Kagera: Mchepuko aua Mchepuko kwa wivu wa mapenzi

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia Derick Dambuve (26), kwa tuhuma za kuwaua Mama na mtoto wake mwenye miaka 2, baada ya mtuhumiwa kumtaka Mama huyo kimapenzi wakiwa baa na kukubaliwa, lakini baadaye alimkuta mwanamke huyo akishiriki tendo la ndoa na rafiki yake.

Kagera.jpg

=======
Jeshi la polisi mkoani Kagera linamshikilia kijana mmoja aitwaye Derick Dambuve mwenye umri wa 26 kwa kumuua mke wa mtu, aitwaye Helda Amon (28) na mwanae Gradnes Amon (2) baada ya kufumaniwa mwanamke huyo 'Helda' akifanya tendo la ndoa na Kajere Ibrahim (mchepuko mwingine) nyumbani kwa Derick.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi amesema kuwa tukio hilo limetokea Agosti 22, mwaka huu katika kijiji cha Mukoma wilaya ya Ngara mkoani Kagera na uchunguzi wa awali umebainisha kuwa Helda alikuwa mke wa mtu, yeye na mwanae Gradnes walikwenda kijiji cha Mukoma kwa ajili ya kushiriki mnada wa gulio, akiwa gulioni hapo aliingia kwenye kilabu cha pombe ambako ndiko alikokutana na Derick na kuanzisha mahusiano.

"Baada ya kuanzisha mahusiano siku hiyo hiyo walikubaliana kuwa wangekuwa pamoja usiku huo, ndipo Derick alipomkabidhi Helda kwa rafiki yake (Alex Gray) ili ampeleke nyumbani kwake atamkuta baada ya kumaliza kufanya kazi ya ujenzi ambayo alikuwa hajaikamilisha.

"Derick aliacha amewanunulia pombe akaenda kumalizia kibarua chake, walipomaliza kinywaji Alex alimpeleka Helda nyumbani kwa Derick na kumfikisha salama akamuacha akimsubiria mwenyeji wake 'Derick'," alisema Malimi.

Malimi alisema wakati Helda na mwanae wanaendelea kumsubiri Derick nyumbani hapo ndipo Kajere alipofika ambaye naye alimuomba Helda waanzishe mahusiano ombi ambalo lilikubaliwa na kuanza kutenda tendo la ndoa nyumbani kwa Derick.

"Wakati wakiendelea kutenda tendo la ndoa nyumbani kwa Derick ndipo Derick mwenyewe aliporudi nyumbani na kuwakuta bado hawajamaliza na baada ya Kajere kugundua kuwa wamefumaniwa alifanikiwa kumkimbia na kumuacha Helda.

Kufuatia fumanizi hilo, Derick alimpiga Helda kwa kutumia silaha mbalimbali ikiwemo kifaa cha mazoezi cha kunyanyua kwa ajili ya kutunisha kifua na kumsababishia mauti.

Baada ya Derick kuwa tayari amemuua Helda, naye mtoto Gradnes alianza kulia jambo lililosambabishia Derick hasira na kuanza kumshambulia kwa kumpiga na kifaa hicho cha mazoezi na kusababisha kifo cha mtoto huyo", ameeleza Kamanda Malimi.

Malimi alisema kwa sasa Derick anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Helda na mtoto wake Gradnes na upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakani kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.
 
Hiyo kitu Mungu aliifanya tamu sana aisee, yaani mchepuko wako unauonea wivu hadi unaua...duh... Mwenye mume je afanyaje
 
Back
Top Bottom