Kagera: Katibu Tawala aagiza uchunguzi wasababu ya Walimu wengi kuomba kustaafu kabla ya kufikisha miaka 60

Kagera: Katibu Tawala aagiza uchunguzi wasababu ya Walimu wengi kuomba kustaafu kabla ya kufikisha miaka 60

Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Prof. Faustine Kamuzora amewaagiza maofisa wa idara ya elimu katika mkoa huo kutathimini sababu zinazochangia wimbi kubwa la walimu wa shule za msingi na sekondari mkoani humo za kuchukua uamzi wa kuomba kustaafu kazi kabla ya kufikisha umri wa miaka 60 wakati hawana matatizo yoyote ya kiafya...
Ukiona Prof anateuliwa kuwa Katibu Tawala na kukubali kuacha kufundisha Chuoni ujue kuna matatizo kwa uongozi mzima wa Nchi maana Kazi hiyo ilitakiwa ishikwe na mwanafunzi muhitimu wa Prof anayezunguka na bahasha ya khaki.

Prof angewapongeza walimu wanaostaafu kwa kuachia nafasi ili walimu ambao hawana ajira wajaze nafasi hizo. Professor nae astaafu kupisha vijana!
 
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Prof. Faustine Kamuzora amewaagiza maofisa wa idara ya elimu katika mkoa huo kutathimini sababu zinazochangia wimbi kubwa la walimu wa shule za msingi na sekondari mkoani humo za kuchukua uamzi wa kuomba kustaafu kazi kabla ya kufikisha umri wa miaka 60 wakati hawana matatizo yoyote ya kiafya...
Kamati ya Nini yeye hajui kwa nn wanaacha kazi?Profesa?hatari kweli kweli sababu hata mtoto wa shule ya msingi anajua.asubiri this ataona ongezeko.
 
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Prof. Faustine Kamuzora amewaagiza maofisa wa idara ya elimu katika mkoa huo kutathimini sababu zinazochangia wimbi kubwa la walimu wa shule za msingi na sekondari mkoani humo za kuchukua uamzi wa kuomba kustaafu kazi kabla ya kufikisha umri wa miaka 60 wakati hawana matatizo yoyote ya kiafya....
Hata wenye Mwaka mmoja wanataka namana ya kutoka huko, na sio waalimu tu, hata wengine wana mawazo sawa
 
Ni kitu kizuri vijana wanalia ajira wanasema wazee hawataki kuondoka vijana waingie.Kama wanastaafu mapema wanapunguza tatizo la ajira pia ili wapishe vijana

serikali ihamasishe watu kustaafu mapema kupunguza tatizo la ajira
Mnayo hela ya kuwalipa mafao yao au unahorojoka tu hapa.

Kuna wastaafu wana miaka 4 hawajalipwa mafao yao mpk leo.
 
Sasa kwani tatizo ni nini maana sheria iko very clear kuwa kustaafu Utumishi wa umma ni HIARI mtu afikishapo 55 na LAZIMA mtu afikishapo 60...?

Na kwa kazi ya ualimu, kazi ya kelele na unga wa chaki, 55 ni tosha kabisa. Ukisubiri ufikishe 60 utakuwa choka mbaya na wengine huwa matatizo ya kifua kutokana na vumbi la chaki....
 
Waweke mzigo mezani tu hata wa miaka 15 tu kazini mtu aruhusiwe kuchukua chake waone kama hawatabaki wenyewe...
Roho mbaya imewajaa unamnyima mtu hata nyongeza ya kawaida ya mwaka...

Yaani mpaka shetani mwenyewe aje kujifunza huu ukatili
 
Hii ngoma hakuna kutema wala kumeza!

Ukistaaf kwa hiyari kosa, ukiacha kazi kwenda private kosa, ukifundisha tuition kosa, ukidai nyongeza kosa, ukidai promotion kosa!...
Hatareeeeh sana lol.
 
Bila shaka huyo Katibu Tawala amekosa shughuli ya kufanya. Kwani Sheria si inamruhusu Mtumishi kustaafu kwa hiyari yake mwenyewe afikishapo huo umri wa miaka 55!

Aache kuwapangia watu maisha yao.
Pili walimu wamekua wazalendo, kutokana na uhaba wa ajira kwa vijana wao ambao tayari wana vyeti mbali mbali vya ualimu, wanaamua kustaafu ili kutoa nafac kwa vijana wao kuajiriwa kwenye nafac wanazo ziacha baada ya kustaafu.

Pia uncertainity ya kikokotoo,ambacho kinabadilika kutokana na wakubwa wanavyo jisikikia, kwahiyo wanachelea kikokotoo kisije kubadilika ,kikawaumiza zaidi ya hali ya sasa.

Mazingira magumu ya kazi nayo yanachosha ,kwahiyo mwalimu akifikia muda unao takiwa kisheria kustaafu anaondoka ili aachane na matatizo hayo.

Ucheleweshwaji wa mafao nao unachangia ,walimu wanaona waondoke mapema ili waanze kuhangaikia mafao yao wakiwa bado na nguvu kuliko kusubiri wamechoka ndio waanze kupigania mafao hayo.
 
Ukiona Prof anateuliwa kuwa Katibu Tawala na kukubali kuacha kufundisha Chuoni ujue kuna matatizo kwa uongozi mzima wa Nchi maana Kazi hiyo ilitakiwa ishikwe na mwanafunzi muhitimu wa Prof anayezunguka na bahasha ya khaki. Prof angewapongeza walimu wanaostaafu kwa kuachia nafasi ili walimu ambao hawana ajira wajaze nafasi hizo. Professor nae astaafu kupisha vijana!
Vijana ambao hawana ajira wanaoenda Sana kupishwa issue hapa ni kushighulikia changamoto zinazowakabili walimu hata ukipishwa ukaja wewe muda so mrefu utaanza kulalamika na utapoteza Hari ya kufanya kazi
 
Na mimi naagiza ufanyike utafiti kwa nini Professor hupo Kagera ofisini akiwa ni katibu tawala wakati kuna uhaba mkubwa wa maprofessor vyuo vikuu?....
Wamefuata maslahi uko ni pazuri kuliko darasani nchi hii walimu wote kwenye ngazi zote za elimu wako hoi wamebeba maumivu makubwa wanafanya kazi Haina allowance ,overtime mshahara ni mdogo kuwa mwalimu ni dhambi kwenye hili taifa
 
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Prof. Faustine Kamuzora amewaagiza maofisa wa idara ya elimu katika mkoa huo kutathimini sababu zinazochangia wimbi kubwa la walimu wa shule za msingi na sekondari mkoani humo za kuchukua uamzi wa kuomba kustaafu kazi kabla ya kufikisha umri wa miaka 60 wakati hawana matatizo yoyote ya kiafya.
Mchawi yupo anaye yeye mwenyewe huko kufanya utafiti ni kufuja fedha za walipakodi
 
Tuna viongozi wa ajabu kweli kweli. Hili nalo linahtaji uchunguzi wakati ni dhahiri watumishi wengi wanakimbia Kikokotoo cha 2023? Mnatengeneza sheria za kuumiza wananchi halafu Waziri wa sheria anaropoka eti hakuna sheria kandamizi Tanzania!!!
Ccm usipokuwa mropokaji unafukuzwa
 
Points of correction.
Kudhoofisha×
Kudhohofisha✓.
Walioudhulia×
Waliohudhuria✓.
Ni mtumishi mwenye matatizo ya akili tu ndiye ataweza kuendelea na kazi huku ametimiza umri wa kustaafu kwa hiari.
Kudhohofisha?

Unaongea kikuyu au.
Correct ni kudhoofisha
 
Wamefuata maslahi uko ni pazuri kuliko darasani nchi hii walimu wote kwenye ngazi zote za elimu wako hoi wamebeba maumivu makubwa wanafanya kazi Haina allowance ,overtime mshahara ni mdogo kuwa mwalimu ni dhambi kwenye hili taifa
Sasa kama ni uhalifu basi mhalifu anaagiza wahalifu wachunguzwe. Kituko cha awamu ya Tano
 
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Prof. Faustine Kamuzora amewaagiza maofisa wa idara ya elimu katika mkoa huo kutathimini sababu zinazochangia wimbi kubwa la walimu wa shule za msingi na sekondari mkoani humo za kuchukua uamzi wa kuomba kustaafu kazi kabla ya kufikisha umri wa miaka 60 wakati hawana matatizo yoyote ya kiafya.

Prof. Kamuzora ametoa agizo wakati akizungumza na walimu wakuu wa shule za msingi kutoka kwenye wilaya zote zilizoko mkoani humo waliohudhuria mafunzo maalumu yanayotolewa na wakala wa maendeleo ya uongozi wa elimu (ADEM), amesema uamzi huo unachangia kudhoofisha suala zima la taaluma kwani unapunguza nguvu kazi.
Life is tough.
Sa watafanya nini
 
Katibu Tawala Kagera unataka kufanya uchunguzi wa nini kama siyo kuharibu rasilimali? Ndungai alisema walimu waongezewe masomo, sasa limeongezwa somo la Historian ya Tanzania ambalo walimu watalifundisha bila semina.

Serikali imepanga kuleta kikokotoo, yaani kila mnachowaza ni kukandamiza walimu. Waache wastaafu ili Serikali iajiri wengine mbona vijana wapo wengi tu mtaani?

Waache walimu wastaafu. Yaani kama ingewezakana kustaafu katika umri wa 40,45 au 50 wangetoka wengi sana. Unawabana iweje? Waache wastaafu.
Mm nilifanya hiyo kazi nikiwa huko sekondari kwa miaka 12 nikajistaafisha,baada ya hapo nikaenda private miaka 3 nikajistaafisha tena.NSSF wakanirusha sh.5 yangu,nikawa mjasiria mali.

Ni kazi ambayo inataka moyo kunifanya ,imejaa manyanyaso.

Kwanza angalia mabosi wa mwalimu na wote wanaweza kutoa maelekezo muda wowote: yawe ya kujenga/kunyanyasa/yasiyo na msingi.
Mkit wa mtaa/kijiji
Afisa mtendaji wa kata/Kijiji
Mratibu Elimu kata
Mwl mkuu/mkuu wa shule
Afisa elimu na DED na Katibu wa TSD
Afisa elimu mkoa
Management ya utumishi wa umma
Waziri wa elimu
Ofisi ya waziri mkuu
Raisi

Kwa muda niliofanya hiyo kazi,watu wote hao wanaweza kuja shuleni muda wowote wakatoa maelekezo,wakakutisha na hata kukukebehi, mbaya zaidi anaweza kuwa mwalimu km ww ana kadiploma tu anakebehi watu wenye hata digrii 2. Yani kila mmoja na lake.Yaani waalimu ni kichwa cha mwendawazimu kila mtu anajifunzia kunyoa.

Nilikua na diploma na bachelor ya elimu,na bachelor ya business administration,anakuja mjinga aliishia la nne anajiita mkiti wa mtaa naye ananielekeza Cha kufanya tena kwa mambo mengine ambayo ni ya kiprofesheno.
 
Back
Top Bottom