Kagame awatuhumu SADC na Ramaphosa kuwaunga mkono Congo. Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama SADC ni Rais Samia!

Kagame kweli kajaa kiburi!

Kwenye kurasa zake za Mitandao ya Kijamii amerusha Video akiongea kuhusu Mgogoro wa Congo jana kwenye kikao chake na Wakuu wa EAC

Kamgombeza kama mtoto mdogo Rais wa Afrika Kusini kuhusu majeshi yake yanavyoisaidia Congo.

Kawananga SADC ambayo mwenyekiti wa Kamati yake ya Siasa na Usalama ni Rais Samia kuhusu support wanayoitoa kwa Congo.

Ameongea kama yeye ndo mwenye Congo na hakuna wa kumfanya lolote lile.

Aisee acha niendelee kummiss Jakaya Kikwete. Acha niendelee kuwamiss Majenerali bora kabisa wa JWTZ ( Mwamunyange, Shimbo, Mella na Mwakibolwa)

Kiburi cha Kagame kimefikia kiwango cha juu kabisa na kutokana na ujinga wa hawa viongozi wa Afrika tulionao sasa nina uhakika anaenda kuimega rasmi Congo.

Where is my JWTZ?

View attachment 3218616
Kinachotia kichefchef ni kwamba wote wako EAC pamoja na South Sudan-wanaoishi na mitutu mikononi. Badala ya kuwatoa kwnye jumuia yetu wanapoteza muda kushauriana kuh. amani!! Wawaache wahangikie maisha yao wenyewe
 
basi sio kenge ni fisi maji, na wewe ndio fisimaji mwenyewe unayetaka kuleta stress
Kama unaweza kuongea na fisi maji basi na wewe ni fisi maji na wazazi wako walikuwa au ni fisi maji ndio maana wakamzaa fisi maji anayeongeana fisi maji! Fisi maji oyeee!!!!
 
Kagame kweli kajaa kiburi!

Kwenye kurasa zake za Mitandao ya Kijamii amerusha Video akiongea kuhusu Mgogoro wa Congo jana kwenye kikao chake na Wakuu wa EAC

Kamgombeza kama mtoto mdogo Rais wa Afrika Kusini kuhusu majeshi yake yanavyoisaidia Congo.

Kawananga SADC ambayo mwenyekiti wa Kamati yake ya Siasa na Usalama ni Rais Samia kuhusu support wanayoitoa kwa Congo.

Ameongea kama yeye ndo mwenye Congo na hakuna wa kumfanya lolote lile.

Aisee acha niendelee kummiss Jakaya Kikwete. Acha niendelee kuwamiss Majenerali bora kabisa wa JWTZ ( Mwamunyange, Shimbo, Mella na Mwakibolwa)

Kiburi cha Kagame kimefikia kiwango cha juu kabisa na kutokana na ujinga wa hawa viongozi wa Afrika tulionao sasa nina uhakika anaenda kuimega rasmi Congo.

Where is my JWTZ?

View attachment 3218616
Kesho atamtuhumu mkewe. Kijamaa hiki kimechanganyikiwa sina mfano. Sijui ndiyo mwanzo wa mwisho wake au mwisho wa mwanzo wake.
 
USAHIHI wa Kagame uko sehemu gani?
Kwanza si lweli kwamba hao wakimbizi aliowasema wapo. Hakuna wakimbizi wa DRC waliopo Rwanda...hiyo imekuwa officially established.
Kagame kuvamia kwake Congo na kuteka maeneo na kufanya eneo zima lisiwe na amani na utulivu...,ndo anakuwa sahihi?
utulivu wa mashariki ya Congo na watu kufanya shughuli zao kiuchumi kuna uhusiano wa moja kwa moja na maslahi ya Tanzania. Pata picha moja tu rahisi..,..japo Congo kuna utajiri wa miti mingi kuliko Tanzania,lakini wakazi wa mashariki ya Congo ndo wanunuzi wakubwa wa mkaa Tanzania,...unafikiri hizo bidhaa nyingine amabzo kule hazizalishwi wanazinunua kwa kiasi gani huku kwetu?
Kwa kuwa kuzingatia jiografia ya eneo na ukaribu na miundo mbinu ya kuifikia Dar port..kwa vyovyote wakazi wa mashariki ya Congo wanaitegemea Tanzania kama export getaway. Utasemaje hatunufaiki na DRC?
Hili suala umelivamia kama mabishano ya Simba na yanga.

Ili uwe katika position ku argue rudi kasome literature review ya huo mgogoro ulianzaje hadi hapo ulipofikia ndipo unchangie.

Mgogioro ulianza wakati wa Mobutu.

Marehemu Kabila alisaidiwa na Rwanda kumtoa Mobutu mbona hulaumu au ilikuwa haki Rwanda kusaidia Kabila lakini sio haki kusaidia Banyamulenge.
Somalia kuna mgogoro muda mrefu je Tanzania hauathiriki nao? Mbona husemi tukapigane huko? Mgogoro wa Ukraine na Russia Tanzania hatuathiriki mbona hudai Tanzania ijiingize huko.

Eti unajisifu tunauza mkaa Congo hivi hii ni sifa kuaccelerate jangwa Tanzania? Kwamza ilipaswa biashara ya export ya mkaa ipigwe marufuku ili kulinda misitu.

Rwanda ana athari kubwa na huu mgogoro kuliko nchi yeyote kwanza wakimbizi watakimbilia kwake, pili wale waasi wa intraramwe watatumia fursa hii kushambulia Rwanda.

Tatu Banyamulenge wana asili ya Rwanda hivyo hawezi kukaa kimya wanaponyanyaswa kama vile Russia haikukaa kimya wale waukraine wenye asili ya Russia huko Donbass walivyonyanyaswa na Ukraine au waarabu ambao hawakai kimya kwa sababu wanaona wapalestina wananyanyaswa. Hii ni kawaida. Au Uganda na Ethiooia walivyowasaidia SPLA ya Sudani Kusini kupigana na waarabu wa kaskazini hadi wakashinda. Au sisi tulivyoqasaidia waafrika wenzetu wa MsumbijizimbBwabwe,, Namibia kwa sababu tu ni waafrika wenzetu.

Wewe unajua kuwa Congo wana bandari au unadhani kika mzigo wa Congo unapita Dar? Hujui kuna Mombasa mizigo mingi tu inapita huko au kuna reli ya Lobito ambayo USA aneweka heavy investment na ndiyo itakuwa tegemeo kubwa la Congkuliko bandari ya Dar.

Unajua ahtari za nchi kupigana wewe? Pengine wakati wa Amiin ulikuwa hujazaliwa. Athari za vita ya Uganda hadi mwaka 2000 tulikuwa bado tunaifeel.
 
Kagame kweli kajaa kiburi!

Kwenye kurasa zake za Mitandao ya Kijamii amerusha Video akiongea kuhusu Mgogoro wa Congo jana kwenye kikao chake na Wakuu wa EAC

Kamgombeza kama mtoto mdogo Rais wa Afrika Kusini kuhusu majeshi yake yanavyoisaidia Congo.

Kawananga SADC ambayo mwenyekiti wa Kamati yake ya Siasa na Usalama ni Rais Samia kuhusu support wanayoitoa kwa Congo.

Ameongea kama yeye ndo mwenye Congo na hakuna wa kumfanya lolote lile.

Aisee acha niendelee kummiss Jakaya Kikwete. Acha niendelee kuwamiss Majenerali bora kabisa wa JWTZ ( Mwamunyange, Shimbo, Mella na Mwakibolwa)

Kiburi cha Kagame kimefikia kiwango cha juu kabisa na kutokana na ujinga wa hawa viongozi wa Afrika tulionao sasa nina uhakika anaenda kuimega rasmi Congo.

Where is my JWTZ?

View attachment 3218616

Tatizo la hii issue, ipande wa SADC M23 wanawawachukulia kama ni kikundi cha Kigaidi wakati huku EAC kuna nchi zinawaunga mkono M23. Huu mgogoro badala ya kushughulikiwa na SADC ni bora ushughulikiwe na EAC. Kitendo cha DRC kukacha mikutano ya EAC na kukimbilia SADC tayari inaonyesha ni jinsi gani DRC wanataka kuushughulikia huu mgogoro.

Nimemuelewa Ksgame, M23 ni Watsusi wa DRC siyo Rwanda.
 
Hii dunia inahitaji watu wababe wababe kama Kagame ili maisha yaende.

Kagame bila ubabe na umwamba Rwanda ingekuwa kama DRC tu, PK amewafanya Tutsi na wanyarwanda kuwa proud na utaifa wao popote pale.
 
Tatizo la hii issue, ipande wa SADC M23 wanawawachukulia kama ni kikundi cha Kigaidi wakati huku EAC kuna nchi zinawaunga mkono M23. Huu mgogoro badala ya kushughulikiwa na SADC ni bora ushughulikiwe na EAC. Kitendo cha DRC kukacha mikutano ya EAC na kukimbilia SADC tayari inaonyesha ni jinsi gani DRC wanataka kuushughulikia huu mgogoro.

Nimemuelewa Ksgame, M23 ni Watsusi wa DRC siyo Rwanda.
Endeleeni tu kujaa kwenye propaganda za Kagame.

Jua tu Mgogoro huu ukisuluhishwa na EAC ambayo ina nchi 2 zinazotaka kuimega Congo ( Uganda na Rwanda) kesho DRC itakuwa imemegwa.

Hakuna lugha ambayo KAGAME na MUSEVENI wanaweza kuielewa zaidi ya kichapo.

Na wakimaliza CONGO jua kituo kinachofuata ni KAGERA TZ
 
Hili suala umelivamia kama mabishano ya Simba na yanga.

Ili uwe katika position ku argue rudi kasome literature review ya huo mgogoro ulianzaje hadi hapo ulipofikia ndipo unchangie.

Mgogioro ulianza wakati wa Mobutu.

Marehemu Kabila alisaidiwa na Rwanda kumtoa Mobutu mbona hulaumu au ilikuwa haki Rwanda kusaidia Kabila lakini sio haki kusaidia Banyamulenge.
Somalia kuna mgogoro muda mrefu je Tanzania hauathiriki nao? Mbona husemi tukapigane huko? Mgogoro wa Ukraine na Russia Tanzania hatuathiriki mbona hudai Tanzania ijiingize huko.

Eti unajisifu tunauza mkaa Congo hivi hii ni sifa kuaccelerate jangwa Tanzania? Kwamza ilipaswa biashara ya export ya mkaa ipigwe marufuku ili kulinda misitu.

Rwanda ana athari kubwa na huu mgogoro kuliko nchi yeyote kwanza wakimbizi watakimbilia kwake, pili wale waasi wa intraramwe watatumia fursa hii kushambulia Rwanda.

Tatu Banyamulenge wana asili ya Rwanda hivyo hawezi kukaa kimya wanaponyanyaswa kama vile Russia haikukaa kimya wale waukraine wenye asili ya Russia huko Donbass walivyonyanyaswa na Ukraine au waarabu ambao hawakai kimya kwa sababu wanaona wapalestina wananyanyaswa. Hii ni kawaida. Au Uganda na Ethiooia walivyowasaidia SPLA ya Sudani Kusini kupigana na waarabu wa kaskazini hadi wakashinda. Au sisi tulivyoqasaidia waafrika wenzetu wa MsumbijizimbBwabwe,, Namibia kwa sababu tu ni waafrika wenzetu.

Wewe unajua kuwa Congo wana bandari au unadhani kika mzigo wa Congo unapita Dar? Hujui kuna Mombasa mizigo mingi tu inapita huko au kuna reli ya Lobito ambayo USA aneweka heavy investment na ndiyo itakuwa tegemeo kubwa la Congkuliko bandari ya Dar.

Unajua ahtari za nchi kupigana wewe? Pengine wakati wa Amiin ulikuwa hujazaliwa. Athari za vita ya Uganda hadi mwaka 2000 tulikuwa bado tunaifeel.
Nimekupa mfano tu....,kama Congo wananunua vitu minor kama mkaa..,utawauzia vitu vingapi vikubwa unavyozalisha? Kusipokuwa na wananunuaje?
Umesema kwa nini hatuingili mgogoro wa Somalia....ni jambo lisilo na uwiano na maelezo yangu kuhusu DRC....kwa sababu nilisema upande wa mashariki ya Congo ,kutokana na kijiografia watatarajiwa kuitumia zaidi Dar port kwa export jambo ambalo linainufaisha Tanzania. Somalia siyo land locked,wana bandari..na position yao kijiografia haiitegemei Tanzania..kwa hiyo hatuwezi kunufaika directly na Somalia...,kwa hiyo kwa nini tuhusike Somalia. Lakini Mashariki ya Congo ikiwa na misukosuko, Tanzania inaathirika moja kwa moja kiuchumi na kibiashara.
Umesema nikasome historia ya huo mgogoro....na kwamba rais Kabila na aliingia mikataba na Rwanda. Sijui unamaanisha nini kuhusu hilo....au una maanisha misemo ya vichochoroni inayodai kwamba Kabila alikubaliana na Rwanda kwamba endapo Rwanda itamsaidia kumuondoa Mobutu madarakani,malipo kwa Rwanda iwe ni kumegewa Kivu kaskazini?
Hayo ni maneno ya vichochoroni kwa sababu hata huyo Kagame hajawahi kudai hilo popote na kamwe hawezi kudai.
Madai ya Rwanda na Uganda yalikuwa kuna waasi wamefanya makazi ndani ya Congo lakini wana malengo ya kuzipiga nchi zao. Wote Uganda na Rwanda wakaingia na kuweka kambi ndani ya Congo na kujihusisha na uchimbaji wa madini. Uganda kaondoa majeshi miaka michache tu nyuma baada ya kitisho cha kushtakiwa kimataifa. Lakini wote Uganda na Rwanda wakatumia ujanja wa kutengeneza waasi wa kuchonga M23 ili wafanye yale yale kwa niaba yao.
 
Tatizo la hii issue, ipande wa SADC M23 wanawawachukulia kama ni kikundi cha Kigaidi wakati huku EAC kuna nchi zinawaunga mkono M23. Huu mgogoro badala ya kushughulikiwa na SADC ni bora ushughulikiwe na EAC. Kitendo cha DRC kukacha mikutano ya EAC na kukimbilia SADC tayari inaonyesha ni jinsi gani DRC wanataka kuushughulikia huu mgogoro.

Nimemuelewa Ksgame, M23 ni Watsusi wa DRC siyo Rwanda.
Hao watusi wametoka wapi toka lini Congo ikawa na watusi wengi hivyo aseme ukweli..anataka kupokonya ardhi ya congo.
 
Nimekupa mfano tu....,kama Congo wananunua vitu minor kama mkaa..,utawauzia vitu vingapi vikubwa unavyozalisha? Kusipokuwa na wananunuaje?
Umesema kwa nini hatuingili mgogoro wa Somalia....ni jambo lisilo na uwiano na maelezo yangu kuhusu DRC....kwa sababu nilisema upande wa mashariki ya Congo ,kutokana na kijiografia watatarajiwa kuitumia zaidi Dar port kwa export jambo ambalo linainufaisha Tanzania. Somalia siyo land locked,wana bandari..na position yao kijiografia haiitegemei Tanzania..kwa hiyo hatuwezi kunufaika directly na Somalia...,kwa hiyo kwa nini tuhusike Somalia. Lakini Mashariki ya Congo ikiwa na misukosuko, Tanzania inaathirika moja kwa moja kiuchumi na kibiashara.
Umesema nikasome historia ya huo mgogoro....na kwamba rais Kabila na aliingia mikataba na Rwanda. Sijui unamaanisha nini kuhusu hilo....au una maanisha misemo ya vichochoroni inayodai kwamba Kabila alikubaliana na Rwanda kwamba endapo Rwanda itamsaidia kumuondoa Mobutu madarakani,malipo kwa Rwanda iwe ni kumegewa Kivu kaskazini?
Hayo ni maneno ya vichochoroni kwa sababu hata huyo Kagame hajawahi kudai hilo popote na kamwe hawezi kudai.
Madai ya Rwanda na Uganda yalikuwa kuna waasi wamefanya makazi ndani ya Congo lakini wana malengo ya kuzipiga nchi zao. Wote Uganda na Rwanda wakaingia na kuweka kambi ndani ya Congo na kujihusisha na uchimbaji wa madini. Uganda kaondoa majeshi miaka michache tu nyuma baada ya kitisho cha kushtakiwa kimataifa. Lakini wote Uganda na R3wanda wakatumia ujanja wa kutengeneza waasi wa kuchonga M23 ili wafanye yale yale kwa niaba yao.
Hamna hoja hapa.

Historia ya Congo haianziijkwa Kabila ndio maana nilikujibumwanzo kasome vizuri historia ya Congo.

Biashara na Congo yeyote atakayetawala mashariki kama kutakuwa na ulazima wa biashara ataifanya tu na Tanzania siyo kazima awe Tshisejedi.

Ciongo kwa jiografia yake haitegemei kabisa bandari ya Dsn pekee, kuna bandari ya Angola ikisapotowa na reli ya Lobito wana bandari kule Atlantic ( matadi) **** bandari ya Mombasa.

Unasema somalia haituhusu na haina athari , hawa magaidi wa kiislanu waliosumbua Kilwa na kule kusini na pia upande wax¹ msumbiji wana mahusiano na Alshabaab na wanasaidiwa mafunzo na silaha, je hiyo siyo athari?

Vita ya Uganda wewe uliishuhudia na madhara yake unayajua au ulikuwa haujazaliwa.

Kama unamshabikia Tshisekedi wewe binafsi funga safari uende ukajiunge na wapiganaji wa huko kama Maimai ambao wanapambana na M23.,

Hakuna justification ya Tanzania kuingia vitani mashariki ya Congo.

Serikali iwaondoe askari wa Tanzania wanaolinda amani Congo.
 
Historia ya Congo haianziijkwa Kabila ndio maana nilikujibumwanzo kasome vizuri historia ya Congo.
Historia nchi zote za Afrika naijua vema siyo Congo tu. Lakini hapa hapa mjadala ni kuhusu Rwanda na Uganda kuongiza majeshi yao katika nchi ya Congo na kuvuna madini kwa kisingizio cha kulinda mipaka yao. Sasa sijui ni historia ya gani kuhusu hilo eneo uliyoisoma endapo hili dogo tu hujui. Mwanzo, Rwanda na Uganda walisema wameingiza majeshi yao Congo ili kujilinda. Sasa unajilinda kwa kuweka kambi ndani ya nchi ya watu?
Sasa hivi Rwanda amegeuza habari..anasema anaingiza kikosi kulinda watusi raia wa Congo.
Sasa kazi ya kulinda raia wa Congo wenye asili ya kitusi.
Muda huu vikosi vya Rwanda viko Rubaya toka mwaka jana wanachimba coltan. Ya nini ukasome historia ya zamani uruke hii ya sasa kuna jeshi la Rwanda linalopora na kuua raia Kivu?
Ciongo kwa jiografia yake haitegemei kabisa bandari ya Dsn pekee, kuna bandari ya Angola ikisapotowa na reli ya Lobito wana bandari kule Atlantic ( matadi) **** bandari ya Mombasa.
Acha ujinga na kuleta ubishi usio na kichwa wala miguu. Kuna vitu unatakiwa kuvisoma na kujifunza ..siyo kubisha wakati huelewi.
Nilisema Kijiografia ,eneo la Mashariki ya Congo wataitegemea Dar port zaidi kama export gateawy .
Umeongelea habari ya Congo kutumia Angola kama export point. Watu wanaoweza kutumia njia hiyo ni watu majimbo ya kusini ya Congo hasa kwa miji ya Kolwezi na Lubumbashi..kwa vile luna reli toka Kolwezi kwenda Lobito,Angola.
Lakini watu wa mashariki ya Congo....miji ya Goma,Bukavu na Kindu wanaitumiaje Angola wakati umbali kutika Goma hadi Lobito ,Angloa ni umbali wa zaidi ya km 3000....na achlia mbali moundo ya kubahatisha. Kwa nini wasitumie Dar port umbali mfupi kabisa na miundo mbinu ya uhakika?
Unajua maana ya eneo kuwa na advantage kijiografia au unaongea tu alimradi umejibu hata kama huna hoja?
Kwa taarifa yako tu..hata Congo wenyewe bahari imegusa katika nchi yao na wana bandari eneo la Matadi. Lakini bado eneo la mashariki watatumia kirahisi Dar port.
 
Biashara na Congo yeyote atakayetawala mashariki kama kutakuwa na ulazima wa biashara ataifanya tu na Tanzania siyo kazima awe Tshisejedi.
Uwezo wako mdogo sana kuchanganua masuala ya kiuchumi....ndo maana unabisha kijinga. Hakuna sehemu niliyoandika kumtetea Tsishikedi as a person. Nimeizungumzia Congo na hali yake kisiasa eneo la mashariki na uhusiano wake moja kwa moja na Tanzania kibiashara na kiuchumi.
Hapo juu umeandika.....,'"Tanzania itafanya biashara Kama kutauwa na ulazima". Ulichokiandika hapo kimeonesha hujui maana na umuhimu wa biashara kimataifa katika kukuza uchumi....kwa sababu sababu kwa nchi kufanya inter trading siyo suala la uchaguzi...kwamba mkipenda mnaweza kuacha tu. Inter trading ni jambo la lazima. Hilo nalo huelewi?
 
Mkuu Lord Denning , matamshi ya Kagame yamekuja kutokana na kauli ya rais Ramaphosa aliyoitoa siku chache nyuma wakati akitoa taarifa na kuomboleza vifo vya askari 13 wa South Africa waliouawa na M23, DRC. Ramaphosa alisema wameuawa katika shambulio lililofanywa na M23 na jeshi la Rwanda.
Na Kagame katumia kuteleza kwa Ramaphosa kidiplomasia kwa kuitaja Rwanda kuhusika na hilo shambulizi kama kivuli cha kuficha uhalifu wake halisi wa kuwafundisha,kuwapa silaha na kupigana moja kwa moja kijeshi na M23.
Kwa kutumia hicho kivuli akapindisha ukweli kwamba majeshi ya SADC yaliiyopo Congo yanasaidia jeshi la serikali,japo anajua ukweli kwamba hilo jeshi lipo pale kulinda amani tu kama lilivyokuwa jeshi la UN......Na ndo maana askari wa hilo jeshi wanauawa kwa kuviziwa wakiwa katika relaxed mode, na siyo katika combat action.
Ndo maana nasisitiza kama nilivyosema jana kwamba kulisaidia jeshi la Congo kimya kimya kwa mlango wa nyuma ni njia bora zaidi kwa vile inamnyima Kagame na washirika wake nafasi ya kupindisha maneno.
Uhuni wa Kagame wa uvamizi wa Goma ni strategy yake kuilazimisha DRC iingie katika meza ya mazungumzo kwa terms za Rwanda.
Imekuwa jambo bora DRC imetangaza kujitoa katika mazungumzo....na kwa vyovyote kwa ushauri wa wanaotoa backing nyuma ya pazia.
Ni suala la muda tu....when the screws are tightened hard enough on the battle ground...,that tall and lean statesman will surely feel the heat and ....will utter a different rhetoric.
Isitoshe, Kagame naye alipotea kidilomasia katika hotuba yake fupi ya malalamiko. Aliji implicate katika kile anachotumiwa kwa muda mrefu. Alisema anashangaa nchi zote zimefumbia macho raia wa Congo wenye asili ya kitusi wanavyoteswa kwa muda mrefu ndani ya DRC kiasi wengi wao kuwa wakimbizi ndani ya Rwanda. Akasema, .."hao watusi wakinyanyaswa na kushambuliwa na jeshi la Congo ,nchi zote zinakaa kimya... lakini M23 ambao wakiwatetea hao wanaonyanyaswa ,kila mtu anawashutumu.... hii haikubalik ...lazima jambo lifanyikei".
Kwa kauli yake hiyo inayoonesha yuko sympathetic na M23, amejikamatisha mwenyewe.

Ulikua makini Sana kufatilia Kila Neno katika matamshi yake
 
Endeleeni tu kujaa kwenye propaganda za Kagame.

Jua tu Mgogoro huu ukisuluhishwa na EAC ambayo ina nchi 2 zinazotaka kuimega Congo ( Uganda na Rwanda) kesho DRC itakuwa imemegwa.

Hakuna lugha ambayo KAGAME na MUSEVENI wanaweza kuielewa zaidi ya kichapo.

Na wakimaliza CONGO jua kituo kinachofuata ni KAGERA TZ
Una uoga mno na Rwanda, ambayo si chochote. Hiyo hofu yako kwa Rwanda huenda pia Ina chuki kwao ndio maana unategeneza narratives za kila aina, Mara JWTZ waende kupogana, mara hivi

Ondoka kwenye hayo mawazo utakua huru
 
Endeleeni tu kujaa kwenye propaganda za Kagame.

Jua tu Mgogoro huu ukisuluhishwa na EAC ambayo ina nchi 2 zinazotaka kuimega Congo ( Uganda na Rwanda) kesho DRC itakuwa imemegwa.

Hakuna lugha ambayo KAGAME na MUSEVENI wanaweza kuielewa zaidi ya kichapo.

Na wakimaliza CONGO jua kituo kinachofuata ni KAGERA TZ
Nakubaliana na wewe kagera ipo katika ramani zao
 
Back
Top Bottom