Kagame kawachana Marais wanafiki wa Afrika, hacheki na wowote

Kagame kawachana Marais wanafiki wa Afrika, hacheki na wowote

Kubwa jinga kabisa...
Wao ni kulia tu kila siku, nchi ina wananchi milioni zaidi ya 100, bad wanalia kila siku...
Hii dunia ilipofikia si kama miaka ya 1970s, hivi sasa hakuna mtu wa kukupambania, hii ni dunia ya ubinafsi..
Trump huyo hapo kasema hatoi pesa kununua dawa za ARV...
Gaza imechakazwa dunia inatizama, wananchi 50000 wanauawa.. hakuna wa kukusaidia kama hujisaidii wewe kwanza..

Vijana wa DRC waamke, wapambanie nchi yao...
 
Mgogiro wa DRC ni mradi tata - money making scam kwa 'watabe' wa dunia.
Mi naamini hizi ni excuse, Hamas pale Gaza wamekaza na hawajaondoka wamekomaa pale hadi Israel kanyoosha mikono.
Israel ina teknolojia kubwa sana kijeshi na bado wakapewa bajeti na wakubwa kupambana na Hamas lakini wameshindwa kuwafuta Hamas.
Ukiamua kujipambania, hakuna kinachoshindikana, hata Mungu atajidhihirisha hapo as long as unapigania haki yako.
 
Vita siyo lelemama broo.

Mwezi February 2022 Putin alituma ule msafara wa 60km (wanajeshi wakiwa na vifaru, mizinga, makombora, nk) kwenda kuteka Kiev, ni miaka 3 sasa Kiev haijawahi kutekwa!

Na ukubwa wa eneo la nchi ya Russia ni mara 17 ya Ukraine
Russia inapambana na kuivunja Ukraine nguvu za kijeshi.
DRC inapambana kuiondoa M23 ndani ya ardhi yake na bado M23 wanazidi kuimega DRC zaidi.

Angalia huo utofauti, najua vita ni ngumu....

Russia inavamia, DRC inavamiwa, kuvamia ni vita ngumu zaidi kuliko kuvamiwa, lakini bado Russia imechukua sehemu kubwa Ukraine.
Plus NATO anatoa kila aina ya msaada kwa Ukraine lakini haijasaidia kuwatoa Russia Ukraine, pia Russia haina lengo kuiteka UKraine.

DRC wanatia aibu kuvamiwa na kuchukuliwa maeneo...
 
Unazani Rwanda yupo peke yake?Wanao mpa kiburi ni EU na US,sababu ya zile Cobalt na Coltan. Hebu msikilize huyu mbunge wa Ubeligiji.

View: https://m.youtube.com/watch?v=ajQhHy6U830&pp=ygUfV2hlbiB3b21hbiBiZWcgbWFuIHRvIG1hcnJ5IGhlcg%3D%3D

Wewe unazani wale Mercenaries wa juzi wapo DRC kwa maslahi ya nani?

Halafu wale Mercenaries juzi wamjisalimisha kwa M23 na kuruhusiwa kupitia nchi ya Rwanda kurudi makwao. Hivi ushajiuliza M23 wana huruma ya kiasi gani ya kuwachia wale Mercenaries bila kuwagusa.

EU na US wanajua wanacho kifanya DRC na Kagame wanamtumia kulinda maslahi yao na kuficha maovu yao.

Hauwezi kuwakamata Wazungu na kuwadhuru, ile kuwaachia ni kawaida vinginevyo Wazungu watakushukia kama mwewe.
 
DR_Congo-Rwanda_bilateral_map.png

Ila Congo kuna shida gani? hivi ki Rwanda kilivyo kidogo inakuwaje kinawapelekesha kiasi hiko?
Bro congo iliharibiwa na Mobutu,hakujenha jeshi imara,Bali jeshi la kumlinda yeye binafsi,aliwagawa wraia ili aweze kuwatawala kizuzu, na toka ameondolewa haijatulia kuweza kujenga jeshi lake.
Kwa udhaifu huo kagame anahakikisha haijijengi kijeshi na hata kiuchumi.
 
Price hiyo kupanda haina mahusiano ya demand na suppy? Ngoja wadadisi wa mambo watufungue zaidi
Sio kupanda price, ni kupanda export quantity, price fluctuation huwa ni asilimia 2 hadi 5, sio 100 to 200 %
 
Bro congo iliharibiwa na Mobutu,hakujenha jeshi imara,Bali jeshi la kumlinda yeye binafsi,aliwagawa wraia ili aweze kuwatawala kizuzu, na toka ameondolewa haijatulia kuweza kujenga jeshi lake.
Kwa udhaifu huo kagame anahakikisha haijijengi kijeshi na hata kiuchumi.
Ni sawa, lakini ndio imetokea watafanya nini?
Naamini kuna namna watafanya watoke walipo naamini ipo namna, tena wakiweka malengo miiaka 20 mingi.

Angalia nchi kama Iran, wana vikwazo toka 1970s hadi leo, lakini hawakukaa kulia, kulaumu na excuses nyingine, wamepambana na heshima imeonekana...

DRC ikiamua kwa dhati kutoka walipo wanatoka, itakuwa ngumu lakini wataweza tu...

Hii 2025 kuanza kulaumu uongozi wa Mobutu ni kama kurudi nyuma... walishavuka pale, waweke malengo, waweke nia na mipango ya siri...
Rwanda mid 1990s hapo walikuwa hawana jeshi lolote la maana, yakatoea mauaji ya kimbari, lakini wamefika hapo walipo.
 
Back
Top Bottom