Ifike muda kama Bangi / Bange mnazovuta huwa zinawadhuru ( hasa Ubongo ) ni bora mziache tu.
Pia ifike muda kama unajijua kabisa umesahau Kunywa Dawa zako za Uwendawazimu kabla ya kuja ( Log In ) hapa JamiiForums basi uwe unazinywa Kwanza.
Na pia ni vyema kama unajijua umezaliwa na Kipaji cha Upumbavu na Masuala ya Kiitifaki ( hasa kwa Marais ) huyajui basi uwe unauliza uelimishwe.
Ni kweli Rais Kagame hakuja Msibani kwa Hayati Rais Dkt. Magufuli ila katika Siku ya Kuagwa Kitaifa pale Mkoani Dodoma aliwakilishwa na Waziri Mkuu wa Rwanda ( kama sijakosea ) pamoja na Balozi wao hapa Tanzania ambaye kwa taarifa yako tu ni kwamba Balozi huyu wa Rwanda alienda Mikoa yote ambayo Mwili ulipelekwa Kuagwa.
Siku ya Mazishi pale Chato Kiitifaki Rwanda na Rais Kagame aliwakilishwa vyema na Balozi ambaye alitoa Salamu mbele ya Hadhira kwa Niaba ya Wanyarwanda na Serikali yao.
Taratibu za Kiitifaki za Viongozi huwa hazijalishi kama Viongozi ni Marafiki ( Maswahiba ) au hapana bali hujumuisha mambo mengi na Kubwa ni la Usalama na 'Current Situation' ya nchi au hata Ratiba za Rais kwani Kifo kwa Binadamu huwa akina Ahadi ( Ratiba ) ila Ratiba za Kiutendaji za Marais huwa zinakiwa 'fixed' na hutenguliwa kwa dharula ya maana iliyo karibu na siyo ya mbali.
Na ulivyo 'very Foolish indeed' leo hii unahoji ni kwanimi Rais Kagame ambaye alikuwa ni 'Swahiba' wa Hayati Rais Dkt. Magufuli hakuja Msibani halafu hujahoji wala Kushangaa ni kwanini Hayati Rais wa Afrika Kusini Nelson Madiba Mandela aliyekuwa 'Rafiki' wa karibu wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere nae hakuja Msibani Tanzania.
Mbona hata Rais wa Uganda Mzee Yoweri Kaguta Museveni nae ni Rafiki mkubwa wa Tanzania na hata kwa Hayati Rais Dkt. Magufuli hakuja Msibani wala hujahoji ila 'Utahaira' wako umekutuma tu uhoji la Rais Paul Kagame wa Rwanda?
Hivi baadhi ya Watanzania Wapumbavu ( Mipopoma ) ni nani aliyewajazeni 'Utahaira' wenu huu na Kuwapandikizeni 'Chuki' dhidi ya Rwanda kama nchi, Wanyarwanda kama Raia na Kagame kama Rais?
Mlianza Kuzusha na Kuaminisha Watu kuwa Kikosi cha Ulinzi cha Rais wa Tanzania ( PSU ) kimechukua Walinzi kutoka nchini Rwanda kwa Kagame. Hivi kwa Mtu aliyeiva na anayejua vyema masuala mazima ya Kijasusi ( Intelligence ) hili linawezekana? Ndiyo kuna muda huwa nawadharau sana baadhi ya Watanzania ( ila siyo Wote ) kwakuwa hamna Akili na mmekalia tu Majungu, Umbea na Chuki.
Yaani kuna Mpumbavu Mwenzenu Mmoja ( sasa Mstaafu ) kwa Chuki zake tu binafsi na Uchapakazi na Ujasiri wa Rais Kagame kwa Kuiletea Maendeleo makubwa na ya haraka Rwanda Yeye alichokifanya ni Kueneza 'Propaganda' ya 'Chuki' kwa Wanyarwanda ( hasa Watutsi ) huku akiwahonga Wahariri wa Habari wa Tanzania waje na 'Agenda Setting Theory' ya Kuisema vibaya Rwanda ili Watanzania baadhi wasiojua 'Kufikiri' waamini.
Baadhi ya Watanzania kuzidi Kuichukia na Kuiandama Rwanda, Wanyarwanda na Rais Paul Kagame ni Kujitafutia tu Dhambi za lazima kwa Mwenyezi Mungu kwani Wanyarwanda kupitia Rais wao wameamua kusahau yaliyopita na Kuijenga vyema nchi yao, Kuchapa Kazi, Kujijenga Kimshikamano, Kupambana na Kudumisha Uzalendo wa Kweli huku wakiachana na Mambo ya Kipuuzi ambayo yangewachelewesha Kufikia Maendeleo makubwa ambayo leo hii wanayo japo waliuwana katika Machafuko ya Halaiki ( Genocide ) ya mwaka 1994 ukiachilia ile ya Kwanza ya 1959.
Dhambi ya Kuichukia Rwanda itawauwa.