Kagame: Nipo tayari kuendelea kuongoza Rwanda kwa miaka 20 zaidi

Rais Kagame angeiongoza Tanzania kwa alivyo Mpenda Maendeleo na Mtu wa Mikakati na siyo Mtu wa kupenda Upuuzi, Uswahili na kupoteza muda hivi sasa ingefanana na Dubai.
 
Nimependa uliposema ni swala la kusubiri bahati tu! Kwa kifupi kutoka na maelezo yako kama ilivyotokea kwa Raisi Magufuli! Ilikuwa ni bahati tu mtu mwenye "maono " kama Magufuli akatokea! Je huoni ni hatari nchi kusubiri "bahati "tu kumpata kiongozi, Bali njia ya hakika ni taasisi imara na dira inayojulikana ambayo taifa limekubaliana kuliongoza taifa.Angalia "maono" au "uzalendo" wa mtu Mmoja ulivyoondolea na kifo! Inabidi Tanzania kwa baadhi ya mtazamo wa wananchi inachukua mwelekeo tofauti! Mwanafalsa nakubali kabisa Demokrasia sio Coca-Cola, lakini lazima kuwe na mfumo wa aina fulani ambayo jamii kwa sehemu kubwa itawashirikisha wengi katika kuamua mustakabali wa maisha yao.Africa tuna nafasi nzuri ya kujifunza nini cha kuchukua au kuacha katika mfumo wa demokrasia ya Kimagharibi, na pia kujifunza kutoka nchi za Kikomunist au Kijamaa. Mbona China iliweza kufanya adjustment kubwa kwenye system yao baada kuona wazi kiuchumu hawatafiki mbali. Nachokubaliana na wewe utawala wa Kiimla unaweza kuikwamua jamii iliyokwama kwa muda tu! But in long,the oppressive elements inaanza tena to destroy ilichokuwa inakijenga! Kwa mtazamo wangu hata Magufuli asingweza kufika mbali! Tungerudi nyuma zaidi ya tulipokuwa. Namheshimu kwa sehemu! Hata kina Mao waliofanya mengi,kuna kipindi maono yao yalikoma! Maono ya Magufuli na modal yake isingefikisha taifa let mbali! Ingekwama tu,historia imeonyesha hivyo.
 
Aisee mnajua kurukia kichwa cha habari tu! jamaa alijibu hivo kuendana swali la wale watangazaji wazungu la kuachia madalaka,ikabidi amjibu hivo. aka mjibu nitaka nitaongeza myaka 20 Raia wakiamua sasa shida ikowapi?kuna mwingine wakutupangia nani awe Rais na nani asiwe Rais?.
 
Rais Kagame angeiongoza Tanzania kwa alivyo Mpenda Maendeleo na Mtu wa Mikakati na siyo Mtu wa kupenda Upuuzi, Uswahili na kupoteza muda hivi sasa ingefanana na Dubai.
Democracy ni msendeleo siyo kupishana ikulu . bira we unaelewa!
 
Udikteta sio ukomunisti na ukomunisti sio udikteta Lee Kuan Yew, Park Chung Hee , Franklin Delano Roosevelt, Donald Trump, Malkia Elizabeth hawa wote sio wakomunisti , Deng Xiaoping Ni mkomunisti lakini alitawala China kwa miaka 10 tu . Narudia tena kwa herufi kubwa UDIKTETA SIO UKOMUNISTI NA UKOMUNISTI SIO UDIKTETA.
 
Mbona Rwanda haijafanana hata na Dar es Salaam mpaka sasa??
Rais Kagame angeiongoza Tanzania kwa alivyo Mpenda Maendeleo na Mtu wa Mikakati na siyo Mtu wa kupenda Upuuzi, Uswahili na kupoteza muda hivi sasa ingefanana na Dubai.
 
Huyu anataka ya Sri Lanka Tu.......watu wake watakuja kumbandua sebuleni kwake na familia yake wewe mwache
 
Ukiona hivyo ujue anakaribia kufa.. Hizo huwa ni dalili za kifo... Akiishi sana ni miaka miwili toka sasa..!
Acha uchuro kwa wenye madaraka wewe, unajua anapambana na changamoto zipi katika huo Urais wake kuhakikisha ulinzi na usalama, uchumi wa nchi na hata maendeleo ya kesho kiujumla [emoji848][emoji57]
 
Ni hivi kwanza kwenye demokrasia za kweli Rais au waziri mkuu ambaye anaongoza vibaya hawezi kukaa hata zaidi ya miaka mitano madarakani achilia mbali hiyo kumi uliyoizoea na unayoizungumzia wewe.

Pia common sense tu itakuambia ni heri kuwa na mfumo ambao hauruhusu mtu yeyote kutawala zaidi ya miaka 10 bila kujali amefanya vizuri sana au vibaya sana.Mfumo wa utawala mfupi ni kwamba ikitokea mmepata bosheni kwa bahati mbaya(kama ilivyo kwa nchi nyingi za Africa) hamtakaa nalo miaka mingi likiwatesa na kuwafanya muishi kama mko jehanamu kwa miaka 20 au 30 au 40.
Naona hujasoma andiko langu lote. Tulia ulisome tena maana nimewaongelea viongozi kadhaa. Ishu sio kukaa madarakani. Ishu ni akili, utendaji, maono na uzalendo.
 
Mkiwa mmeshafanya mapinduzi ya kiuchumi sawa mnaweza kuwa na demokrasia ya uhuru mpana.

Lakini mkiwa wachanga kiuchumi demokrasia ya uhuru mpana ni mbaya. Ndo maana mtoto haachiwi uhuru. Yaani ukiwa unategemea misaada wewe ni kama mtoto, demokrasia ya uhuru mpana inaweza kukupoteza kirahisi sana.

Kupotea kwenyewe ni kukosa muendelezo, maana wakuu wa nchi wanakuwa wanachaguliwa kwa umaarufu wao na sio kwa ufanisi wao.
 
Kawaida ya madikteta wanavyozidi kukaa sana madarakani ndivyo wanazidi kuwa wanyama.

Madikteta hawataki kabisa mifumo au taasisi zinazofanya kazi ila wao ndio taasisi. Huyo Kagame bila ya kufanya mbinu za kumuangamiza, atawatawala huku akiwaminya marenge hadi kufa.
 
Paul Kagame akijitazama katika kioo chake anamuona LEE Kuan Yew Kasimama mbele yake!! Kagame Mtu wa fursa "Nothing is impossible".
 
Paul Kagame akijitazama katika kioo chake anamuona LEE Kuan Yew Kasimama mbele yake!! Kagame Mtu wa fursa "Nothing is impossible".
Hamna chochote anahofia aki retire anayekuja huenda akamuwajibisha yeye na biashara zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…