Kagera : Yaliyojiri kwenye Maandamano ya Amani yaliyoandaliwa na Chadema

Wana bodi. Chadema hivi punde wanaaza maandamano ya Amani katika mji wa Bukoba mkoani Kagera. tayari tupo eneo la mafumbo kashai yanapoanzia maandamano hayo hadi uwanja wa uhuru maarufu kama mayunga.

Tarrifa ambazo uchumi TV imezipata ni kuwa kuna kutoelewana baina ya viongozi wa chadema na polisi juu ya njia kwa kuwa chadema wanataka kupitia soko kuu la bukoba kisha kupinda kuelekea stendi kuu hatimaye uwanjani wakati polisi hawaoni sababu za kupitia sokoni wakati njia inanyooka kuelekea uwanjani.

Njia inayopendekezwa na chadema ni kutoka Kashai,hadi kwenye mataa njia panda ya Nshambya,lakini wanataka wakifika Bugabo house wateremke na njia ya kuelekea dampo la kuu kisha kuchepuka na njia nya bamboo na kukunja tena kuelekea mataa ya CRDB kuelekea stendi kisha uwanja wa mayunga

polisi wanataka wakitoka Kashai,hadi kwenye mataa njia panda ya Nshambya,lakini wanataka wakifika Bugabo house wasichepuke bali wanyooshe hadi mataa ya CRDB kuelekea stendi kisha uwanja wa mayunga.

hatujapata kujua nini hatma ya njia hizo.

Tutaendelea kuwajuza kwa picha text,video na picha.

View: https://youtube.com/live/POK4oXZcFyE?feature=share
 
Yote uliyotaja sio matatizo ya hao ndugu zet.Fikiria tena
 
 

Attachments

  • photo_2024-04-22_12-39-36.jpg
    308.6 KB · Views: 1
  • photo_2024-04-22_12-39-41.jpg
    236.7 KB · Views: 1
Nipo hapa ELCT-Bookshop ila maandamano yamedoda bojo
 
Wiki ya mazoezi ukiwauliza toka wameanza kuandamana kuna impact gani hawana majibu hiii week itaisha mama samia hajatikisa hata nywele yaani haogopi

Maandamano ambayo mtawala haogopi jua ni geresha tu

Jogging la chadema
 
Huko Moshi Maandamano yatafanyika siku ya Mwisho 😂😂
 
Reactions: Tui
Maaaana yaaakee hiiii ndio idadi kamili ya wanachama mkoa mzimaa
 
Muitikio wa wananchi kwenye maandamano haya ni mdogo sana. Inaonekana bado hawajaguswa mioyoni mwao.
 
Picha ya Siku : Diwani wa ccm ashiriki Maandamano .

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…