Kafulila: Hata Ulaya ilijengwa kwa Mikopo toka Marekani Marshall Plan si dhambi kukopa ili kujenga miradi ya maendeleo kama SGR au JNHP

duuuh, Kazi ipo but this won't happen in our country,

Mifumo ya Tanzania ni so tested and testified sana
Kwetu madhara yatakuja kwa njia tofauti, pale ambapo maliasili zetu zitakapo vunwa mchana kweupe.
 
Ni kati ya vijana machachari bungeni, alihoji maswali ya msingi mpaka mafisadi wakachukia. Alipachikwa jina la tumbili. Ana kipaji cha kuongea kwa mantiki. Big up Kafulila.
Kafulila ni Mwamba sana kwenye kusimamia Rasilimali za Taifa
 
Mbona nguvu kubwa inatumika sana kuna nini?
 
Ni kati ya vijana machachari bungeni, alihoji maswali ya msingi mpaka mafisadi wakachukia. Alipachikwa jina la tumbili. Ana kipaji cha kuongea kwa mantiki. Big up Kafulila.
Maliasili ni Mali ya watoto wa Tanzania ni ngumu kwenda kwa wangeni,
 
Mama anaupiga mwingi sana apewe maua yake, Tuna taka maafisa wa Serikali waje humu wajibu hoja mbalimbali
 
Kukopa sio tatizo ila tatizo ni usimamizi wa mkopo husika na mara nyingi katika nchi yetu usimamizi wa mikopo si mzuri hali inayopelekea hasara. Hasara hii inatokana na mikono michafu ya wasimamizi (wapigaji) wanaopewa dhamana na kukosa weledi katika usimamizi, hali hii hupelekea lengo la mkopo kutofikiwa au kutekelezwa kwa kiwango cha chini.

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
Kafulila anajua sana aisee we proud of him

Watu wengine ni wepesi sana kudanganyika na propaganda.

Sasa kama Ulaya ilijengwa kwa mikopo walikopa kwa miaka 60 mfululizo kama sisi ....!!?

Siku nikisikia wamekopa pesa kwenda kuchimba chuma Mchuchuma na Liganga ndiyo nitaanza kuwasikiliza. Ila hii mikopo ya kwenda kujenga shule na zahanati kila mwaka ni uhuni mtupu....!!
 
HUYU NDO YULE TUMBILI?
 
Huyu amekuwa chawa namba moja; na kwa bahati mbaya sana kuwa mnadishaji wa nchi hii kiholela.

Kama anajuwa Ulaya ilivyojengwa, kwa nini sasa yeye ndiye awe Dalali Mkuu wa kunadi mali zetu?
Ulaya na wao walijipitisha pitisha kila sehemu kuuza mali zao?
Ndiyo, walichukua mikopo, na walikuwa mstari wa mbele kujenga wao, siyo kuwategemea wageni kama tunavyofanya sisi.
Ulaya nako waliuza misitu yao; mbuga zao za wanyama; kujengewa barabara za kulipia, wao wakiwepo tu wakishangaa kama tunavyoshangaa sisi?
 
Huyo Tumbli" ingetakiwa aone michango kama huu hapa, halafu arudi kueleza anachoeleza yeye.

Ulaya na Marekani wananchi wamewekeza, wamenunua 'bonds' kujenga barabara; yeye kutwa nzima anaimba PPP!
 
Nadhani ni vema ungeishambulia hoja yake kuliko kumshambulia Kafulila,

Kafulila amesema kukopa kwa malengo hasa ya miradi ya Maendeleo ni jambo jema,

Sasa kama. unahoja kinzani ulifaa kuiwasilisha ila sio kumshambulia mleta mada huo ni Ushamba.
 
Sasa kama mtu anakupa pesa na unailipa kwa riba ya 0.5% shida iko wapi hapo?

Kumbuke money depreciation value yake ni kubwa,

Acheni ushamba jisomeeni
 
Usimamizi ni mzuri ndio maana maendeleo ni makubwa sana kwa sasa kuliko pengine wakati wowote katika historia ya Taifa hili
 
Haka kajamaa, kameshiba pesa ya CCM, sasa hv kanatapika tu make no kama Malaya vile, unalinganisha USA na TZ? Katika kukopa? Sie tunakopa kulipa mishahara na kununua V8, wenzetu wanakopa kujenga viwanda, na kuweka Sera Bora za, uchumi, Tweeter, inamapato makubwa kuliko nchi zote za, Africa!
Yaani mwalimu wa primary akope, anunue dera,na kununua tv, ajiringsnishe na Bakheresa anayekopa kujenga viwanda!
 

Reasoning ya aina hii ni hatari sana! Unaona watu wengine wanafanya madudu, halafu na wewe unayafanya, na ukiuliza unajibu kwamba hata wengine wanafanya hivyo: wanaiba, wavuta bangi, wana madeni, wanaua, wanalawiti, etc. Kwa upande wangu, tufanye mambo kwa sababu tunaona ni mazuri kwetu na yanatusaidia na si kwa sababu hata wengine wanafanya hivyo. Hiyo siyo sababu ya msingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…