Kagasheki: Mtindo wa Makonda kuwapa tumbo joto Mawaziri haufai. Dunia nzima kuna utaratibu wa kusikiliza kero za wananchi

Huwezi Kuwa mchafu ukatoa hoja ya maana! Kama unaujua umaana ungedeal na uchafu wako kwanza.

Kagasheki hana moral authority ya kumnyoshea mtu kidole!
Mkuu kumbuka hata saa mbovu kuna muda inasema ukweli!
 
Makonda anatukosea sana makada, nilifikiri amekaa benchi amejifunza kumbe kichwa bado iko loose.
 
Mama atakwambia hapendezwi lakini inasaidia...kama hutaki Makonda akuropokee fanya kazi yako kwa wakati sahihi
Kiufupi hiyo style haina tija, muda utatuambia
 
Viongozi wenyewe ndo wachangiaji wa kero za wananchi, ufisadi, ubabe, ujinga, kutojali wananchi, wizi wa Mali za umma, uzembe, na kutaka kutokukaripiwa, na kupenda kuabudiwa na kutokusemwa waziwazi kwaiyo makonda waseme na waropokee hadharani, hakuna staha yoyote anayostahili kiongozi asiyewajibika so Kagasheki kaa kimya wakati Makonda anafanya kazi. Mnataka tuwapetpet tena?
 
Mwizi mkubwa na kundi lile linaloishi kwa kuikamua nvhi hii!
 

Balozi yupi ana impact kwa taifa hili
 
Pole Sana, hakuna mpinzani wa kuitikisa CCM.
 
Mzee tulia ulishastafu mwache kijana afanye kazi wakati ilishapita

Nakumbusha hata manabii Zama hizo walipigwa na watu Kama nyinyi
 
Alikuwa waziri anayeitumikia nchi .....sio bukoba
Kagasheki aache ubabaishaji. Alikuwa waziri asiye na tija. Ni miongoni mwa mawaziri waliokuwa wanajisikia na kujiona kuwa wao ni watofauti.

Yaani Waziri kutoa majibu kwa kero za wananchi anasema ni kuwashushia heshima! Huyu mzee. Shida Africa uwaziri au uongozi tunaona ni mwanya wa kuwa mkubwa na kuwaweka wananchi chini.

Nimekuwa serikalini Viongozi wengi wenye nafasi kubwa wanajiona wao ni watu maalum. Uwa hawana muda kuonana na wananchi na kumaliza kero zao.

Mawaziri wengi wapo kutafuta fedha kwa maslahi yao. Tanzania imejawa na kero nyingi za wananchi. Hawana wa kumweleza awasaidie.

Makonda anatumia nafasi ya Ukatibu mwenezi kichama kuwafikia wananchi na kuwashirikisha mawaziri waweze kujibu kero hizo na wananchi waone jambo linafanyika.

Hivi Tanzania hii kumuona tu waziri ni kazi. Mwananchi wa kawaida tu hata kumuona Mkurugenzi wake au Mkuu wa Mkoa ni kazi. Ndo ije waziri anayeishi Dar kwenye viyoyozi.

Mzee huna hoja, na hakuna cha maana ulichofanya wakati wa uongozi wako. Umejawa na roho ya wivu tu. Mwache Makonda achape kazi kwa staili yake.
 
Hivi wakati kina Kinana na Nape wanaita mawaziri mizigo alikuwa wapi? Kinachoenda kwenye uchaguzi ni chama sio serikali. Kazi ya chama ni kuhakikisha serikali inatekeleza ilani ya uchaguzi.
Tabu yote ya nini wakati wana uhakika wa kutawala milele?
 
Mwenezi (wa CCM) Makonda kazi yake kuu ni kusikiliza na kutatua kero za wananchi wanyonge dhidi ya mawaziri na watendaji wa serikali ya CCM! Kwamba wanyonge sasa wamepata mtetezi. Kwamba serikali ya CCM ilikuwa haiwajali!This is comedy of the absurd!

Ni nchi ya ajabu sana hii. Rais na chama chake (CCM) wanaingia madarakani kwa “ushindi wa kishindo”. Wanaunda serikali “makini” na kutekeleza ilani inayotatua kero za wananchi. Halafu Rais anateua “mtetezi wa wanyonge” kusikiliza kero za wananchi na kuamrisha mawaziri na watendaji wakuu wa serikali hadharani kuzitatua! What a dysfunctional system!
 
Kagasheki anatumia mitandao kufikisha ujumbe,utadhani hajui Makonda,Mwigulu, January na wengine,wanao vijana kwenye mitandao yote na wanalipwa kwaajili ya kuwasafisha na kuanzisha propaganda mbalimbali?
Amakinike.
 
JPM alikuwa akifukuza hapohapo pasipokufuata utaratibu na wananchi mkawa mnashangilia sana, na akienda kwenye mkutano wa hadhara na siku hiyo asitumbue mtu watu wanatoka kinyonge kweli, lkn yaliyotokea wote tunajua ni lawama kwake kila kona.
 
Ktk job description yao kna "kskliza kero bila kupatia solution"! Kiila sku nawaona kuanzia UVCCM hadi KM wakizngka kufatlia kero za wananchi lkn kla mwk CAG anatoa ripoti chaf. Huyu Mwenezi yy anatoa ultimatum bila kujua jinsi ya kuzfatlia, nao wahusika wanazidharau, wanamjua. Ndo kusema Katiba ni kijitabu tu...nk
 
Kwa hiyo awape matumbo ya kwenye furiji siyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…