Kagoda: Ni Rostam

Kagoda: Ni Rostam

kazi nzuri ya majina ya makampuni yaliyotufisidi lakini naomba kutoa marekebisho kidogo kuhusu umiliki wa Njake Hotels mmiliki ni Japhet Lema sio Jeetu Patel
 
Tusikubali kamwe Kagoda itushinde

Na Mbasha Asenga
Source: Mwanahalisi~Maslahi ya Taifa Mbele


ZIPO simulizi nyingi zinazoelezea hatari mbalimbali. Wapo wanaotumia joka hatari kama nondo mla watu; wengine hutumia mijitu ya miraba minne inayoishi mapangoni; na wengine hutumia majina ya wanyama wakali.

Haya yote yanatumika kuasa au kufunza watoto kuchukua hadhari maishani mwao. Ni simulizi za kuwatisha ili wapende uadilifu.

Inashangaza kuwa hata leo, yapo majina au vitu ambavyo vikitajwa tu huonekana ni vya kutisha kama mijitu; nondo na wanyama wakali.

Kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, moja ya makampuni 22 yaliyochota kwa njia haramu Sh. 133 bilioni kutoka Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ilioko Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ni mfano wa ninachokieleza. Inaweza kutajwa kama moja ya vitu vya kuogofya.

Katika kashfa ya aina yake kwa serikali, imethibitishwa na maodita wa Ernst & Young kuwa Kagoda ilichota Sh. 40 bilioni (Dola 30.8 milioni); kiasi ambacho ni asilimia 30 ya fedha zote zilizoibwa EPA.

Wengi wanaona Kagoda ndiyo kampuni asisi ya ufisadi huu na wala muono huo si kwa bahati mbaya, bali ni kwa vile ilivyojipanga ikafanikisha uchotaji huo huku ikimwingiza mtegoni Gavana wa BoT wakati huo, Daudi Ballali.

Si hivyo tu. Ilimvuta ndani aliyekuwa Waziri wa Fedha, Zakia Meghji, mwanamke wa kwanza kushika wizara hiyo tangu uhuru. Na kikubwa kuliko yote, ni namna viongozi serikalini walivyoshindwa kuwa na ujasiri wa kuieleza vizuri Kagoda.

Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, mfanyabiashara aliyethubutu kusimamia kwa dhati mapambano ya ufisadi ili kumsaidia Rais Jakaya Kikwete katika azma ya kukomesha ufisadi, ameuliza: Huyu mdudu Kagoda hasa ni nani?”

Mengi angali anashangaa imekuaje hasa serikali haijathubutu kueleza kwa ufasaha taarifa muhimu zinazoihusu kampuni hii iliyoiba fedha nyingi za umma?

Kwa hakika, viongozi wote serikalini wanakosa amani wakiulizwa chochote kuhusu Kagoda inayojitokeza mfano wa jini linalotafuta damu. Inapotajwa tu, kila mmoja hunywea na kujiona kama damu yake inasisimka kwa sababu mumiani yu karibu naye.

Nini kinasukuma Kagoda kuogopwa hivi? Sababu ni nyingi ila mbili ni dhahiri; ya kwanza: Kagoda ni dhambi mbaya iliyotendwa na baadhi ya watendaji serikalini kwa kushirikiana na wafanyabiashara na kwa maana hiyo wapo wengine wasiotaka kabisa kukaribia dhambi hiyo. Lakini ya pili inayoogofya zaidi ni kwamba imethibitishwa dhambi hiyo ni mbaya maana imeathiri baadhi ya watu waliokuwa na madaraka.

Kagoda inahusika sana katika sababu zilizomtoa roho Ballali; pia ina mkono katika sababu za Meghji kutoteuliwa tena Waziri wa Fedha na pengine popote baada ya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa Februari mwaka jana serikali ilipoanguka kwa kujiuzulu Waziri Mkuu, Edward Lowassa.


Lakini Kagoda ndiyo chimbuko la sakata lote la EPA maana baada ya maodita wa Deloitte & Touche kung’amua ufisadi wao na baadaye Ballali akaamua kudanganya na tena kuvunja mkataba nao, ndiyo mambo yote maovu yakaibuka kuhusu wizi ndani ya BoT.

Ni Kagoda hiyohiyo ilimsukuma Waziri Meghji kuandika barua ya uongo – na akaifuta huku akijitetea kuwa alidanganywa na Ballali baada ya kubaini ameingia mtegoni – kwa Deloitte. Kwanini Kagoda isitishie wakubwa na kukwepwa na watumaini madaraka milele!

Sasa kama huu ndio ukweli wa Kagoda na kwa kuwa viongozi hawataki kufungamanishwa nayo, ni kwa nini basi wasithubutu na kuhimiza suala lake kumalizwa haraka ili wapate kupumua?

Wiki iliyopita magazeti yaliripoti kuwa jalada la Kagoda alipelekewa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Elieza Feleshi. Baada ya kulipitia, akamrejeshea Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba.

Ripoti zikaeleza DCI anatakiwa na anafanya uchunguzi wa kuthibitisha taarifa ambazo hazijijajulikana akishirikiana na makachero wa nje.

Majibu na mbinu zote zinazotumiwa na vyombo vya usalama kuchunguza Kagoda ni vichekesho. Kwanza wanaoogopa kuzungumzia Kagoda wanaendeleza unafiki mchana kweupe; kwa sababu wanajua wazi kilichotokea na kilitokeaje.


Maelezo na mbinu za kukwepa ukweli wa Kagoda ni mbinu tu za kupoteza muda ili Watanzania wasahau. Tatizo kwa wakubwa, ni “mbona Watanzania hawasahau?”

Lakini tukija kwa uchunguzi huu mpya, ipo shida nyingine. Hivi si kweli kwamba Sh. 40 bilioni zilichotwa BoT, na si kweli kwamba ziliingizwa benki za humuhumu nchini? Na je, si ni kweli wapo watu waliokwenda kwa miguu BoT kuchukua fedha iwe kwa hundi au zililipwa kwa mtandao na wahusika wanajulikana?

Na je, si ni kweli kwamba benki hizo zipo nchini na kwa mujibu wa sheria za nchi zinapaswa kushirikiana na vyombo vya dola kuzuia uhalifu?

Watu wanajiuliza hivi sababu ya kuikuza Kagoda ili ionekane kama kampuni yenye hadhi maalum, inayoshughulikiwa kwa hadhari kubwa kiasi cha kufanya mambo mengine ambayo wananchi wanaanza kuhoji utashi wa kuwafikisha mahakamani wezi wa Kagoda nini hasa? Analindwa nani na kwa maslahi gani; ya nani? Ya taifa au ya kikundi kidogo cha wahalifu?

Kwa nini Kagoda imeruhusiwa kutikisa serikali na nchi kiasi hiki? Mwalimu Nyerere katika hotuba zake alipata kusema “ni lazima serikali iwatishe wala rushwa.” Alisema hivi kwa sababu yupo mwehu mmoja akibwabwaja mitaani eti “ameiweka serikali mfukoni.”

Mwalimu pia alihoji huyu binadamu anayeiweka serikali mfukoni, ana mfuko mrefu kiasi gani hata kushinda nguvu za serikali? Hili ndilo swali la kujiuliza kuhusu Kagoda; inaengwaengwa, inaogopwaogopwa na kuangaliwa kama jini vile au jitu linalotisha, linaloweza kumeza watu, kila kiongozi akitajiwa Kagoda anataharuki, kwanini lakini?

Lazima serikali ikae macho na ikatae mbinu chafu zinazojengwa ili kuionyesha Kagoda jini nyonya damu. Serikali ijiepushe na mbinu zozote zinazolenga kukwamisha au kuzuia Kagoda kubanwa na wahusika wake kushitakiwa.


Na Serikali ina sifa moja; ina mkono mrefu wa kufika popote. Mbona haiutumii mkono wake kufika benki na kuchukua taarifa muhimu za vile Kagoda ilivyochota mabilioni, ilivyoyaingiza kwenye akaunti na kuzisambaza kwa wanufaikaji wengine?

Umma unataka kusikia DPP, DCI na wote wanaohusika na uchunguzi kukamilisha kazi yao ya kuchunguza na kushitaki Kagoda na washirika wake. Sasa ielezwe basi wapi uchunguzi umefikia maana hakuna uchunguzi usiokamilika.

Haipo sababu ya kutengeneza mazingira ya kuionyesha Kagoda jitu lililoshindikana, badala yake taasisi za kiuchunguzi na mashitaka ziwajibike na kuthibitisha kazi ya maodita walioitaja Kagoda ni moja ya makampuni 22 yaliyochota EPA.

Si vizuri serikali kuachia ukungu kuzidi hata umma kuamini kuwa wapo wahalifu serikali inawaogopa. Yetu ni serikali ya Watanzania wenye akili na ujuzi wa kupambanua mambo.
 
Poisoned?

2009-02-08 11:29:17
By Guardian on Sunday team


As two opposition legislators detected spy gadgets in their hotel rooms in Dodoma this week, a lawyer who registered Kagoda company, is said to have been poisoned last week, casting a bleak future to where the country was heading as the war against corruption takes its pace.

corruption takes its pace. A Dar es Salaam-based lawyer, whose law firm spearheaded the registration of Kagoda Agricultural Co Ltd and dozens of other companies that swindled money from the Central Bank`s External Payment Arrears (EPA) account, was allegedly poisoned last week.

Bered Maregesi (31), a close associate of former Bank of Tanzania Governor Daudi Ballali and a man believed to have key clues about the ownership of Kagoda Company, was admitted to Mikocheni Hospital on January 26, just nine months after Ballali died mysteriously in US amid speculation that he had also been poisoned.

``Maregesi was brought here unconscious after thorough laboratory examination it was established that he was suffering from a poisonous substance,`` a doctor at the hospital who requested anonymity told The Guardian on Sunday.

Hospital records show that Maregesi was discharged on Thursday, after spending 11 days at the hospital recovering from the illness.

Doctors believe the poison must have been sprinkled in his food a few hours before he fell sick.

A nurse who was attending to Maregesi but who declined to be named because he is not an official spokesperson, told this newspaper on Friday that his patient was constantly vomiting and complaining of general body malaise and fever.

``His state worried us greatly. He looked entirely helpless and the whole medical team at his care was jolted,`` the nurse said.

``We have had hopeless situations before, but this one smacked of something unusual.``

A nursing officer added: ``A team of us (nurses) was keeping regular watch over this patient.

We could not tell whether he ate some food that was poisoned or not.

On the first days here it was all frustrating, but as days went by, he came to his senses, to our relief.``

Medical ethics prohibit doctors and nurses from releasing medical records to the public, and because of this particular clause they declined to reveal further findings from the laboratory tests.

``We can`t disclose which kind of poison or any further findings detected during laboratory examination without his prior permission,`` said a senior nursing officer who also declined to be named.

The doctor who did the diagnosis advised further laboratory tests to establish the extent to which the poison has spread in the patient`s system, although he prescribed medication that included anti-vomiting drugs, pain suppressing medicines and poison sucking agents.

Contacted on Friday, Maregesi said that he is not accusing anybody of poisoning him yet, but he hasn`t ruled out the possibility of foul play.

``I am puzzled,`` he said. ``My health condition is deteriorating but I don`t know who did this to me.``
``It might be a natural cause, because all human beings are subject to get sick, but I am at the crossroads,`` Maregesi told The Guardian on Sunday.

Maregesi said his doctors have advised him to seek further diagnosis abroad, but he can`t travel far because his passport is being held by the presidential taskforce formed to investigate the EPA scam.

``My doctor has told me that this is a complicated case that requires further medical examination abroad,`` he said. ``Hopefully I will make it soon, if God wishes.`

``I have submitted all evidence showing that I need to travel abroad for further treatment but I can’t travel without my passport,`` Maregesi said.
 
ajiwekee sumu ili iweje, kama njama za kwenda nje si angesingizia ugonjwa tu na serikali ingempeleka kama balali, sasa serikali inawasiwasi wa kujua ni nani atareveal ukweli kwa hiyo ahijuhi pa kushika na watu wote ambao wana angalau ideas nani ni nani basi wako kwenye hatari kubwa
 
Mkapa na Rostam watajwa
Peter Noni, Malegesi wamo

Na Saed Kubenea
Mwanahalisi~Maslahi ya Taifa Mbele
USHAHIDI wa kwanza na muhimu kwamba fedha zilizoibwa na Kampuni ya Kagoda kutoka Benki Kuu (BoT) uliidhinishwa na viongozi wakuu nchini, sasa umepatikana, MwanaHALISI limeelezwa.

Waraka wa wakili aliyeshuhudia mikataba ya Kagoda na makampuni mengine ya kupata fedha hizo, unamtaja rais mstaafu Benjamin Mkapa kuwa miongoni mwa waliofanikisha mpango huo.

Katika andishi rasmi kwa Kamati ya rais Jakaya Kikwete ya kushughulikia wizi kwenye akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), wakili huyo anakiri kuwa ni yeye alifanya attestation – "kushuhudia mikataba ya Kagoda na makampuni mengine ya nje."

Bhyidinka Michael Sanze, wakili katika kampuni ya mawakili ya Malegesi – Malegesi Law Chambers – ya Dar es Salaam, anasema katika andishi lake kuwa alishuhudia mikataba hiyo ndani ya ofisi za kampuni ya Caspian Construction Limited ambayo inamilikiwa na mfanyabiashara na mbunge wa Igunga, Rostam Aziz.


Aidha, kwa ushahidi wa Sanze, mbunge Rostam Aziz, ndiye kinara wa mpango mzima uliofanikisha wizi wa zaidi ya Sh. 40 bilioni kutoka BoT.

"Niliitwa na Bw. Malegesi ofisini kwa Bw. Rostam Aziz, 50 Milambo, Ofisi za Caspian Construction Limited. Nilipofika…niliwakuta Bw. Rostam Aziz, Peter Noni na Bw. Malegesi, wakaniambia fedha hizo zinahitajika kwa ajili ya kugharamia uchaguzi wa CCM na rais wake," ameeleza Sanze.

Wakili anaeleza kuwa alikuta "documents – nyaraka zimeshaadaliwa ambazo niliombwa nizi-sign (niziweke saini). Nikauliza hizo fedha zinakotoka na nitathibitisha vipi kabla ya kusaini."

Andishi la wakili linaeleza kuwa Rostan Aziz, Peter Noni na Bered Malegesi walimthibitishia Sanze kuwa Rostam alikuwa kwenye kikao ambako rais mstaafu Mkapa alitoa maelekezo kwa Gavana Ballali kutoa fedha hizo kwa Rostam kwa ajili ya uchaguzi.


Wakati huo Peter Noni alikuwa Mkurugenzi wa Mipango na Uchumi katika BoT. Hivi sasa ni Mkurugenzi wa Mpango ya Kimikakati. Ballali alikuwa gavana wa BoT. Alifariki dunia mwaka jana nchini Marekani.

Sanze anasema Malegesi aliishakwenda kujiridhisha kwa Ballali na Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Philip Mangula kuwa yaliyosemwa na Rostam yalikuwa kweli.

Hata hivyo Sanze anaongeza kuwa, "Rostam mwenyewe alisema, ‘system yote inajua.'" Anasema kwamba baada ya maelezo hayo ya Rostam, alishuhudia mikataba hiyo kwa kusaini.

Kwa mujibu wa andishi la Sanze ambalo linathibitishwa kwa saini yake, Malegesi alimwita Noni ofisini mwake baada ya jina la Sanze kutajwa magazetini akihusishwa na Kagoda, lakini aliambiwa kuwa "nitulie tu serikali inalishughulikia swala hilo."


Haya hivyo, Sanze anasema katika andishi hilo kuwa baada ya kumaliza kazi yake ya kushuhudia mikataba hakufuatilia kilichoendelea.

Hii ni mara ya kwanza Mkapa kutajwa katika sakata la kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, lakini ni mara nyingi Rostam amehusishwa na ukwapuaji huo ndani ya BoT.

Hata hivyo, haijathibitishwa iwapo kweli kulikuwa na kikao kinachomtaja Mkapa akiamuru gavana Ballali kutoa fedha kwa Rostam, kwani kauli ya Sanze inatokana maelezo ya Malegesi na Rostam Aziz; ama ukiwa ukweli au njia ya kumshawishi Sanze kushuhudia mikataba ya Kagoda.

Kwa miezi 15 sasa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekuwa kikikana kushiriki au kutumia fedha zilizotokana na wizi uliofanywa na Kagoda ingawa kimeshindwa pia kuthibitisha kilipopata mabilioni ya shilingi kugharamia kampeni zake ghali za uchaguzi mkuu wa 2005.

Katibu Mkuu Yusuph Makamba na Katibu Mwenezi John Chiligati wamekana chama chao kutumia fedha za EPA katika uchaguzi mkuu wa 2005. Wamesema kama kuna aliyechukua fedha hizo, basi hakutumwa na chama chao bali ni kwa matumizi yake binafsi.


MwanaHALISI liliwasiliana na wakili Sanze kupitia simu yake ya mkononi, likitaka kujua undani wa andishi lake. Sanze alimwambia mwandishi wa habari hizi, "Siwezi kujibu swali hilo."

Alipoulizwa kwa nini aliitwa na Malegesi kushuhudia mikataba wakati yeye Malegesi alikuwepo alisema, "Hilo muulize Malegesi mwenyewe."

Kuhusu kampuni yake kupata mgao na kuchangia CCM na kama kuna risiti inaonyesha walitoa mchango huo, Sanze alisema kwa ufupi, "Sijui lolote. Niambie wewe. Sijui zilitoka mwaka gani."

Alipong'ang'anizwa kuhusu kuchangia CCM alijibu, "Nikuulize wewe kama zilitoka lini."

Wakati wote simu ya Malegesi ilijibu kuwa haipatikani. Simu ya Rostam Aziz ilijibu pia kuwa hapatikani lakini ujumbe ulioandikwa na kumwomba awasiliane na mwandishi, ulionyesha kuwa umepokelewa. Hata hivyo, hadi tunakwenda mitamboni, Rostam hakuita.

Namba ya simu ya Mangula nayo ilisema kuwa hapatikani. Mwanasheria Mkuu wa serikali Johnson Mwanyika hakupatikana kuzungumzia andishi la Sanze.

Wiki iliyopita vyombo vya habari viliripoti kuwa 26 Januari mwaka huu, Malegesi alikula kitu kilichodaiwa kuwa sumu na kulazimika kulazwa hospitali ya Mikocheni, Dar es Salaam.

Uvumi ulioenea jijini Dar es Salaam unasema inawezekana Malegesi amelishwa sumu kwa makusudi kwa kuwa ni mtu muhimu katika sakata la Kagoda linalogusa watu wengi na wa nyadhifa mbalimbali.

Ni miezi tisa sasa tangu Daudi Ballali aage dunia kutokana na kile kilichodaiwa "kulishwa sumu" huku akieleweka kuwa mtuhumiwa mkuu au shahidi muhimu katika wizi mkubwa ndani ya BoT.


Gazeti la Nipashe Jumapili, 8 Februari 2009 limeandika kuwa Malegesi alitumia siku 11 hospitalini Mikocheni akipata matibabu ya kuondolewa sumu anayodaiwa kuipata kwenye chakuka.

Muuguzi mmoja aliliambia gazeti hilo kwamba hawawezi kutoa taarifa yoyote juu ya aina ya sumu au lolote walilobaini katika vipimo bila ruhusa ya mgonjwa mwenyewe.

Kampuni ya Kagoda ilikwapua zaidi ya Sh. 40 bilioni kutoka akaunti ya EPA, ikiwa ni wiki moja baada yakusajiliwa. Kampuni ilitawanya fedha hizo katika matawi saba ya Benki ya CRDB jijini Dar es Salaam.

Ni takriban mwaka mmoja sasa tangu rais aunde Kamati ya watu watatu kuchunguza wizi katika akaunti ya EPA, ikiongozwa na Mwanasheria Mkuu wa serikali Johnson Mwanyika. Wengine ni Mkurugenzi wa TAKUKURU, Edward Hosea na Inspekta Jenerali wa Polisi Saidi Mwema.

Haijafahamika iwapo wote ambao Sanze ametaja kwenye andishi lake walihojiwa na Kamati. Lakini taarifa zilizopo zinasema rais mstaafu Mkapa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Philip Mangula, hawajawahi kuhojiwa.

Mwishoni mwa mwaka jana, waandishi wa habari walimuuliza Waziri Mkuu Mizengo Pinda iwapo serikali inaogopa kukamata na kushitaki wahusika katika Kagoda; lakini alijibu kuwa, "Wahusika wote watafikishwa mahakamani."
 
Last edited:
...hivi uchunguzi bado unaendelea!? Wanataka tuamini uchunguzi ulioshindikana kwa timu iliyoundwa na Mwanzasheria mkuu, mkuu wa Jeshi la polisi na bosi wa Takukuru utakuwa unaendelea?

Kalaghabao
 
Rostam mbona hii yupo kimya, au alishalishtaki mwanahalisi tayari?
 
Wajameni hili ni dili la 'The King Maker'. Hata tupige kelele vipi, ni kelele za mlango, hazimnyimi usingizi mwenye nyumba.
Hiyo Tume ya Mwanyika inajua A-Z. Wenye zile accounts za benk ambapo fedha za Kagoda zilitawanywa wanajulikana. Andiko la Balali lenye kufichua kila kitu wanalo. Na mikataba ya 'caveat' kati ya BOT na Kagoda just incase things will go the other way round ipo.
Kwa kifupi issue ya Kagoda haiendi mahakamani hata kwa dawa.
Amini msiamini, kuna taasisi mbili tuu zenye mamlaka kubwa ya ajabu. Hizi ni Presidential na DPP tuu. Hata Bunge linajidai dai tuu, kila sheria wanayoipitisha haiwi sheria mpaka isainiwe na rais. Rais anaweza kuamua kulivunja Bunge wakati wowote as he pleases.
Hukumu kubwa kabisa katika mfumo wetu wa Sheria ni Capital Punishment (adhabu ya kifo). Mtu pekee mwenye madaraka ya utekelezaji adhabu hiyo ni rais pekee. Pia ana madaraka ya kusitisha hukumu yoyote ama kutoa msamaha kwa wafungwa.

Hiyo mtu mwingine mwenye madaraka ambayo hayaingiliwi na taasisi yoyote hata rais mwenyewe ni DPP. Huyu ana mamlaka ya kuamua 'Kagoda haina kesi ya kujibu' hata kama kuna ushahidi wa asilimia 100% na hakuna mamlaka yoyote yenye uwezo wa kuuliza sababu.
Pia DPP ana power to declare 'Nole Proseque', yaani hakuna kesi ya kujibu. Haya ni mamlaka ya kuingilia kesi yoyote ya jinai na kusema hakuna kesi. Hata PCCB ni cha mtoto mbele ya DPP, hawawezi kuendesha kesi yoyote bila kibali cha DPP na asipotoa kibali, hairuhusiwi kumuuliza sababu.

Hivyo hizi kelele za Kagoda tuendelee kuzipiga sana tuu, itafika wakati wapiga kele watapiga mchana na usiku watalala.
Tatazipiga wee..., tutapiga wee...
... hata 'ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ikapita'.
 
Kaaz kweli kweli kweli........ Duh, Kiwira, sijui Kagoda, sijui............... Waheshimiwa kule Dom, jamani ni kazi gani mnafanya na mnaona haya madudu yote yanaendelea kupeta tuuuuuuuu????
 
Mimi naona kama Serikali inatuzuga inaficha huh!au labda kuna watu wa juu ngazi za serikali
 
Kuwekwa kwa habari hii kwenye gazeti sasa kmeikisha suala hili kwenye hatua nzuri. Ndio maana wajuvi walikuwa wanasema wanaokamatwa ni vidagaa tu, mapapa wenyewe bado wanatesa. Slowly but surely tunaelekea kufahamu hasa EPA na mafia wake. Aliepiga filimbi ya kupambana na rushwa na ufisadi sasa imeanza konekana wazi kuwa he preached A and practiced Z!
 
Walijua MwanaHALISI alikuwa anaelekea huku nini ndio maana wakaamua kumtisha? Tusubiri tuone mwisho wa hii series, episode iliyofikia ni tamu(masterling wameanza kufahamika bayana), kiasi cha kutufanya tusubirie kinachoendelea.
 
Ninacho shukuru wananchi wanaelewa nini kilifanyika na nini kinaendelea kufanyika. Hapa JK anatakiwa asafishe wenzie kwanza halafu afuate yeye kwa sababu ni mhusika mkuuu pia.
 
Vigogo waanza kumalizana kimya kimya
HOFU imezidi kutawala kwa baadhi ya vigogo wa siasa, hasa kuwepo kwa taarifa za kulishwa sumu kwa baadhi ya vigogo na watu wanaoijua siri ya uanzishwaji wa Kampuni ya Kagoda Agricultural iliyochota sh bilioni 40 katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Mmoja wa wafanyabiashara na wanasiasa maarufu hapa nchini (jina tunalo), anadaiwa naye kulishwa sumu na mwenzake ambaye inasemekana amekuwa na siri nzito kuhusu uanzishwaji wa kampuni hiyo, mahali fedha zilipopelekwa na matumizi yake.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari cha Tanzania Daima Jumapili, kimesema kupewa sumu hiyo kunatokana na hofu waliyonayo baadhi ya vigogo kuwa kuna uwezekano mkubwa baadhi ya watu wakatoa siri kuhusu uchotwaji wa fedha.

Hofu hiyo imeongezeka zaidi hivi sasa baada ya kuwepo kwa taarifa za wakili maarufu hapa nchini, Beredi Maregesi, wa Kampuni ya Maregesi Law Chambers kulishwa sumu kama ile anayodaiwa kupewa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), marehemu Daudi Ballali, aliyefariki dunia mwaka jana huku akikabiliwa na shutuma nzito za uidhinishaji wa fedha za EPA kwa kampuni 22.
Ballali ambaye alilazimika kukimbilia nchini Marekani kwa matibabu, inadaiwa aliwahi kueleza kiini cha kuumwa kwake kuwa ni kupewa sumu na mwanasiasa mmoja ambaye inadaiwa kuwa ni miongoni mwa watu waliochota fedha BoT.

Taarifa ambazo Tanzania Daima Jumapili, imezipata zinadai hivi sasa baadhi ya wanasheria walioshiriki au kujua siri za Kagoda wamekuwa na wasiwasi mkubwa juu ya maisha yao, kutokana na mwenendo wa mambo ulivyo hivi sasa. Wakati wanasheria hao wakiwa na wasiwasi huo, kigogo wa siasa anayedaiwa kulishwa sumu hiyo inayofanya kazi taratibu, amekuwa akipata matatizo ya kiafya na huenda katika siku za hivi karibuni akapelekwa nje ya nchi kwa matibabu zaidi, baada ya hospitali za hapa nchini kuonekana kutokuwa na uwezo wa kumtibu.

Chanzo cha habari kimedai kuwa kama kweli kigogo huyo atakuwa amelishwa sumu hiyo, uwezekano wa kupona ni mdogo, kwani sumu hiyo huenda mbali zaidi kwa kuingia kwenye mifupa.

“Kama kweli amelishwa sumu ninayoijua, uponaji wake utakuwa mdogo, hata kama atapelekwa katika hospitali za nje,” kilisema chanzo hicho ambacho hakikutaka kutajwa jina lake.

Kigogo huyo inasemekana ndiye aliyekuwa na mipango imara ya kuwaokoa baadhi ya vigogo waliodaiwa kuhusika na Kampuni ya Kagoda ambayo katika siku za hivi karibuni wamiliki wake wametajwa lakini baadhi ya watu wanapinga kuwa si wamiliki halisi, bali ni kivuli cha vigogo wa siasa ambao walichukua fedha hizo kwa ajili ya kuwasaidia katika masuala yao ya siasa.

Baadhi ya wanasheria walio karibu na Maregesi wameweka bayana kuwa matumizi ya kijasusi, hasa ya kuwekeana sumu si mazuri na ni vema serikali ikachunguza madai hayo ili kubaini kama yana ukweli wowote kuliko kuyapuuza, kwa kudai kuwa huo ni uzushi.

Maregesi anadaiwa kuwa mtu wa karibu wa marehemu Ballali na anazijua siri nyingi, pamoja na mali za gavana huyo, jambo linalomfanya kuonekana mtu muhimu katika ushahidi endapo kampuni ya Kagoda ingefikishwa mahakamani.

Pamoja na wasiwasi huo wa kufikishwa mahakamani kwa Kampuni ya Kagoda, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe, wamekwisha kuweka bayana kuwa hawajapata ushahidi wa kutosha wa kuweza kuifikisha mahakamani Kampuni ya Kagoda.

Kagoda ni miongoni mwa kampuni 22 zilizochota kiasi cha sh bilioni 133 katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), ambapo mpaka sasa watuhumiwa 20 na kampuni zao wameshafikishwa mahakamani, huku Kagoda iliyochota kiasi cha sh bilioni 40 ikiwa haijafikishwa mahakamani kwa kile kinachodaiwa kutokuwapo kwa ushahidi wa kuiburuza mahakamani.
 
Jamani Kagoda Agriculture Lilmited in "NOLE PROSEQUE" haishitakiki hiyo!!!! Ni serikali yenyewe. Tutaumiza vichwa bure tu.
 
Fisadi atamalizwa na fisadi mwenzie. Acha wamalizane. Tunataka wauane wamalizane maana wametutesa sana. Nina hasira nao mimi we, acha tu.
 
Back
Top Bottom