Kagera: Watoto 10 wamefariki na 6 kujeruhiwa baada ya shule Msingi Islamic Byamungu kuwaka moto

Kagera: Watoto 10 wamefariki na 6 kujeruhiwa baada ya shule Msingi Islamic Byamungu kuwaka moto

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Watoto 10 wamefariki na sita kujeruhiwa vibaya kufuatia moto ulioteketeza bweni la wavulana shule ya Msingi Islamic Byamungu iliyopo Kyerwa Mkoani Kagera. Hadi sasa chanzo moto huo hakijajulikana.

Watoto waliopoteza maisha ni wa umri wa miaka sita hadi 12.

Taarifa zaidi inakuja...

CFDD1193-D0E8-4034-A950-B4AB4B73A9B7.jpeg


====

Wanafunzi 10 wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa baada ya bweni la shule yao ya Byamungu English Medium Primary School iliyoko wilayani Kyerwa kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo.

Jumla ya wanafunzi 74 walikuwepo kwenye bweni hilo ambalo chanzo cha moto hakijajulikana

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesitisha shughuli za malazi katika shule hiyo kwa muda.’’ Nachukua hatua nyingine za ziada, hatua ya kwanza na ya awali kabisa tunasitisha huduma za malazi katika shule hii watoto wote waliokuwa wakilala katika huduma ya hosteli au bweni huduma hiyo sasa imesitishwa mbaka itakavyoelekezwa vinginevyo’’, amesema Brigedia Jenerali Marco Gaguti alipotembelea eneo la tukio.

Amesema Sambamba na ameelekeza kamati za usalama za ngazi zote kataika mkoa wa kagera kufanya mapitio upya ya shule zinazotoa malazi, kuhakiki kwamba shule hizo kama zinavyo vibali halali vya serikali na ubora wa majengo yanayotumiwa na wanafunzi, na kuangalia mifumo ya uzimaji moto na kujiokoa inapo.

Amesisitza kuwa kama sifa hizo hazitakua zimekidhi basi hatua zichukuliwe za kufungia huduma hizo katika shule husika.

Amesema kuwa serikali itagharamia mazishi ya wanafunzi 10 waliopoteza maisha kufautia ajali ya moto na wengine waliojeruhiwa watapatiwa matibabu kwa gharama za serikali

Awali Mwenyekiti wa kijiji Bw. Munaraka Muhammod aliwaomba watu walioko katibu na Itera wafike kusaidia kuuzima moto huo uliowaka kuanzia jana usiku .

Chanzo za ajali baado hakijajulikana.
 
Natoa pole sana kwa wazazi wa watoto hao marehemu. Mwenyezi Mungu awapungue adhabu ya kaburi hao watoto na wale majeruhi awajalie uponyaji.
 
Poleni wafiwa kwa maafa yaliyotokea. Kuna ulazima wa Serikali kufanya uchunguzi na ukaguzi wa kina kwenye shule zote za bweni na pia zile zenye hostel, kuona kama viwango vya ujenzi vimezingatiwa ili kuepusha maafa ya aina hiyo kuendelea kujirudia.
 
Poleni wafiwa kwa maafa yaliyotokea. Kuna ulazima wa Serikali kufanya uchunguzi na ukaguzi wa kina kwenye shule zote za bweni na pia zile zenye hostel, kuona kama viwango vya ujenzi vimezingatiwa ili kuepusha maafa ya aina hiyo kuendelea kujirudia.
Mkuu kuna shida kwa hizi shule za kiislamu na mm binafsi nasema kuna ugaidi unaoendelea Serikali ifanye uchunguzi.
 
Nyie watu msitutanie na maisha ya watoto wetu wa shule , hizi shule zinafululiza kuchomwa moto kama utani na hakuna watuhumiwa wanakamatwa haiwezekani kabisa roho inauma sana. Ilianza mwanza , dar, moshi, kagera bado mnasubiri kuhesabu mikoa tuu iongezeke? Tafadhali serikali na watu wote tuchukue hatua tuwataje wahusika waadhibiwe.
 
KWANINI SHULE ZA WENZETU ZINAUNGUA KIASI HIKI?!! WAPENDWA SOTE TU WATANZANIA, TUSIKAE KIMYA KUHUSU HILI TUNAHITAJI TUME KUCHUNGUZA KUNA NINI NDANI?! HAIWEZEKANI HILI, MACHUNGU YA KUZAA KUSOMESHA HALAFU MWANANGU ANAKUFA KWA UZEMBE HILI HAIWEZEKANI INAUMIZA SANA SANA SANA..FIKIRIA UWE WEWE MWANAO NDO AFARIKI KWA NAMNA HII OHOOO JAMANI JAMANI JAMANIII[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji2367]
 
Back
Top Bottom