Katibu Tawala Kagera unataka kufanya uchunguzi wa nini kama siyo kuharibu rasilimali? Ndungai alisema walimu waongezewe masomo, sasa limeongezwa somo la Historian ya Tanzania ambalo walimu watalifundisha bila semina.
Serikali imepanga kuleta kikokotoo, yaani kila mnachowaza ni kukandamiza walimu. Waache wastaafu ili Serikali iajiri wengine mbona vijana wapo wengi tu mtaani?
Waache walimu wastaafu. Yaani kama ingewezakana kustaafu katika umri wa 40,45 au 50 wangetoka wengi sana. Unawabana iweje? Waache wastaafu.
Mm nilifanya hiyo kazi nikiwa huko sekondari kwa miaka 12 nikajistaafisha,baada ya hapo nikaenda private miaka 3 nikajistaafisha tena.NSSF wakanirusha sh.5 yangu,nikawa mjasiria mali.
Ni kazi ambayo inataka moyo kunifanya ,imejaa manyanyaso.
Kwanza angalia mabosi wa mwalimu na wote wanaweza kutoa maelekezo muda wowote: yawe ya kujenga/kunyanyasa/yasiyo na msingi.
Mkit wa mtaa/kijiji
Afisa mtendaji wa kata/Kijiji
Mratibu Elimu kata
Mwl mkuu/mkuu wa shule
Afisa elimu na DED na Katibu wa TSD
Afisa elimu mkoa
Management ya utumishi wa umma
Waziri wa elimu
Ofisi ya waziri mkuu
Raisi
Kwa muda niliofanya hiyo kazi,watu wote hao wanaweza kuja shuleni muda wowote wakatoa maelekezo,wakakutisha na hata kukukebehi, mbaya zaidi anaweza kuwa mwalimu km ww ana kadiploma tu anakebehi watu wenye hata digrii 2. Yani kila mmoja na lake.Yaani waalimu ni kichwa cha mwendawazimu kila mtu anajifunzia kunyoa.
Nilikua na diploma na bachelor ya elimu,na bachelor ya business administration,anakuja mjinga aliishia la nne anajiita mkiti wa mtaa naye ananielekeza Cha kufanya tena kwa mambo mengine ambayo ni ya kiprofesheno.