Kafulila: Serikali inakopa T-bills kwa 5% wakati Msumbiji 17%, Kenya 16%, Malawi 16%, Zambia 10%, Namibia 9%, Uganda 9%, SA 8%. Uelekeo wetu ni sahihi

Kafulila: Serikali inakopa T-bills kwa 5% wakati Msumbiji 17%, Kenya 16%, Malawi 16%, Zambia 10%, Namibia 9%, Uganda 9%, SA 8%. Uelekeo wetu ni sahihi

Kumbe Kuna nchi zinazotamani kukopa kwa riba kubwa?
Siyo kutamani kukopa kwa riba kubwa ni kuwa hata mkopeshaji anakuwa anajua uwezo wako wa kuzalisha ziada. Kwa hiyo wakati wa mazungumzo huwezi kumdanganya. Kila kitu kiko wazi. Unafikiri ni kama wewe unavyopeleka fake audited financial statements kukopa benki na ukapewa mkopo based on those fake documents. Hata JPM aliwatimua kule NBAA auditors wanaozitoa hizo fake audited financial statements.
 
Still Tanzania is the best
 
Hili Mimi sikufahamu na sijui kama ni kweli lakini mwisho unakiri alikopa ndio maana Leo ni tajiri
Kwani mimi nimekataa nchi kukopa! Nachangia kuhusu kujisifu kukopa kwa riba ndogo. Ukweli mwingine ni kuwa lazima uwe na uwezo wa kuzalisha ziada ili uweze kurudisha mkopo.
 
 Ephen: Naomba unikopeshe laki 1, nitakurudishia wiki ijayo

Rafiki: kama unataka laki 1 riba ni 50% hivyo utanilipa 150,000

Ephen: Turahisishe mambo nipe laki 1, mimi nakupa Hati ya kiwanja cha familia yetu halafu wiki ijayo nakupa hela yako bila riba.

Rafiki: Sio kweli! Nachukua kiwanja na utanilipa riba ya 10%= 110,000

Ephen: Sawa! Asante kwa wema wako
Very funny, japo umeielezea nchi yako vizuri!!
 
Nadhani hoja ni rates Wala sio matumizi, Kumbuka unapokopa kwa 17% anayeumia ni Mwananchi,

Unadhani Mwananchi anauelipa riba ya 17% maumivu yake ni sawa na yule anayelipa riba 5%?
unachokisema wewe sio tafsiri ya kiuchumi inayotokana na hizo bills.hapo juu nimekupa sababu kwa nini Serikali ina offer hizo bills na bonds,but interest rates zake zinaamuliwa kwa njia ya mnada.
Hivyo basi ukiona matokeo baada ya mnada rates zipo chini maana yake demand ya investors imekuwa kubwa hadi imeshusha hizo rates na rates zikiwa kubwa maana investors wanaohitaji kuwekeza kwenye hizo bills wamekuwa wachache.

Mazingira ya biashara/uwekezaji ndani ya nchi ni determinant factor,ukiona rates zipo chini ujue demand ilikuwa kubwa na tafsiri yake watu wanaona ni ahueni kuweka pesa Bank kwa riba hiyo ndogo kuliko kuipoteza kwa kwenye biashara na kinyume chake.

Kwa kuhitimisha ni kuwa hiyo riba maana yake nchi kiuchumi tupo hovyo compare na hizo nchi ulizo orodhesha hapo-mfano hapo Kenya ametuzidi zaidi ya mara 3.
 
View attachment 3016052
CEO wa PPP Bwana David Kafulila katika Ukurasa wake wa tweeter ( X ) ameisifu Serikali ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa ndio nchi pekee inayokopa ndani kwa riba ndogo kuliko nchi nyingi za Africa.

Kafulila anasema Wakati Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inakopa T-bills kwa asilimia 5 lakini wenzetu uchumi wao ndani ni hoi ndio sababu Riba zao kwenye T-bills ziko juu mafano Msumbiji ni asilimia 17 Kenya ni asilimia 16, Malawi ni Asilimia 16, Zambia ni Asilimia 10,Namibia ni asilimia 9,Uganda ni asilimia 9 na Africa ya kusini ni asilimia 8 hiki ni kielelezo Cha uimara wa Uchumi wetu ndani katika ukanda wa Africa.

Wakati mnaendelea kumtukana msisahau pia kuwaambia hao Wananchi kuwa ni yeye pekee ndio aliyejenga unafuu wa maisha kwa watu wake katika ukanda mzima wa Africa na baadhi ya ushahidi ni hizo taarifa za David Kafulila huko tweeter ( X )

View attachment 3016048
Ifike wakati sasa haya yafanyike;
1. Kafulila awe Msemaji wa Serikali..au
2. Kafulila hizi data awe anampatia Msemaji wa Serikali ili azitoe..
Kafulila kuendelea kutoa hizo takwimu/taarifa kila kukicha kunaifanya ofisi ya Msemaji wa Serikali kupwaya.
 
Huyu jamaa ame concentrate kwenye maelezo ya kwamba tukope na sio ni nini tufanye au tunafanya na hio mikopo..., hata kama ingekuwa tunepewa kama zawadi kama hizo zawadi zinaishia kwenye matumbo ya watu basi hio ni gharama kubwa..., sababu tunabatizwa jina la ombaomba na tutaendelea kuomba mpaka kesho sababu tunachofanya hakina tija....
 
unachokisema wewe sio tafsiri ya kiuchumi inayotokana na hizo bills.hapo juu nimekupa sababu kwa nini Serikali ina offer hizo bills na bonds,but interest rates zake zinaamuliwa kwa njia ya mnada.
Hivyo basi ukiona matokeo baada ya mnada rates zipo chini maana yake demand ya investors imekuwa kubwa hadi imeshusha hizo rates na rates zikiwa kubwa maana investors wanaohitaji kuwekeza kwenye hizo bills wamekuwa wachache.

Mazingira ya biashara/uwekezaji ndani ya nchi ni determinant factor,ukiona rates zipo chini ujue demand ilikuwa kubwa na tafsiri yake watu wanaona ni ahueni kuweka pesa Bank kwa riba hiyo ndogo kuliko kuipoteza kwa kwenye biashara na kinyume chake.

Kwa kuhitimisha ni kuwa hiyo riba maana yake nchi kiuchumi tupo hovyo compare na hizo nchi ulizo orodhesha hapo-mfano hapo Kenya ametuzidi zaidi ya mara 3.
Acha kupotosha,ulichoeleza ndio kinyume chake maana inategemea kama Serikali inauza au inanunua T-Bills.

Mwisho Je malengo ya serikali Huwa hayafikiwi Kwa hizo hizo riba za chini?
 
Back
Top Bottom