Kagera: Katibu wa Mbunge Jimbo la Muleba Kusini atiwa hatiani kwa kujipatia milioni 60 fedha za mfuko wa vijana

Kagera: Katibu wa Mbunge Jimbo la Muleba Kusini atiwa hatiani kwa kujipatia milioni 60 fedha za mfuko wa vijana

Anaandika Mo Mlimwengu.

Wakati Rais wetu Dr Samia Suluhu akipambana usiku na mchana kuhakikisha nchi yetu inakua kiuchumi. Kuna baadhi ya watu na wao wanapambana kuhakikisha wanajifaidisha wao kutokana na ubinafsi wao. Ofisi zao wanazitumia vibaya kuhakikisha wananchi wanazidi kuteseka. Rais wa America Abraham Lincolin aliwahi kusema "You can fool all of the people some of the time, and some of the people all of the time, but you can't fool all of the people all of the time".
Kwamba utawadanganya watu wote kwa kipindi fulani cha muda na utawadanganya baadhi ya watu kwa kipindi cha muda wote lakini huwezi kuwadanya watu wote kwa kipindi cha muda wote.

Katibu wa mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini ndg Adelilius Vedasto Apolinary ambaye ni Mkiti wa Kikundi cha Umoja wa vijana wa Youth Fund amehukumiwa tarehe 03/10/2023 kwa kosa la kufanya utapeli kwa kuidanganya ofisi ya Mkurugenzi. Aliweza kugushi nyaraka za kikundi na kugushi saini za watia saini wa kikundi na kujichukulia kitita cha milioni 60 za kikundi. Kinachohuzunisha zile hela hazikutumika kwenye mradi ambao ulikusudiwa bali alizitumia kwa matumizi yake binafsi.

Wanakikundi wenzake baada ya kugundua mchezo mchafu ambao kaufanya na kujua kwamba wao siyo sehemu ya mradi na kikundi kajimilikisha mwenyewe. Wasiwasi ni akili waligundua watadaiwa hela hizo wakati wao hawahusiki. Ilibidi waende kushtaki tuhuma hizo na kupeleka malalamiko yao kwenye sehemu husika.

Kitendo cha Mwenyekiti huyo kuwa kwenye ofisi ya Mbunge ulikuwa ni kama mfupa mgumu kwa vyombo vya usalama. Lakini kitendo hicho alichofanya katibu huyo kiliwakera watu wengi hivyo kelele zilizidi kuwa nyingi. Kumbuka hizo kelele zilianza tangu mwaka jana mwezi kumi. Naishukuru serikali yetu kuwa sikivu , Mh Dr Abel ambaye ni mkuu wa wilaya pamoja na vyombo vya usalama waliweza kusikiliza kero za wananchi na kuanza kuzifanyia kazi.

Mtuhumiwa akiwa anazidi kutamba kwamba ofisi ya Mbunge haiwezi kuguswa alisahau kwamba serikali mkono wake huwa ni mrefu. Halmashauri ya wilaya chini ya Mkiti Mh Magongo na wao waliweza kufuatilia vyema kuhakikiha mapato ya serikali yanasimamiwa vyema na hata mikopo inayotolewa kwa vikundi inaenda kufanya kazi kama ipasavyo.

Waliosema za mwizi ni arobaini huenda walienda mbali sana huku kabla arobaini hazijafika tayari mwizi alishanaswa kwenye tundu bovu. Hukumu imetolewa ambapo afungwe miezi sita au alipe laki tano kwa ajili ya kupata dhamana. Lakini ndani ya miezi mitatu tayari milioni 60 ziwe zimeisharudishwa halmashauri. Hukumu imerejesha furaha kwa watu, hukumu imewafuta machozi wanyonge wengi, hukumu hii imewapa imani wananchi dhidi ya viongozi wao wa kiserikali, hukumu hii imefanya wananchi waamini vyombo vya usalama vipo kwa ajili ya kuwasaidia wananchi kwa kulinda amani pamoja na mali zao.

Mlimwengu mimi nimefurahi sana kwa hukumu ya leo maana imeonyesha haki inaweza kucheleweshwa lakini baadae inapatikana. Vyombo vya usalama pamoja na mahakama niwashukuru kwa mara nyingine kuhakikisha haki inapatikana. Tunaamini hizi hela zikirudi wataweza kupata watu wengine ambao wataweza kujikwamua kimaisha na wenye kustahili. Serikali yetu ina nia ya dhati ya kuwakwamua watu sema kuna baadhi ya watu wenye nia mbaya na serikali yetu ndio wanaokwamisha. Lakini hii imeonyesha namna tulivyo na viongozi imara wa kusimamia watu pamoja na rasilimali zao.

Ashakum si matusi bwana Katibu alivamia mtumbwi wa vibwengo. Hii ni Muleba na ina viongozi imara. Tuwakatae wote wanaotaka kutumia ofisi za umma kwa faida zao binafsi. Muleba bila wizi inawezekana, Muleba bila ufisadi inawezekana na Muleba bila ubadhilifu wa mali za umma inawezekana.

N:B. Nitakuwa mchoyo wa shukrani nisipowashukuru watu wote ambao hamkujali kuonekana tofauti kwa macho yao kwa kupinga utapeli wa katibu wa kujimilikisha milioni 60. Tukutane wote peponi nitakuwa mstari wa kwanza.

#kataawahuni
#kataavibaka
#kataamajambazi
#kataauvuviharamu

Mohamed.I. Rwabukoba
Mlimwengu.
 
Alikosea kula nyingi peke yake.
Hizo hela huwa zinadonolewa kidogo kidogo sehemu tofauti. Ukikwapua nyingi uwe na watu.
 
Back
Top Bottom