Kagasheki: Mtindo wa Makonda kuwapa tumbo joto Mawaziri haufai. Dunia nzima kuna utaratibu wa kusikiliza kero za wananchi

Kagasheki: Mtindo wa Makonda kuwapa tumbo joto Mawaziri haufai. Dunia nzima kuna utaratibu wa kusikiliza kero za wananchi

Naunga mkono hoja, anachofanya hata Makamu wa Rais hawezi kufanya ni kama kuwashusha Mawaziri
Nakama Mwenezi amewashusha hivyo Mawaziri wa Serikali ya chama chake ni sawa na kutangaza hadharani kuwa CCM ina dhamana ya kuunda Serikali lakini imeshindwa na kuunda serikali mbovu isiyo wajibika kwa raia na inafaa kuondolewa.

Kazi hii anayoifanya Makonda a.k.a Bashite ni ya faida sana kwa wapinzani wa CCM kuliko CCM wanavyodhani kuwa ni uenezi kwao.

Asante sana Mr. Zero brain kwa kazi yako ya kutangaza kuwa CCM imechoka na inatakiwa kufanya overhaul kwa ujumla
 
Viongozi gani wakati watu wanateseka na hao viongozi wanapita na ma V8 bila kutoa msaada wowote.

Kila mahali rushwa na kero nyingi ndiyo maana watu wanatafuta mkombozi. Sasa sijajua kama Makonda anaweza kuwa mkombozi but time will tell.

Hii ni ishara mbaya sana kwa Serikali na chama tawala kwa mwendo huu wa Makonda ambao hauna dira inayoeleweka. Nchi inakuwa kama haina mwenyewe.
 
Tuna aminishwa kuwa Katibu Mwenezi ..... ni bosi wa wote Serikalini kuanzia Waziri Mkuu hadi yule wa nyumba kumi.

Ukiacha Kagasheki sijamsikia yeyote mwingine akisema neno. Naona Magufuli mwingine anatayarishwa tupende tusipende.
 
Utaratibu wa kusikiliza kero zs wananchi haujaandikwa kwenye kitabu, ambacho ulimwenguni kote tunatakiwa kujifunza huko.

Kero za wananchi zinasikilixwa kwa namna mbalimbali kulingana na jiografia ya eneo husika, na desturi ya watu wa sehemu hiyo.

Sio lazima kwetu Tanganyika tujifunze namna wamarekani na wafaransa wanavyosikiliza kero za wananchi wao, hjko kutakuwa sawa na utumwa wa kifikra kwetu.
Naunga mkono hoja 100%
 
Nani katoa ushauri kuwa mfumo wa matamko unasaidia?

Mfumo mkakati ndo uliobadilisha Malaysia, Indonesia na nyingine nyingi lakini matamko hayawezi kuondoa mgao wa umeme, ukosefu wa ajira, Wanafunzi kukosa Walimu, Hospital kukosa dawa na madaktari wanafunzi kukaa chini? mfumko wa bei Dollar kupaa na Shilingi kushuka, mdororo wa biashara, bili za maji mabomba kutoa upepo badala ya maji milipuko ya magonjwa
 
Kagasheki hana lolote ni mmojawapo wa viongozi waliokuwa wabinafsi alichangia pakubwa kudumaza bukoba wakati wa Enzi yake yupo waziri na mbunge wa bukoba mjini hakuna lolote alilosaidia mkoa wa Kagera atulie tu muda wake umepita amwache bwana mdogo Makonda apige kazi.
Kimsingi ndo ameifanya Bukoba ichekwe hadi leo kwa miundombinu mibovu kwa ugomvi wake na Mayor huyo.

Asingekuwa yeye Bukoba ingekuwa na Soko, Stendi Kuu, barabara za mjini zaidi ya km 20...

Ila ubinafsi wake ukasababisha pesa za World Bank kurudishwa. Sidhani kuna mtu anachukiwa na wana Bukoba kama huyu

Hata kujenga Airport ya Bukoba katikati ya mji huyu ndo sababu.
 
Ndg. Kagasheki kwa nchi za ulimwengu wa tatu kama Tanzania na ambapo upinzani na Wabunge hawana meno, jitihada na style ya Makonda vyahitajika sana.

Hebu wewe jiulize ni vipi mkoa mkongwe kama Kagera tena unaopakana na nchi 3 hakuna Kituo cha basi wala Soko la Kisasa kama mikoa mingine? Wachina wanasema katika kumkamata panya haijalishi kama paka ni mweusi au mweupe.
 
"Pamoja na kelele nyingi kwamba mateso yapo lakini kila kukicha watu wanapanda ndege wanakwenda, na msingi unaowaongoza ni uleule kheri nife nikijaribu kuliko kukaa naangamia bila kujaribu kwa sababu ambazo hazina mashiko, na ndiyo maana Serikali zetu zimeingia mikataba hii ili kuweka mazingira mazuri ya watu kwenda, yeyote anayetaka kwenda kufanya kazi nje afuate utaratibu kwa kupata uthibitisho wa hiyo ajira,"- Balozi Abdallah Kilima

#MkutanoIkulu
#EastAfricaTV
 
Nakama mwenezi amawashusha hivyo mawaziri wa serikali ya chama chake ni sawa na kutangaza hadharani kuwa CCM ina dhamana ya kuunda serikali lakini imeshindwa na kuunda serikali mbovu isiyo wajibika kwa raia na inafaa kuondolewa.
Kazi hii anayoifanya Makonda aka Bashite ni ya faida sana kwa wapinzani wa CCM kuliko CCM wanavyodhani kuwa ni uenezi kwao.
Asante sana Mr Zero brain kwa kazi yako ya kutangaza kuwa CCM imechoka na inatakiwa kufanya overhaul kwa ujumla
Naunga mkono hoja
 
Back
Top Bottom