Kagame kawachana Marais wanafiki wa Afrika, hacheki na wowote

Wewe muongo. Nenda kawaulize Hamas,Hizbullah, Iran na Assad yu wapi sasa. Hoiiiii..... Hujui kitu dogo.
 
Umemwambia mtu akuelezee anachozungumzia lakini? Maana umetoa tu maoni general. 😁
Muongo huyo Kagame. Anaposema eti M23 wametokea Uganda, mbona DRC hawailaumu Uganda. Kama amekiri kuwa waasi walioingia Rwanda ni kati ya 500 hadi 600 ndio ukweli amekubali wako kwake. Na yeye ndiye mfadhili. Apigwe ndani ya Kigali na yeye aone uchungu.
 
Ukishangaa ya Congo vs Rwanda hujayaona ya Russia vs Ukraine
Huo mfano ulio utoa hauendani na kinacho endelea Congo,maana Ukraine hajaishinda Urusi bali ni ana toa upinzani mkali tu kwa Urusi na penyewe ni kwasababu ana wasaidizi kibao nyuma yake ,na ndo maana mpaka sasa Urusi amemnyanganya robo nzima ya ardhi ya nchi yake.
 
Aangalie wasimchane
 
Ukweli mchungu, bila M23 kagame angekuwa ameshaondoka madaraka, maana waaasi wa kihutu wangekuwa wamejipanga, hivyo m23 ni kufanya wahutu wa 1994, wasipange....ila Ukweli ushauri wa Jk ni bora kuliko wote. Kagame anapaswa aongee na waasi wa kihutu . Na kongo itatulia...
 
Yuko wapi wa kumpiga?
Watu wazima wanaitana tena kwa dharura na kuishia kulaani, si bora wangesubiri kikao chao cha kawaida wakalaani vizuri?
Mambo mengine yanaudhi kweli kweli.
 
Ushauri wangu hii vita itamalizwa kwa mazungumzo ya kusikilizana pande zote zinazohusika. Hapa namanisha M23 , serikali ya Kongo, serikali ya Rwanda na FDLR wote wakae mezani mambo ya msingi yawekwe wazi. Kagame akubali kuwasikiliza FDLR pia .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…