Kagera : Yaliyojiri kwenye Maandamano ya Amani yaliyoandaliwa na Chadema

Chadema wamekumbuka ngome zao za asili. Namuona Chief hapo, matata sana, wananchi wanasema Chief ni mbunge wao, ila anacheleweshwa tu.

Ta Byabato amekimbia jimbo kwa muda mrefu, anajenga majumba Mwanza na Dodoma, amesahau kwao Kagera.

Huku na kule CCM kuna kaka yake na JAMCO amemkaba Byabato mpaka kwenye nyusi, huyu jamaa alimshinda Byabato kwenye kura za maoni, Byabato alishinda uchaguzi kwa kupigiwa kura na wazee wa makoti meusi pale mlima wa Kashura. Zikapigwa sana bomu za machozi
 
Jambo jema kabisa. Tushikilie hapo hapo. Maana wahafidhina wa ccm wamemuweza. Amegeuka na kuiacha nia yake njema aliyokuwa nayo toka mwanzo. Waliomgeuza moyo na walaaniwe kabisa kwa sababu hawajali uhai wa watanzania nyakati za uchaguzi hasa pale walioshinda wanapopokwa ushindi wao kutokana na tume ya uchaguzi kama ya akina mapesa (mahela).
 
Mkuu bagamoyo nakuona Online , karibu useme neno
 
Polisi wa Usalama wa Barabara mjini Bukoba akisoma Bango la Kikokotoo kwa Umakini

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…