View attachment 3011907
===
David Kafulila, Mkurugenzi PPP TANZANIA katika ukurasa wake wa tweeter ( X ) amechambua haya,
Kafulila anasema, kukopa kwajili ya miradi ya maendeleo ndio njia sahihi na ndio mpango wa dunia nzima kwa sasa.
Kafulila anatufumbua macho kwamba nchi zote kubwa duniani tunazoziona zikimea zinajengwa kwa mikopo kwa wastani wa 97%
David anasema, wakati uchumi wa dunia umefikia US$ 105trilion, Deni lote la dunia ( serikali & private ) ni US$315trilion
Kwa lugha nyepesi,deni la serikali zote duniani limefikia US$ 97trilion sawa na 97% ya uchumi wa dunia,
Kafulila anasema deni lote la dunia kwa ujumla ni US$ 315 Trilioni zaidi ya 300% ya GDP ya dunia.
Vietnam ni nchi ya mfano duniani kwa muujiza wa kukuza uchumi ndani ya muda mfupi,
Mwaka 1990, uchumi wa Vietnam ulikuwa US$ 6.4bilion, mbele kidogo ya Tanzania iliyokuwa na US$ 4.5bilioni na nyuma ya Kenya iliyokuwa na US$ 8.4bilioni,
Lakini Leo miaka 30 baadae, uchumi wa Vietnam ni US$ 400bilion, karibu mara nne ya Kenya na mara tano ya Tanzania.
Hata hivyo, Mwaka 2007, wakati uchumi wa Vietnam ukiwa US$77bilion, sawa na Tanzania leo,
Mwaka huohuo wa 2007 uwiano wa deni kwa uchumi ulikuwa asilimia 43% karibu sawa na uwiano wa deni kwa uchumi wetu Tanzania.
Kukopa kujenga uchumi ndio njia na ndio Afya yenyewe ya nchi anasema David Kafulila.
View attachment 3011554