote ni ule wa fikra.
Hii ndiyo changamoto inayojenga na kuimarisha msingi wa umasikini wa Tanzania na Africa ya weusi (waarabu na makaburu ni tofauti, kwa wale tuliofika kwao na tuna akili tuliona na kupata uzoefu).
Viongozi wetu na watumishi wa uma wanatakiwa kuelewa kwamba, tafiti za kweli na suluhu ya matatizo yetu itapatikana kwa wananchi wenyewe.
Sera ya elimu lazima ibadilishwe kuondoa elements za ile ya kikoloni.
Hizi elimu za kukariri ni changamoto.
Tunatakiwa pia kuhakikisha watoto na vizazi vijavyo, kuanzia gen z, kutokubaliana na ujinga, uwe kwa wenyewe au kutoka kwenye mamlaka za kiserikali, hivyo wataweza kushindana na kujenga taifa lao kufaidi duniani.
Hata hivyo, tunatakiwa kuwaanda na kuwadhibiti wasifanye fujo kama Kenya.
Kenya unataka kuifananisha na Tanzania, Unajua hata Kama Wakenye wangekuja Tanzania wasinge goma
 
Kenya unataka kuifananisha na Tanzania, Unajua hata Kama Wakenye wangekuja Tanzania wasinge goma
Toa maelezo yanayojitosheleza ukiainisha kutokufanana huko na pia ambacho kingewafanya wasigome.
Kupeana elimu ni muhimu sana kwa maendeleo ya taifa letu.
 
Back
Top Bottom