Kafulila: Kwa Utafiti uliopo ndani ya miaka 25 ijayo Tanzania italazimika kujenga uchumi sawa au zaidi ya Afrika ya Kusini ya leo

Kafulila: Kwa Utafiti uliopo ndani ya miaka 25 ijayo Tanzania italazimika kujenga uchumi sawa au zaidi ya Afrika ya Kusini ya leo

===
Akihojiwa na kituo Cha runinga Cha Clouds Media Group Mkurugenzi wa PPP -Centre Bw David Kafulila alikuwa na haya ya kusema "Tafiti zilionesha mwaka 2015 mahitaji ya miundombinu yaliyokuwepo mwaka 2015 yalijitosheleza kwa asilimia 30% tu ya mahitaji ya mwaka 2050.

Ukitazama mwenendo wa uchumi unaona kwamba Tanzania itahitaji kujenga uchumi mkubwa zaidi ya Afrika kusini ya leo ndani ya miaka 25. Hii inaokuonesha umuhimu wa kutumia PPP kufikia matarajio makubwa.

Tunachakata kupata mwekezaji kujenga barabara ya kisasa ya kulipia Kibaha - Chalinze mpaka Morogoro, wawekezaji wanajua pamoja na uwepo wa SGR ya kisasa bado mahitaji ya usafiri yataendelea kuwa makubwa kutokana na ukubwa wa uchumi unaojengwa "


=====

View attachment 3074274
Safi sana Kafulila
 
Mhhhhh......!!!! Kwanza najiuliza kwanini hii PPP iliundwa kama taasisi, ilifaa kuwa kuwa chini ya Tanzania Investment Centre kama kitengo. Haya mambo ya kafulia siyaelewagi. Huyu ndugu yake na Kibu hachelewi kutuingiza sokoni
Maswali yako nadhani ni ya watanzania wengi, unajiuliza kazi ya TIC ni nini sasa, anachoeleza Kafulila si ni uwekezaji ambayo ndio kazi ya TIC, hizi taasisi zinajichanganya zenyewe na ni matumizi mabaya ya kodi zetu.
 
Inabidi tufunguke kiakili kwanza ndipo tutaendelea.

Obama, baba yake alikuwa Mkenya akachguliwa kuwa Rais wa Marekani.

Trump, baba yake alikuwa Mjerumani na mama yake Mdcotland akachuguliwa kuwa Rais wa Marekani.

Kamila Harris, baba Mjamaika, Mama Mhindi kwa sasa ni Makamu wa Rais and the next President of the USA.

Sasa kama Kafulila amezaliwa hapa, kakulia hapa anakuwaje bado ni Mrundi...!!?
Urundi wake unaonekana pale tu anapotaka kuwa rais.
 
Maswali yako nadhani ni ya watanzania wengi, unajiuliza kazi ya TIC ni nini sasa, anachoeleza Kafulila si ni uwekezaji ambayo ndio kazi ya TIC, hizi taasisi zinajichanganya zenyewe na ni matumizi mabaya ya kodi zetu.
Uwekezaji TIC ni 100% private ila PPP ni Gvnt na private Kila mmoja anakuwa na share
 
Tahahira mwengine

Asiejua majukumu ya serikali kwenye ‘merit and public goods’ investments kwa faida zingine za uchumi na jamii.

Serikali ndio inaamua kwenye hizo investment anazoingelea Kafulila based on its political view points.

Na serikali nyingi duniani kwenye “public and merit’ goods particularly kwenye infrastructure projects and education ni majukumu yao (somewhat socialist) the bigger picture in doing so is the direct opportunities it creates hasa kwenye kufungua access za uwekezaji. Faida yake ni kutengeneza employment, kutumia resources na kulipwa kodi in the long run.

Linapokuja swala la kubinafsisha taasisi za kibiashara au ‘cost centres’ za serikali inataka financial information zake ziwe public ili jamii idadavue na kuona logic ya serikali kuwapa private sector na wao kuelezea justification namna watakavyo improve, serikali iwape targets on contracts wakishindwa kufukia wanyan’ganywe contract bssd on agreed terms.

Ni mtu anaejiropokea tu na kuaminishana mambo ya investments ni rahisi.
 
Huko kwingine wanajitambua sana na hutii sheria bila shuruti
Watu waungwana sana sio wababe baby na dharau kama kwingine.Sio rahisi mgeni akapenya kufikia uraisi kutoka huko kwingine

Kigoma mtu aweza shika ila Vetting yake sio ya kitoto imekakamaa hasa

Mbona Phillip Mpango ni makamu wa Raisi na anatokea Kigoma

Raisi kutoka kigoma Yawazekana ila Vetting yake kali kuliko kwingine
Hahahaaaa, kule usipokuwa makini unaweza kuingiza ndg yake na Nkurunzinza kuwa Raisi. Hata zedzedkei naye wanasema ni mtiizedi wa kuungaunga
 
Mhhhhh......!!!! Kwanza najiuliza kwanini hii PPP iliundwa kama taasisi, ilifaa kuwa kuwa chini ya Tanzania Investment Centre kama kitengo. Haya mambo ya kafulia siyaelewagi. Huyu ndugu yake na Kibu hachelewi kutuingiza sokoni
Nadhani uwezo wako wa kielimu pia ni mdogo ndio maana huwezi kutofautisha kati ya TIC na PPP
 
Wanajamvi Heshima kwenu,

Kwako Mh Dr Samia Suluhu Hassan Rais wetu mpendwa.

Nakuandikia kwa heshima na taadhima kuhusu kauli tata, aliyoitoa waziri Mkuu Majaliwa huko Tabora, kuwataka vijana wasomi wa vyuo vikuu kujiunga na vyuo vya VETA Kusomea ufundi wa fani mbalimbali.

Kwa upeo wangu wa kutafakari mambo naona Waziri Mkuu amevuka mstari,kwa kauli aliyoitoa.
Ni kauli

Mosi ya kudharau kada mbalimbali zilizosomewa na vijana chuo KIKUU mpaka kuwataka waziache.

Kada kama uhasibu, uhandisi ,Udaktari, Ujiolojia,ualimu, Procurement kuzitaja chache.

Watu hao juu wametumia muda mwingi,pesa kusoma kidato Cha kwanza mpaka Cha sita, Kisha miaka mitatu mpka minne chuo KIKUU.

Hili ni group kubwa la wanazuoni ambao wapo mtaani hawana ajira,walipokuwa wanasoma walikuwa na malengo yao,

Walijua kabisa VETA zipo, ukweli kuhusu VETA ni kada ya kati ya kawaida iliyokuwa na malengo ya kutoa skills study kwa ajili ya kujiajiri, kwa namna ya pekee watu ambao waliishia darasa la saba zamani, lakini sasa kidato Cha nne, ambao hawakuweza kuendelea na masomo ya juu ili wajiajiri.

Mh Rais mashaka yangu ni kuwa Kuna ombwe kubwa la ajira nchini, safari hii wapiga kura wengi nchini ni vijana, ambao hawana ajira.

Kwa Nini kauli kama hii inatoka kuelekea uchaguzi mkuu?? sio nzuri, itachochea chuki kwa vijana wasio na ajira ambao Bado wana matumaini na serikali Yako.

Kwa namna ilivyo vijana hao wamekuwa underrated, hadhi ya degree za vyuo vikuu ni bure, haina maana, mpaka leo hii vijana hao washauriwe kusomea ufundi🤔🤔🤔

Mwisho Mwishoni natamani Waziri Mkuu ajitafakari, na Mama kama mkuu wa nchi utafakari hii kauli tata, ambayo kwangu mimi kama mtanzania inatosha kwa Waziri Mkuu kukaaa pembeni baada ya Bunge kuvunjwa.

Ni imani yangu ujumbe huu utafika mezani kwako, kwa wewe mwenyewe kusoma, au kupitia wasaidizi wako.

Nandagala One -Mpumalanga South Africa.
 
Back
Top Bottom