Kafulila: 2008 SYNOVATE walisema tatizo namba moja la Watanzania ni maji

Kafulila: 2008 SYNOVATE walisema tatizo namba moja la Watanzania ni maji

View attachment 3027430

Katika Ukurasa wake wa ( X ) zamani tweeter Mkurugenzi wa PPP-Cetre Tanzania Bw David Kafulila amesema kuwa utafiti uliofanywa na taasisi ya kitafiti ya Steadman au SYNOVETe mwaka 2008 ulibaini kuwa tatizo namna moja la Watanzania ni maji safi na Salama.

Kafulila amesema kuwa Rais Samia katika kukabiliana na tatizo hili namba moja la Watanzania amekuwa akitoa pesa nyingi pengine kuliko Marais wote tangu Uhuru wa nchi hii.

Kafulila anasema, kabla ya mwisho wa mwaka wa Fedha wa Kila mwaka na katika miaka mitatu ya Rais Samia bajeti ya maji imetekelezwa kwa zaidi ya asilimia 75 na 92 miezi minne kabla ya wakati uliokusudiwa.

Mkurugenzi huyo pia ananakili baadhi ya miaka ya Fedha huko nyuma kabla ya Rais Samia bajeti ya maji ilitekelezwa kwa chini ya asilimia 40.

Hii ndio tofauti ya Rais Samia na Wengine ndio maana Mzee Kikwete ametamka wazi kuwa Rais Samia katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo hakamatiki.

Hata hivyo takwimu zinaonesha upatikanaji wa Maji vijijini umepanda kutoka 70.1% mpaka 89.6% wakati upatikanaji wa Maji mjini umeongezeka kutoka 85% mpaka 90%.

#Mama Samia hakamatiki​
Samia mitano tena unataka hutaki ndio hivyo
 
Kafulila kwanini ameliongelea hili sasa? Atamponza huyo mama yake, kwa wakati huu 80% ya Dar kuna mgao wa maji wa HATARI.
Tofautisha mgao na watu kufikiwa na maji,

Anachozingumzia Kafulila ni Wananchi kufikiwa na maji sio mgao wa maji
 
Maji ni kweli maeneo mengi yamefika ila Tatizo ni kwamba hayatoki,

Unakuta maeneo mengi maji yanatoka mara moja moja sana
Nadhani kasi ya usambazaji wa maji iéndane na upatikanaji wa maji
 
Ila ni baaddhi tu ya maeneo kumbuka Kuna miundombinu imekuwa ya muda mrefu
Kama uchakavu wa miundombinu unasababisha kukosekana kwa maji hivi maana yake ni nini kweli? Au upatikanaji wa maji hauhusishi miundombinu?
 
Ila ni baaddhi tu ya maeneo kumbuka Kuna miundombinu imekuwa ya muda mrefu
Effectiveness ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma wanazostahili 24/7, bila kuleta kisingizio cha miundombinu. Kutoa huduma siku zote na mahali pote inajumuisha miundombinu. Bila miundombinu hakuna huduma bwashee!
 
Nadhani Kila kitu ni hatua Tanzania ni nchi kubwa sana
 
Nadhani Kila kitu ni hatua Tanzania ni nchi kubwa sana
Ukubwa wa nchi ni kisingizio tu, kwa sababu hata kule ambako miundombinu iko vizuri bado huduma siyo za uhakika. Tungekuwa effective ktk kutoa huduma, basi kule ambako tumeshafikisha miundombinu huduma zingekuwa za uhakika 24/7. Lakini mpaka sasa hakuna huduma hata moja tunayotoa kwa ufanisi!
 
Nadhani tuipe muda Serikali, Kila kitu ni hatua
 
Back
Top Bottom