Kafulila: Uchumi wa dunia ni US$ 105trilion 97% ni deni kukopa na kujenga ndio mpango mzima Duniani

Kafulila: Uchumi wa dunia ni US$ 105trilion 97% ni deni kukopa na kujenga ndio mpango mzima Duniani

Moja wapo ya ID za kujisifia za kafulila.
 
View attachment 3011907
===
David Kafulila, Mkurugenzi PPP TANZANIA katika ukurasa wake wa tweeter ( X ) amechambua haya,

Kafulila anasema, kukopa kwajili ya miradi ya maendeleo ndio njia sahihi na ndio mpango wa dunia nzima kwa sasa.

Kafulila anatufumbua macho kwamba nchi zote kubwa duniani tunazoziona zikimea zinajengwa kwa mikopo kwa wastani wa 97%

David anasema, wakati uchumi wa dunia umefikia US$ 105trilion, Deni lote la dunia ( serikali & private ) ni US$315trilion

Kwa lugha nyepesi,deni la serikali zote duniani limefikia US$ 97trilion sawa na 97% ya uchumi wa dunia,

Kafulila anasema deni lote la dunia kwa ujumla ni US$ 315 Trilioni zaidi ya 300% ya GDP ya dunia.

Vietnam ni nchi ya mfano duniani kwa muujiza wa kukuza uchumi ndani ya muda mfupi,

Mwaka 1990, uchumi wa Vietnam ulikuwa US$ 6.4bilion, mbele kidogo ya Tanzania iliyokuwa na US$ 4.5bilioni na nyuma ya Kenya iliyokuwa na US$ 8.4bilioni,

Lakini Leo miaka 30 baadae, uchumi wa Vietnam ni US$ 400bilion, karibu mara nne ya Kenya na mara tano ya Tanzania.

Hata hivyo, Mwaka 2007, wakati uchumi wa Vietnam ukiwa US$77bilion, sawa na Tanzania leo,

Mwaka huohuo wa 2007 uwiano wa deni kwa uchumi ulikuwa asilimia 43% karibu sawa na uwiano wa deni kwa uchumi wetu Tanzania.

Kukopa kujenga uchumi ndio njia na ndio Afya yenyewe ya nchi anasema David Kafulila.
View attachment 3011554
Acha ujinga we mjinga! Kwa rasilimali tulizo nazo tunaweza kuendesha nchi bila mikopo. Mnakopa bado hatuoni mnachokifanya,kazi kununuliana mavx na Prado za bei kubwa! Hadi ma rpc ambao wangeweza kutumia land cruiser hardtop. Mnatafuna pesa za walipa Kodi kwenda kuzurura na wasanii. Hovyo sana! Bado tumeona thread humu Mt Meru Hotel inachukuliwa Kwa USD million 45. Au ndio hiyo mikopo!?
 
Usitumie kichwa kubebea kamasi, hiyo barabara ya Dar Moro ijengwe na serikali yenyewe bila PPP, PPP ichukue miradi mikubwa ya kiuchumi. Haizidi bilioni 500 kuifanya iwe ya kisasa
Hawa watu sijui vichwa vyao vikoje!! Takataka kabisa. Mimi Nina hakika hata madini pekee yangetosha kuijenga barabara nchi nzima.
 
Nimegundua Kafulila anapendwa sana na Watanzania mkubali mkatae, Uaminifu unalipa sana
 
Kafulila anahitaji kujibiwa kisomi sio propaganda hizi zinazoendelea
 
Na anayenufaika ni mkopeshaji zaidi ya mkopaji....; Na unakopa ili ufanye nini ?

Yaani sababu wengine wanakopa na wewe uende kukopa ili ufanye vitu ambavyo ungeweza kufanya bila mkopo ? (kunjenga madarasa, vyoo n.k) By the way kama kila kitu tunawapa watu wafanye sisi tunakopa ili iweje ? Kwanini hicho tunachokopea ili tukifanye tusiwape hao watu wafanye ?

Hii awamu sio tu kwamba ina wapuuzi bali ina wapuuzi wanaodhani kila mtu ni mpuuzi hence insulting our intelliegence....
 
Back
Top Bottom