Akizungumza katika maadhimisho ya miaka mitatu ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan Mkurugenzi Mkuu wa Ubia nchini PPP Mhe David Kafulila amesema,
Nchi ya Tanzania kwa awamu hii ya sita imeamua kujikita zaidi kwa kuwekeza kwenye Sekta ya Kilimo ambayo inagusa Jamii kubwa ya Watanzania,
Kilimo ndio Sekta ambayo Kila Mtanzania inamgusa kwa namna moja au nyingine huko nyuma haikupewa kipaumbele sana kama ilivyo Leo,
Mathalani, Kilimo bajeti yake imekuwa kutoka TZS 230BL mpaka TZS 970BL karibu mara Nne ,
Sote tunafahamu zaidi ya 70% ya wakulima wote ni Wanawake ambao ni karibu Wanawake mil 28 wanategenea Kilimo na hata hivyo zaidi ya 64% ya Watanzania ambao ni karibu wakulima mil 40 ni wakulima huku zaidi ya 80% ya malighafi zote za viwandani zinatemea Kilimo.
View attachment 2947980