Kagasheki awaasa kiaina Watanzania kuhusu kauli ya ukomo wa Urais kwa kutumia mfano Paul Kagame 2012

Kagasheki awaasa kiaina Watanzania kuhusu kauli ya ukomo wa Urais kwa kutumia mfano Paul Kagame 2012

Ni ujumbe unaoonekana wa kawaida kabisa kutoka kwa Dr Kagasheki. But timing yake inaufanya ujumbe huu ubebe uzito mkubwa sana.

Ni ujumbe kwa Watanzania kuwa tusiamini kila kitu kitokacho vinywani mwa wanasiasa.

"Tafakarini kwa makini Watanzania" that seems to be the bold message from this distinguished doplomat.

Bravo; CCM ina wachache wenye akili; wengi ni waimba mapambio.....kusifu na kuabudu....so sad.
 
Sasa mbona unafananisha vitu tofauti?

Hiyo molestation imeshafanyika, unataka kuifananisha na habari za 2025 ambazo hazijafanyika?

Swali langu ni dogo tu.

Inafaa kumhukumu mtu kwa makosa ambayo unafikiri atayafanya, lakini hajayafanya?
Of course, mtu anahukumiwa kwa 'record' yake; unataka ahukumiwe kwa kitu gani?

Kama mtu amejijengea rekodi ya kutoaminika kwa aliyokwishayafanya huko nyuma, unataka watu wamhukumu kwa yapi?
 
Wrongful accusation ni kitu kibaya sana.
Hakuna 'wrogful accusations', wakati mtu anajulikana kwa matendo na tabia zake za miaka yote ya nyuma. In fact it is not even a 'wrongful accusation', it's an experience/record on which someone is running on that will determine how s/he is perceived and judged.

Naona hapa hakuna jipya, ni kazi bure kurudiarudia yaleyale yaliyokwisha andikwa bila ya kutoa 'position' mpya.

When there is something new to discuss call me back.
 
Unamhukumu mtu leo kwa kosa atakalolifanya mwaka 2025?

Mwaka 2020 kuna uchaguzi pia, mmeshakubali Magufuli kashinda uchaguzi huo?
 
Kagasheki zama zake zilishapita ajitulize. Kila mtu ana Bahati yake. Wahenga walishasema Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi.

Sisi watanzania tunampenda kwa wingi Mkubwa, na tunasema katiba sio Vitabu vitakatifu.

Kupitia wawakilishi wetu ambao ni wabunge na ndio wenye dhamana ya kurekebisha vifungu kwa maslahi mapana ya Taifa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hao wabunge wanaopatikana kwa kubaka box la kura ndio wanaamua kwa maslahi mapana ya taifa? Hii kunajisi box la kura lengo lake hasa ni kupata bunge la makondoo wa ndio mzee ili kumuongezea muda wa kukaa madarakani, na ujue hata wao wakifanya hivyo wanajiwekea mazingira ya kuendelea na mlo. Ukishaona kiongozi anachezea box la kura, basi ujue mtu huyo ana uwezo mkubwa wa kujiongezea muda wa kukaa madarakani.
 
Hiyo movement huwa hawaifanyi wao directly. Yaani anahitaji watu watatu tu kuimuvuzisha hii kitu na bahati mbaya sana wote hao kila anapoenda, na wao humfuata nyuma as if Mihimili na Vyombo vyao ni tawi la Gogoni

Tuombe uzima ikifika 2025 turudi hapa kucomment. Naona wasiwasi ni mkubwa mno wakati ndani mambo hayapo kama yanavyoonekana!
 
A person is considered innocent until proven guilty.

Magufuli hatavunja katiba ili kuendelea kuwa rais.

Si kwa sababu anaipenda sana katiba. La hasha.

Magufuli ameshajua kwamba urais hauwezi. Ndiyo maana haishi kusema amechoka, kazi hii hakuitaka, muombeeni etc.

Huyu mtu angekuwa na uwezo wa kuacha urais bila aibu 2020 angeacha awe rais mstaafu.

Ni mtu ambaye maji yamemzidi kina. Ndiyo maana kika sikua anabwatuka maneno ambayo hayana staha za kirais.

Sasa mtu huyo ambaye kashachoka ndiye wa kuogooa kwamba atazidisha muda wake wa urais?

Kasema hatavunja katiba katika hili.

Mnataka afanye nini zaidi mkubali?

Kwa nini mnamhukumu kwa makisa ambayo hajayafanya bado, wakati ana makosa kibao ambayo kashayafanya?

You are losing focus.

You are not dealing with the real, you are dealing with the hypothetical.

Wewe tukikuhukumu kwa makosa tunayosema utayafanya mwaka 2025 utaona sawa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Duh..Mzee unaamini kweli Magufuli amechoka na hatamani kuwa Rais..? Eti 2020 angestaafu kama sio aibu?
Mwanzo niliona una hoja zenye mashiko kusema tusimhukumu kabla ya muda, ila hapa umekuwa naive sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unamhukumu mtu leo kwa kosa atakalolifanya mwaka 2025?

Mwaka 2020 kuna uchaguzi pia, mmeshakubali Magufuli kashinda uchaguzi huo?
Naona unapenda kuendeleza mjadala huu.

Kingekuwa kipimo kizuri sana na kilicho sahihi kwa jinsi anavyokubalika kwa wananchi, endapo uchaguzi huo ungefanyika kwa haki na uhuru kamili kwa wapiga kura kumchagua au kutomchagua.

Sasa hutaki hata hapa nigusie historia ya uchaguzi kutokuwa huru na wa haki kutokana na historia tuliyoishudia katika miaka hii mitano inayoelekea ukingoni.

Kutokana na historia hiyo, na uzoefu tuliopata hadi sasa, sijui ni kitu gani kitatuhakikishia kuwa uchaguzi 2020 utakuwa huru na wa haki!

Kwa hiyo atakaposhinda uchaguzi huo kwa njia alizozoea kuzitumia, bado utashangaa alivyoshinda?
 
Kama wewe unajulikana ni jambazi sugu, na mitaani unajulikana pasi shaka hiyo ndio sifa yako inayokupambanua; tutajuaje kuwa kati ya leo hadi hiyo 2025 utabadilika?

Nitakuwa naiweka familia yangu hatarini nisipokutolea gobole nikikuona unazongea mlangoni pangu.
Mkuu, ni kweli Magufuli kavunja katiba mara nyingi, lakini hili la kuongeza muda wa Urais zaidi ya 2025 lipo extreme kidogo, sio jepesi kama mengine aliyovunja, japo inawezekana, tumpe benefit of doubt.

Maana ataivuruga sana CCM akifanya hii move

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh..Mzee unaamini kweli Magufuli amechoka na hatamani kuwa Rais..? Eti 2020 angestaafu kama sio aibu?
Mwanzo niliona una hoja zenye mashiko kusema tusimhukumu kabla ya muda, ila hapa umekuwa naive sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Yani hata kama nimekosea kuona Magufuli amechoka, tuseme nimekosea hilo.

Tuseme mara zote Magufuli anaposema hakuitaka kazi (kaona maji marefu, kazi nzito (hakujiandaa), tumuombee (anahitaji divine intervention), anatamani angekuwa IGP (anatamani wengine wangekuwa juu yake wanampa amri badala ya yeye kuongoza nchi) etc, hajachoka.

Tuseme Magufuli ana uwezo sana wa kuwa rais, ndiye rais mwenye uwezo kuliko marais wote waliompita na ana tamaa sana ya kuendelea kuwa rais hata baada ya 2025.

Huko kote nakuruhusu wewe uwe sawa, mimi ndiye niwe nimekosea.

Baada ya yote hayo.

Hoja ya msingi zaidi ni kwamba, hatutakiwi kumhukumu mtu kwa kosa ambalo hajalifanya, na kakana kutaka kulifanya, tunasema atalifanya mwaka 2025.

Twende kwa facts, si kwa speculations.

Tukianza kwenda kwa speculations, yeyote anaweza kutunga lolote kuhusu yeyote mwingine na kumbambikia kesi.

Nitasema wewe unataka kuniibia mwaka 2025.Tukufunge.

Itakuwa sawa hiyo?
 
Binafsi naamini asilimia 99, Jiwe atabaki zaidi ya mihula miwili. Naweza kuwa nakosea, lakini kauli zake na za wana CCM wengine inaonyesha kabisa kuna jambo kubwa linaendelea nyuma ya pazia
 
Naona unapenda kuendeleza mjadala huu.

Kingekuwa kipimo kizuri sana na kilicho sahihi kwa jinsi anavyokubalika kwa wananchi, endapo uchaguzi huo ungefanyika kwa haki na uhuru kamili kwa wapiga kura kumchagua au kutomchagua.

Sasa hutaki hata hapa nigusie historia ya uchaguzi kutokuwa huru na wa haki kutokana na historia tuliyoishudia katika miaka hii mitano inayoelekea ukingoni.

Kutokana na historia hiyo, na uzoefu tuliopata hadi sasa, sijui ni kitu gani kitatuhakikishia kuwa uchaguzi 2020 utakuwa huru na wa haki!

Kwa hiyo atakaposhinda uchaguzi huo kwa njia alizozoea kuzitumia, bado utashangaa alivyoshinda?
Uchaguzi kutokuwa wa haki au huru Tanzania si kitu cha kuniambia wewe leo hii.

Mimi nakaa na wakuu wa usalama wa Tanzania wananieleza jinsi chaguzi zilivyopinduliwa tangu enzi ya chama kimoja, mfano Zanzibar uchaguzi wa Idris Abdul Wakil kuwa rais Zanzibar, Wakil hakupata kura za kutosha, ingawa uchaguzi ulikuwa wa "Ndiyo/ Hapana". Mtu kashindanishwa na kivuli, halafu akashindwa uchaguzi.

Matokeo yakafika mpaka vyombo vya habari vya serikali. Wakubwa wa Daily News waliyapata matokeo halisi. Idris Abdul Wakil kashindwa uchaguzi Zanzibar, wakaambiwa subirini msiyachapishe matokeo. Serikali ikafanya sarakasi, matokeo yakabadilishwa. Idris Abdul Wakil akawa rais.

Kwa aibu Mzee Wakil aligombea term moja tu, kisha hapo hakutaka kuwa rais tena.

Watu wengi wanapoongelea wizi wa kura, wanaongelea katika zama za vyama vingi tu, wizi huu una mizizi tangu enzi za chama kimoja.

Sasa hutaniambia jipya kuhusu wizi wa kura Tanzania, nimeanza kuzunguka corridors za Ikulu Tanzania tangu nikiwa tumboni mwa mama yangu. Tangu enzi za Mwalimu Nyerere na Mama Joan Wicken Ikulu.

Kura zinaibiwa, but that's not the point.

The point is, unafanya nini kubadili hilo?

Kulialia kwamba Magufuli ata violate term limits ndiyo kutasaidia kura zisiibiwe 2020?

Mimi nafikiri mngejipanga kuhakikisha kura haziibiwi 2020, mkapiga kampeni ya nguvu kuelimisha watu ubaya wa Magufuli, mkanadi sera zenu nzuri, pengine huyo Magufuli asingeweza hata kushinda uchaguzi hiyo 2020. Habari ya ku violate term limits 2025 iwe moot.

Moot. Unaelewa?

Kwa nini mnapoteza muda wenu kushabikia hypothetical problems kuhusu term limits 2025 wakati mna real problems za uchaguzi wa 2020?

Uchaguzi wa 2020 mmejipanga vipi kumuondoa Magufuli? Au mshakubali tu kwamba atawashinda by hooks and crooks?
 
Binafsi naamini asilimia 99, Jiwe atabaki zaidi ya mihula miwili. Naweza kuwa nakosea, lakini kauli zake na za wana CCM wengine inaonyesha kabisa kuna jambo kubwa linaendelea nyuma ya pazia

Kwa nini asilimia 99 na si 98, 97 au 49?

Kuwa specific, taja kauli gani, kaisema wapi, tuzichambue kwa kituo.

Ukisema kauli zake tu, watetezi wake watasema ameshasema hatavunja katiba, unataka aseme nini zaidi?
 
Mkimaliza naomba niwakumbushe yule ni Baloz Khamis... Yupo kazini kupima upepo kikubwa tufanye kazi hayo mambo mengine tutakuja kuwapa shida Familia zetu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uchaguzi kutokuwa wa haki au huru Tanzania si kitu cha kuniambia wewe leo hii.

Mimi nakaa na wakuu wa usalama wa Tanzania wananieleza jinsi chaguzi zilivyopinduliwa tangu enzi ya chama kimoja, mfano Zanzibar uchaguzi wa Idris Abdul Wakil kuwa rais Zanzibar, Wakil hakupata kura za kutosha, ingawa uchaguzi ulikuwa wa "Ndiyo/ Hapana". Mtu kashindanishwa na kivuli, halafu akashindwa uchaguzi.
Keep your focus. Hapa tunamzungumzia mtu 'specific', halafu unatoka na hao wengin?

Si hata afadhali ya hao wengine hawakuwa 'blatant' na baadhi ya mambo kama alivyo huyu! Kuna cha kulinganisha hapo kweli?
 
Tatizo unazungumzia mtu, mimi nazungumzia zaidi ya mtu.

Ni nchi gani zimeingia katika lindi la marais kung'ang'ania madaraka?

1. Ni nchi ambazo hazina utamaduni wa marais kupokezana madaraka kwa chaguzi.

2. Ni nchi zenye historia ya mapinduzi ya kijeshi.

3. Ni nchi zenye charismatic leaders na strong opposition.

4. Ni nchi ambazo viongozi na rais wanaogopa wakitoka madarakani wanaweza kufungwa kwa maovu waliyoyafanya.

5. Ni nchi ambazo rais akitoka madarakani anaweza kutaifishwa mali zake.

Tanzania hatufit katika hata moja kati ya hayo juu.

Magufuli kawapiga mpaka mkiona kivuli chake tu mnaogopa.

Mhukumuni kwa makosa aliyoyafanya.

Si kwa makosa mnayopiga ramli na kuona atayafanya miaka kadhaa ijayo.

Tanzania tuna udikteta mamboleo ambao hauhitaji mtu mmoja kuhodhi madaraka.

Tuna oligarchy utapokezana madaraka.

Magufuli anajua hilo. Ndiyo maana kaamua kuipoza hiyo oligarchy kwa kusema wasiwe na shaka, wasubiri zamu yao inakuja, yeye hana mpango wa kuharibu term limits.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom