Kagera: Watoto 10 wamefariki na 6 kujeruhiwa baada ya shule Msingi Islamic Byamungu kuwaka moto

Kagera: Watoto 10 wamefariki na 6 kujeruhiwa baada ya shule Msingi Islamic Byamungu kuwaka moto

Watoto 10 wamefariki na sita kujeruhiwa vibaya kufuatia moto ulioteketeza bweni la wavulana shule ya Msingi Islamic Byamungu iliyopo Kyerwa Mkoani Kagera. Hadi sasa chanzo moto huo hakijajulikana.

Watoto waliopoteza maisha ni wa umri wa miaka sita hadi 12.

Taarifa zaidi inakuja...

Hii inatakiwa kuwa breaking news..
 
Watoto 10 wamefariki na sita kujeruhiwa vibaya kufuatia moto ulioteketeza bweni la wavulana shule ya Msingi Islamic Byamungu iliyopo Kyerwa Mkoani Kagera. Hadi sasa chanzo moto huo hakijajulikana.

Watoto waliopoteza maisha ni wa umri wa miaka sita hadi 12.

Taarifa zaidi inakuja...

Inauma sana. Shule za kiislam kuungua moto kila kukicha nj jambo la kusikitisha Sana. Kwanini jeshi la polisi linashindwa kubaini wanaoratibu huu uhalifu?

Hii sio bahati mbaya ni wazi kuna wahalifu wanaratibu haya matukio kwa ajenda ovu! Badala ya kushughulika na wahalifu serikali inashughulika na wapinzani wasiojua hata kushika bunduki.

Lawama zote kwa jeshi la polisi!
 
Acha Udini na Siasa kwenye janga kama hili.
Sasa udini upi hapo? Lazima watu tushangae ni kwanini haya matukio kipindi hiki yamekuwa mengi sana kwenye shile za kiislamu!! Kwani toka ilipoanza ile ya kinondoni, haipiti wiki mbili hujasikia shule nyingine imeungua!! Japo kuna wengine walikamatwa juzi juzi hapo, dar kwa kuhusika kuichoma shule, na ni miongoni mwa waislam wenzao!! Sasa mtu akihoji mnakimbilia eti aache siasa /udini!!!
 
Mungu awapumzishe mahali pema peponi

Hivi Majaliwa si aliunda tume kuchunguza hili la shule za Waislamu kuungua? Majibu ya tume hiyo hayajatoka?
 
Acha Udini na Siasa kwenye janga kama hili.
No sio udini,kwa siku za karibuni,shule za kiislam zimeungua moto kama nne au tano, kwahiyo katika uchunguzi wao wasikose kuangalia katika misingi hiyo pia, kunaweza kuwa na hujuma
 
Back
Top Bottom