Kagasheki: Mtindo wa Makonda kuwapa tumbo joto Mawaziri haufai. Dunia nzima kuna utaratibu wa kusikiliza kero za wananchi

Kagasheki: Mtindo wa Makonda kuwapa tumbo joto Mawaziri haufai. Dunia nzima kuna utaratibu wa kusikiliza kero za wananchi

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2020
Posts
3,315
Reaction score
5,058
Ameandika Khamis Kagasheki

"Duniani kote, Serikali ni kioo cha nchi. Katika nchi za Kidemokrasia vyama vya siasa hutafuta Dola na kuunda Serikali ambayo huwajibika kwa chama kile. Lakini style ya kutia kitimoto Mawaziri na Waziri Mkuu na kuwapa ultimatum hadharani haijengi bali ina madhara.”

“Ninakiri ulazima wa viongozi kutoa ufafanuzi wa mambo na kujibu hoja za Wananchi kwani wao ndio Waajiri wa Viongozi. Zipo njia nyingi za kuhoji Viongozi na kupata ufafanuzi kutoka kwao bila kuwavunjia heshima. Katibu Mkuu wangu, Daniel Chongolo style hii ya sasa, sio."
 
Utaratibu wa kusikiliza kero za wananchi haujaandikwa kwenye kitabu, ambacho ulimwenguni kote tunatakiwa kujifunza huko.

Kero za wananchi zinasikilizwa kwa namna mbalimbali kulingana na jiografia ya eneo husika, na desturi ya watu wa sehemu hiyo.

Sio lazima kwetu Tanganyika tujifunze namna wamarekani na wafaransa wanavyosikiliza kero za wananchi wao, hjko kutakuwa sawa na utumwa wa kifikra kwetu.
 
Utaratibu wa kusikiliza kero zs wananchi haujaandikwa kwenye kitabu, ambacho ulimwenguni kote tunatakiwa kujifunza huko.

Kero za wananchi zinasikilixwa kwa namna mbalimbali kulingana na jiografia ya eneo husika, na desturi ya watu wa sehemu hiyo.

Sio lazima kwetu Tanganyika tujifunze namna wamarekani na wafaransa wanavyosikiliza kero za wananchi wao, hjko kutakuwa sawa na utumwa wa kifikra kwetu.
Umempa za uso Kagasheki
 
Kagasheki hana lolote ni mmojawapo wa Viongozi waliokuwa wabinafsi alichangia pakubwa kudumaza Bukoba wakati wa enzi yake yupo Waziri na Mbunge wa Bukoba Mjini hakuna lolote alilosaidia Mkoa wa Kagera atulie tu muda wake umepita amwache bwana mdogo Makonda apige kazi.
 
Kagasheki hana lolote ni mmojawapo wa viongozi waliokuwa wabinafsi alichangia pakubwa kudumaza bukoba wakati wa Enzi yake yupo waziri na mbunge wa bukoba mjini hakuna lolote alilosaidia mkoa wa Kagera atulie tu muda wake umepita amwache bwana mdogo Makonda apige kazi.
Alikuwa waziri anayeitumikia nchi .....sio bukoba
 
Amekuwa Waziri na Balozi bila kuwa na positive impact kwa Wananchi.

Leo anataka watu waende kwa utaratibu, Je, utaratibu gani? Yaani aanzie Kata hadi kumfikia Rais itakuwa leo?

Wengi hufa au kupata shida wakiripoti ofisi za Serikali bila matokeo zaidi ya danadana na rushwa.

Haupo utaratibu maalum wa kutoa kero wala malalamiko na kujibu hoja, kama inamuuma hiyo njia ahamie Burundi
 
Kagasheki hana lolote ni mmojawapo wa viongozi waliokuwa wabinafsi alichangia pakubwa kudumaza bukoba wakati wa Enzi yake yupo waziri na mbunge wa bukoba mjini hakuna lolote alilosaidia mkoa wa Kagera atulie tu muda wake umepita amwache bwana mdogo Makonda apige kazi.
Wewe na Bashite naona akili zenu zinafanana
 
Utaratibu wa kusikiliza kero zs wananchi haujaandikwa kwenye kitabu, ambacho ulimwenguni kote tunatakiwa kujifunza huko.

Kero za wananchi zinasikilixwa kwa namna mbalimbali kulingana na jiografia ya eneo husika, na desturi ya watu wa sehemu hiyo.

Sio lazima kwetu Tanganyika tujifunze namna wamarekani na wafaransa wanavyosikiliza kero za wananchi wao, hjko kutakuwa sawa na utumwa wa kifikra kwetu.
Kila mtu ana staili yake ya Uongozi.

Provided Makanda hajatangaza kuwa yeye ndiyo Rais wa Nchi; afanye anavyoweza provided Mama ameridhia; na kwamba kwa kufanya hivyo havunji sheria za nchi na pia hamvunjii heshima mtu au kiongozi mwingine
 
Back
Top Bottom