Watu wanasema kama vile Magufuli anaweza kuwafunika wengine wengi wa CCM wanaotaka urais 2025.
Moja ya kanuni zinazoifanya CCM iendelee kuwepi madarakani ni "kula kwa kupokezana". Kuna wapiga debe wanapiga kwa kujua wanangoja zamu zao. Kuna wengine kina Pinda wanapiga debe kwa kujua washamaliza zamu zao.
Ukiindoq mfumi huo, CCM inakufa. Kwa sababu, CCM haina dira wala muelekeo katika itikadi. Imebaki kuangalua ulaji tu.
Sasa mtu anayewazibia wengine ulaji na kutaka kukaa yeye tu kwenye ulaji atawezaje kuwa rais kwa zaidi ya miaka 10?
CCM wamemuua Chinjachinja Dr. Omar Ali Juma, kwa kugombea urais, itakuwa Magufuli?
Kwa taarifa tu, Dr. Omar Ali Juma ndiye alikuwa chaguo la Mkapa kuwa rais baada yake. Hizi ni taarifa za kutoka ndani ya familia ya Mkapa nilipewa kipindi cha urais wa Mkapa. Huwa sitegemei vyombo vya habari, naenda kwa mtandao wa ndugu na marafiki ambao uko juu ya vyombo vya habari.
Watu wakamuomondoa Dr. Omar Ali Juma "Chinjachinja". Wakamchinja Chinjachinja.
Magufuli hajaweza kumaliza yaliyo ndani ya muda wa urais wake, washamzushia kuhusu yaliyo nje ya urais wake?
Oligarchy ya CCM inautazama urais kwa njaa kubwa. Itaruhusu vipi Magufuli ahodhi madaraka?
Magufuli is not that strong. Magufuli is not that smart. Watu wanaoogopa Magufuli ku violate term limits, wanaonesha weakness yao tu ya kuogopa kivuli cha mtu kabla hata mtu mwenyewe hajatokea.
Kumzushia mtu habari mbaya bila uhakika ni kitu kibaya sana.
Kuna mwaka nilikuwa nasoma Tambaza, Mwalimu mmoja alitaka kunizushia kesi ya uongo.
Nikamuwakia kama nataka kumpiga!
Nilimuwakia kwa Kiingereza ikawa kama nimesahau Kiswahili.
"You are wrongfully accusing me. You are falsely accusing me. What is the meaning of this provocation?".
Yani nilikuwa mbogo mpaka yule mwalimu, mwalimu mkali sana anaogopwa na wanafunzi wengi, ilibidi awe mpole kwangu.
Nguvu hizo nilizipata wapi?
Nilizipata kwa kuwa sikujali huyu Mwalimu mkali
Nilijali haki yangu ya kutoshutumiwa kwa uongo.
Shutuma ya uongo ni kitu kibaya sana.
Yani mtu muovu anaweza kufanya uovu mwingi, halafu, ukimpa shutuma ya uongo, anaweza kutumia shutuma ya uongo kujisafisha.
Inakuwa a case of crying wolf. Kelele zako za shituma za uongo, zinafanya shutuma nyingine zozote utakazotoa zionekane ni za uongo, hata kama ni za kweli.
Watu wanaojua trial law nawanajua hilo. This becomes a matter of credibility. Wanaomsema Magufuli, kwa kuanza kumhukumu kwa makosa atakayoyafanya mwaka 2025, wanaharibu credibility yao. Wanaonekana ni wapinzani wa kisiasa tu ambao Magufuli amewashinda mchezo wa chess katika siasa, sasa wanaamua kumchafua tu. Kitu ambacho si kweli. Hili linaumuza sana kwetu sisi ambao tunaona Magufuli ana matatizo mengi sana ya kweli ambayo kashayafanya, hayahitaji kupiga ramli za 2025.
Kumshutumu Magufuli kwa habari za speculations za 2025 ni kumfanyia favor.
Ni kuiambia dunia kwamba Magufuli hana makosa ya maana aliyoyatenda mpaka leo.
Kwamba hatuna cha kumshutumu na kumhukumu Magufuli ambacho amefanya mpaka leo.
Inatubidi tuanze kutunga makosa ambayo atayafanya mwaka 2025 ili kumhukumu.
Ni ujinga. Ni kukosa kufikiri kimantiki.
Kwa nini tumshutumu na kumhukumu Magufuli kwa makosa ambayo tunasema atayafanya mwaka 2025, wakati ana makosa mengi sana ambayo kashayafanya mpaka leo?
Tunawapa watetezi wake msemo tu, waseme " Wapinzani wa Magufuli hawana hoja. Wanapiga ramli kwamba Magufuli atafanya makosa mwaka 2025".
Sitaki kamwe kujiunga katika ujinga huu.
Sent using
Jamii Forums mobile app