Kagera (Bukoba) mahali pa ovyo kuwahi kutembelea

Siyo kweli wengi choka tu mkuu. Hizo mbwembwe na za wale wenye fedha ila hata mhaya awe na fedha kidogo utadhani ni Mo kwa matambo hayo.
 
Ila kuna vitu kaviongelea zaidi ya lugha..na wengi wamedhibitisha hivyo..so inabidi watu wa huko wajifunze
 
Ila kuna vitu kaviongelea zaidi ya lugha..na wengi wamedhibitisha hivyo..so inabidi watu wa huko wajifunze
Mimi ni mhaya nimezaliwa Temeke lakini nimekulia bukoba nimesoma huko hdi form 4. Ukiwa ndani ya jamii huoni hizo dosari, ukitoka ukatafakari unagundua kuwa kuna shida.
Toka nimalize form 4, zaidi ya miaka 17 iliyopita nimekuwa narudi tu kutembea na kutazama ndugu. Mara ya mwisho nilikuwa bukoba 2021, aisee nilienda madukani kununua vitu nami nikarealize kuwa hakuna customer care. Mtu anakuhudumia kama vile hataki mara akitokea mtu anamfahamu anaacha kukuhudumia wanaanza kupiga story tu. Lakini wanaoishi katika jamii wanaona kawaida nadhani hata mimi nilinotice kwa sababu muda mrefu siishi bukoba.
Mji haubadiliki uko vile vile. Kuhusu ardhi, 5-10 nje ya mji lazima pawe ghali kwanza wenye ardhi wanaithamini na pia mji ule mdogo unapotential ya kupanuka hivyo lazima waiuze kwa bei ghali.
Ila ukienda 50km nje ya mji ardhi mashamba yanauzwa bei chee kabisa.
Kuhusu kutenga wageni sidhani. Kuna mtu hapo kazungumzia kuwa alienda kusoma kule akiwa mtoto akaathirika. Sasa nimemwelewa. Nakumbuka tukiwa sekondari kuna jamaa alihamia kutoka tanga, alikuwa anaongea lafudhi ya pwani. Alikuwa mashuhuri shule nzima kwa sababu ya jinsi anavyozungumza. WAtoto walikuwa wanaona anachekesha wanamtania, si kwamba walikuwa wanamtenga bali kwao ilikuwa kitu cha ajabu jinsi anavyozungumza kishwahili kwani mhaya na kiswahili wapi na wapi.
Lakini jamaa alifit in haraka na kila mtu alikuwa rafiki yake.
Pia bukoba hakuna pesa mzunguko ni mdogo. Kwa sasa hata mimi kuishi bukoba ni kipengele zaidi ya kwenda kusalimu na kuangalia mashamba ya urithi kuishi hapana kwa kweli.
 
Kyupi kikidondoka kubali kuchutama
 
Kumbe mahaya yapo nyuma sana.
 
Majivuno ni asili yetu kabisa mkuu. Yani inatokea automatically hata kama huna ela. Unaweza kuwa unamiliki kuku ukampa sifa utadhani ni ng'ombe. Sijui iko ndani ya genes kama mchaga na biashara.
Na mtu akawajua huwa anaishi vizuri sana na nyie 😁😁
 
Kagera (Bukoba) siyo mji wa kujitafuta, hakuna fursa na ukiiona fursa utakwamishwa mpaka ukimbie mwenyewe! Kifupi wamechagua kudumaa.
 
Na mtu akawajua huwa anaishi vizuri sana na nyie 😁😁
Shida ni kutujua tu. Ukishatuelewa mbona sisi watu poa sana kabisa. Kama hujamfahamu mhaya atakuwa anakukera kila wakati. Wewe unaweza fikiria kuwa anajisifu kumbe mwenzio anaongea kawaida hapo hajaanza kujisifu maana akianza utazimia.
Pia kujichanganya ilikuwa ni changamoto maana unaambiwa kabisa usije kutulete mnyamahanga, yani watu ambao si wahaya ukazaa au kuoa. Lakini mambo yanabadilika. Mimi sijaoa lakini nimeza na mchaga, ndugu zangu wote wameolewa na wachaga na mmoja kaolewa na msukuma, na sidhani kama ntaoa mhaya.
But kiburi na sifa at some point kuna watu huwa wanasema wewe jamaa una kiburi cha wahaya, kitu ambacho mimi sinotice kama ninacho na wala nakuwa sijalenga kuwa na kiburi.
 
1- Something triggered an already underlying trauma (inborn/ancestral).

2- Inawezekana vipi shule ya wanafunzi zaidi ya 200 wote wamchukie mtu mmoja? Tena mtoto mgeni? Ama mlikua watu 10 shule nzima? Waalimu walichukuliaje hali hii? Ulitoa taarifa popote? Wazazi?

3- Chanzo halisi cha kupoteza confidence yako ni kuishi Bukoba ama kuwa bullied na watoto wenzako? Waliishia kwenye maneno tu ama mpaka physical abuse?

4- Hao watu wa kule wanatafauti gani na wewe uliyeishi nao toka una umri wa miaka 9 tu duniani? Una hakika hakuna uliyo adopt/adapt katika makuzi yako kutoka kwao?

5- Kama ni ndugu zako, it means you were cut from the same cloth as them. What makes you think you are any different from them? Nyoka hazai bata, labda maabara ya mzungu.

6- Huwezi kumtambua mtu kwa macho, nasaba zinavutana kujuana. Kumbuka umesema una ndugu zako huko.

7- Hapa umefanya judgement due to your perception or personal experience or simply because wewe pia ni Wale Wale.

8- Umesema mpaka sasa Bado unapambania kurejesha confidence yako, haudhani the toxicity that runs in your DNA could be your main challenge?

9- Hapa unatushauri nini kuhusu wewe na kizazi chako?

10(a) Uko sahihi.
10(b) Hawa ndio wa kuzungumziwa kwa kina, wametumwa kufanya kazi gani Kama wameshindwa kuwamudu wazawa ili kutimiza miradi na mikakati ya maendeleo? Ni wadhaifu? Nao ni Wale Wale? Wapo kimaslahi zaidi?

11- Kwamba Bukoba ni NewYork watu watahitaji Visa kwenda kushuhudia hiyo 1980’s in 2025? Kwanini unaweka machumvi mengi sana?

12(a)- Wangekua hawanukii hakika husingetambua hata.
12(b)- Umeona, wananukia.

Nyanya chungu ndio moja ya mazao yao makubwa ya biashara na chakula, mashamba yao ya biashara na chakula yamezunguka makazi yao ya kuishi.

Matandiko yao ni majani yatokanayo na migomba ama ukoka mrefu, harufu yake ni kijani kibichi mpaka kufikia ukavu wake.

Matandiko hayo yamo barazani mpaka vyumbani wanamolala, hiyo harufu wataikosaje?

Hapo ulipo, usitumie chochote cha ziada kuficha harufu yako ya asili japo kwa siku 3…iache ichanganyike na mazingira ya kazi unayofanya, let’s say mbeba zege ama muuza samaki? Get the picture?

Halafu, hivi ulikua unazunguka unanusa watu kwenye mavazi yao au makwapa yao?

Ungejaribu kutembea kwenye ile miti yao mirefu usiku ufungue mapafu yako na harufu nzuri ya real African Pine 🌲.

13- We are all weird in the eyes of a stranger.

14- Kwamba alikua Rais wa hii nchi kwa miaka mingapi kiasi ionekane matatizo ya Bukoba yeye ndio kisababishi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…