Kafulila: Ifikapo mwaka 2050 kipato cha kila Mtanzania kitakuwa kati ya TZS 12M na 20M pato la Taifa litafikia $700bn mara 9 zaidi ya leo

L

Lakini inflation ni undetermined, unprojectable huwezi kuisema Leo itategemea na matukio ya wakati huo kama Calamities na mengine
Hata mwaka huo kufika na GDP per capita ni undetermined, hatujui nani atafika, hatujui population itakuwa vipi, unprojectable, huwezi kusema leo, inategemea na matukio ya wakati huo kama calamities.

Hilo halijazuia ku project growth na GDP per capita. Kwa kutumia averages za growth za sasa.

Hata inflation ange project kwa average inflation figures za sasa na muendelezo wake.

Shilingi milioni 12 ya mwaka 2000 si sawa na milioni 12 ya mwaka 2025. Hivyo hivyo, milioni 12 ya mwaka 2025 si sawa na milioni 12 ya mwaka 2050.

Sasa anavyotuambia watu watapata milioni 12 mwaka 2050, anamaanisha nini?

Milioni 12 ya mwaka 2050 itaweza kununua nini?

Ukiambiwa milioni 12 ya mwaka 2050 itakuwa na thamani sawa na milioni 2 ya sasa bado utafurahia kupata milioni 12 mwaka 2050?
 
Dira ni prediction,

Inaweza ikawa juu zaidi au chini kidogo,

Swala la purchasing power linaendana na stability ya currency kwa wakati huo,

Kama Taifa kazi yetu kubwa iwe ni kuistabilize currently yetu against foreign currency exchange
 
Duuuuuuuu,hizi akili zingine zinachekesha sana.2025 walioahidi kuwa uchumi wa kati hawaizungumzi Tena wamekuja na 2050 wanawaona watanzania kama mazwazwa vile.
 
Yawezekana makadirio hayo yakaongeza Uchumi kwenye makaratasi huku kihalisia wachina, waarabu na wageni wengine.
Lazima serikali iwe na sera ya kuwafanya wananchi wake mabilionea kivitendo badala ya wageni kufaidi raslimali zaidi.
 
Dira ni prediction,

Inaweza ikawa juu zaidi au chini kidogo,

Swala la purchasing power linaendana na stability ya currency kwa wakati huo,

Kama Taifa kazi yetu kubwa iwe ni kuistabilize currently yetu against foreign currency exchange
Ili hizi projection ziwe na maana, wanatakiwa kuweka na projection za inflation.

Vinginevyo, unaweza kushangilia kipato kuongezeka kuwa shilingi milioni 12, wakati kiukweli kwa kipato hicho mwaka 2050, kwa gharama halisi za maisha, kipato kinaweza kuwa kimepungua kutoka cha sasa badala ya kuongezeka.

Huelewi wapi hapo?
 
Nani kukwambia mfumuko wa bei utakuwa mkubwa?
 
Yawezekana makadirio hayo yakaongeza Uchumi kwenye makaratasi huku kihalisia wachina, waarabu na wageni wengine.
Lazima serikali iwe na sera ya kuwafanya wananchi wake mabilionea kivitendo badala ya wageni kufaidi raslimali zaidi.
Hata Sasa hizo sera zipo na ndivyo inafanya
 
Wakati huo 20m kwa mwaka itakuwa kama milioni kwa sasa.
 
bila kusahau kilo ya sukari itakuwa 20,000/-tsh
 
Umeandika pumba sana ,Tulia unadike vizuri

Tatizo lenu ni uchawa tu hamjui Finance kabisa thamani ya hizo Dollar kwa mwaka kwa mtu kwa miaka 25 ijayo 2050 ni sawa na kiasi gani sasa? Wenzio niwabobea wa Finance ! wewe piga kelele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…