DENG XIAOPING
JF-Expert Member
- Mar 6, 2022
- 2,396
- 2,598
Xi Jinping kabla ya kuwa Rais 2013 amehudumu katika ngazi mbalimbali za chini za chama na serikali kwa muda wa zaidi ya miaka 40Swali zuri.
Hao uliowataja wa Afrika uko sahihi kuwa sio wazalendo. Ni watu ambao wamekosa maono zaidi ya kula bata. akina Nguema wapumbavu sana. Mtoto wa Nguema anapost Instgram kila siku maisha ya anasa anayoishi kwa mauzo ya mafuta ya nchi yake, mpaka wazungu wakakamata baadhi ya mali zake ili utajiri huo urudishwe nchini mwake.
Mifano mizuri ya waliokaa sana lakini walikuwa wazalendo ni Ghaddafi, Kagame na Nyerere. Naamini kwenye sekta ya maendeleo hakuna wa kumpinga kati ya hawa.
Mifano mingine mizuri ni kwenye nchi za Uarabuni zenye wafalme, maamiri na masultani. Kuna muendelezo mkubwa wa maono na mipango ya maendeleo japokuwa wafalme hao wanakula bata lakini kuna kushiba na khivyo kufanya maendeleo kama una uzalendo.
Kuhusu wazungu na wajapani kipindi wanatajirika walitajirika kwa ujambazi wa kutumia silaha. Wazungu walitoka Ulaya na kwenda kuiba ardhi na mali na watu duniani kote kwa mtutu wa bunduki.
Wajapani walifanya vivyo hivyo ukanda wa Asia Mashariki (China, Cambodia, n.k.)
Kipindi wanafanya hayo hawakuwa na demokrasia. Walikuwa na tawala za kidikteta wanazoita "Ufalme"
Marekani ni wazungu wa Ulaya Magharibi. Ni tawi lao na ndo dola kuu iliyoundwa na wazungu wa Ulaya Magharibi so far.
Kwa hiyo Marekani ni muendeleo wa kilichokuwa kinaendelea Ulaya. Suala la "Uhuru wa Marekani kutoka Uingereza" halina maana sana. Waliopata uhuru ni wazungu walewale wa Ulaya Magharibi wakiwa na utajiri ule ule wa Ulaya.
Na wao pia baada ya Uhuru walieendesha nchi kwa miaka mingi kama oligarchy. Yaani siasa ilikuwa mikononi mwa wachache ambao ni wanaume wazungu wanaomiliki ardhi.
Ni mfumo waliorithi kutoka Ulaya kwenye Unyarubanja wa Ulaya (mambo ya Landed Gentry ambao ndo walikuwa wabunge wa House of Lords yaani washirika wa Mfalme katika kuendesha nchi.) Ufalme wa Uingereza ulianzishwa kwa William The Conqueror kupita eneo hadi eneo akifanya mapatano na wamiliki wa ardhi wamuunge mkono kwa kuweka ardhi zao chini ya utawala wa mfalme mmoja. Waliokubali kwa hiyari ikawa poa, walioleta ubishi ikawa vita.
Mbinu ile ile aliyotumia Karl Peters katika kutengeneza himaya ya Deustche Ost Afrika (Tanganyika + Ruanda-Urundi).
Back to Marekani...
Kwa hiyo kwa kuwapa haki ya kupiga kura na kugombea wazungu wenye ardhi ni chini ya 30% tu ya Wamarekani ndo walikuwa wanaendesha nchi.
50% (wanawake wa kizungu tu) waliruhusiwa kupiga kura na kugombea mwaka 1920 wakati nchi ishaendelea tayari.
Weusi hawakuwa na haki za maana mpaka mwaka 1965 wakati nchi ishapiga hatua kubwa zaidi. Kwenye historia wanasema weusi walikuwa na haki toka 1870 lakini sote tunajua nini kilichokuwa kinaendelea. Ni wanaume wachache sana weuzi na kwenye majimbo machache ambao walikuwa wanamiliki ardhi ndo waliweza kufaidi haki hiyo.
Weusi wengi waliendelea kuteseka chini ya sheria za weusi (Black Codes) ambazo ziliwekwa baada ya vita ya wenyewe kwa wenyewe ya kukomesha utumwa wa weusi ili kuendelea kuwakandamiza kwa mujibu wa sheria.
Kwa hiyo utagundua kuwa Marekani demokrasia wanayoisifia sana sasa hivi wameianza juzi juzi tu baada ya kuwa wameshajenga nchi.
Kabla ya hapo walikuwa na qualified democracy. Yaani meritocracy kama wanayotumia China sasa hivi na ambayo inawasaidia sana kupiga hatua kubwa za kiuchumi.
Hata Singapore mapinduzi aliyofanya Lee Kuan Yew aliyafanya akiwa katika utawala wa kidikteta kama wa Nyerere. Hakutaka vyama vingi wakati huo alipokuwa anachukua maamuzi magumu ya kuiweka Singapore katika mstari.
Mfano Singapore haina ardhi. Ukubwa wa Singapore ni nusu ya ukubwa wa mkoa wa Dar es Salaam. Kwa hiyo mipango miji lilikuwa jambo la muhimu sana kulisimamia. Lee Kuan Yew alichoma moto makazi ya watu ambao hawakutaka kuhama kwa hiyari kwenye vijumba vyao ili kuachia maeneo serikali ijenge vizuri na kwa mpangilio.
Demokrasia ya Magharibi ni silaha ya wazungu
Wazungu wanaelewa madhara ya demokrasia kwa nchi ambayo bado haijasimama vizuri kiuchumi. Ndo maana wanailazimisha sana itumike kwenye makoloni yao yote ya zamani.
Demokrasia inatengeneza mwanya kwa mzungu (ambaye ukoloni haujatoka kwenye damu yake) kuwavuruga watu ili achukue rasilimali zao.
Libya alifanya hivyo. aliwarubuni wapinzani kuharibu nchi yao wenyewe.
Hata hapa Tanzania kama Mmarekani akipata ni anamuita Mbowe tu anamvimbisha kichwa na kumuomba alete vijana Marekani au nchi jirani kibaraka wa Marekani wanapigwa brashi ya kijeshi na wanapewa silaha na sapoti ya jeshi la Marekani kupindua serikali.
Unadhani Mbowe atakataa mpango kama huo?
Hiyo ndo faida ya demokrasia kwa mzungu.
Kwetu haina faida. Changamoto ni tupate kiongozi mwenye akili nzuri, mwenye ujasiri wa kusimamia maslahi ya Tanzania na maslahi ya Afrika.
Na muhimu zaidi awe ni kiongozi asiyenunulika au kutishika. Mtu yeyote mwenye mali au akaunti nje ya nchi hafai kuwa Rais au mteule wa Rais au kuwa katika serikali ya Tanzania. Ukishakuwa na mali kwenye nchi za Mzungu huna ujanja. Ni amekushika pumbu, ukimdindia anakamata mali zako.
India inasifiwa kuwa ni Biggest Democracy in the world kutokana na kufuata demokrasia ya Magharibi huku ikiwa na wananchi bilioni 1.3.
Lakini uchumi wa China ni mara 7 ya uchumi wa India. India na China wana population inayokaribiana, ila China ina ardhi kidogo inayofaa kwa kuishi (sehemu kubwa ni jangwa), lakini China imeipikua India kiuchumi.
China ni meritocracy. Wana qualified democrasy ndo maana wameweza kufanya mapinduzi makubwa ya kiuchumi kuliko India.
India vyama na kiongozi mkuu anabadilika na kuja ya yake kila baada ya muda fulani. China wana party supremacy na kura za wananchi wote zinapigwa kuchagua viongozi wa ngazi za chini kabisa. Kutoka hapo unapanda vyeo kwa utendaji wako na sio kwa popularity contest ya uchaguzi mkuu.
Tatizo kubwa la demokrasia ya magharibi ambayo sisi hata Tanzania tunaifuata ni kwamba:
1. Kigezo cha kuchagua kiongozi wa nchi ni uwe na miaka 18. Huu ni upuuzi mkubwa. Kuwa na miaka 18 sio kigezo cha kwamba unaelewa issues na unaweza ukafanya maamuzi ya kuchagua viongozi wakuu wa nchi, maamuzi ambayo yanaathiri hatma ya nchi.
2. Kigezo cha kuchaguliwa pia ni umri fulani na uwezo wa kusoma na kuandika tu. Huo nao ni upuuzi mkubwa.